Kanisa
lililoporomoka mjini Lagos wiki jana na kuwaua watu wengi, lilikuwa
linamilikiwa na mhubiri anayesifika sana nchini Nigeria, TB Joshua.
Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo anatufichulia haiba ya mhubiri huyu ambaye anadai amewaponya watu wakiwemo vipofu
na waathirika wa HIV.
TB Joshua
anadai kuwahi kutabiri matukio mengi kuanzia kwa kifo cha aliyekuwa
gwiji wa muziki, Michael Jackson, hadi kupotea kwa ndege ya Malaysia ya
MH370.
Anajiita mtume na ni mmoja wa wahubiri mashuhuri sana nchini Nigeria ambako makanisa kama lake ni mengi kupindukia.
Alizaliwa mwaka 1963 tarehe 12 Juni katika familia maskini, akidai kwamba alikaa kwenye tumbo la mamake kwa miezi 15.
Baadaye katika maisha yake, anadai kuona kwenye ndoto yake manabii wakimtaka kuhubiri na kufanya miujiza.
Hapo ndipo alipoanzisha kanisa lake analoiita, 'Church of All Nations (SCOAN),' mwanzoni likiwa na waumini 8.
'Maji ya kuponya'
Watu huja kwake kutoka kote duniani wakitaka kuombewa wapone.Hii leo Jushua kama wahubiri wengine nchini Nigeria, ni tajiri wa kupindukia akishabikiwa sana na watu nchini humo.
Wakati
ugonjwa wa Ebola uliporipotiwa katika kanda ya Afrika Magharibi,
serikali ya jimbo la Lagos, ilimtambua muhubiri huyo kwa kuambia
wagonjwa wa Ebola kwenda kwake akawaponye.
Alikubali
kuahirisha baadhi ya programu za kanisa lake za kuponya lakini
inaarifiwa alituma chupa 4,000 za maji ya ''uponyo' nchini Sierra Leone
anayosema kuwa yanatibu magonjwa mengi tu.
TB Joshua
anasema maji hayo ambayo yalitolewa kwa wagonjwa yakiwa ndani ya chupa
ndogo, ndogo, yanaweza kuwasaidia wagonjwa kupona na kupata baraka.
'Utabiri'
Katika
utabiri wake wa kifo cha Michael Jackson, TB Joshua aliwaambia waumini
wake: Katika maeneo yake mwenyewe kuwa yeye ni mashuhuri. "Najulikana
kila sehemu."
Anasifika,
kwa unabii wake, TB Joshua anadai kutabiri matukio mbali mbali kuanzia
kwa kifo cha marehemu Michael Jackson, hadi kupotea kwa ndege ya
Malaysia MH370.
''Kwa sababu
mwanzo huwa naona kwamba jambo litamtokea mtu fulani mashuhuri, na kitu
hicho kitamalizika, ila huwa sijui tu safari hiyo itakuwa lini. ''
Baada ya
kifo cha Michael Jackson, mhubiri huyo alidai kuwa alikuwa amezungumzia
kifo cha Jackson miezi sita kabla ya kutokea kwa kifo hicho.
Wakosoaji wake wanasema matamshi na utabiri wake ni wa kubahatisha.
Lakini hili halijawakosesha usingizi waumini wa kanisa lake.
TB Joshua ni mmoja wa wahubiri mashuhuri barani Afrika. Mwanasiasa
wa Afrika Kusini, Julius Malema, Rais wa Malawi Joyce Banda, na
mwanasiasa wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai na aliyekuwa Rais wa Ghana
John Atta Mills, ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao wamemtembelea.
Hata Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Edward Ngoyayi Lowassa, naye alikwenda huko mwaka 2009.
Baadhi
ya waumini wanadai kufaidika pakubwa kutokana na maombi yake, ni wale
wanaosema wameweza kufanikiwa kifedha, kupona na hata watu kufufuliwa.
Nabii Joshua pia anajulikana kwa kazi yake kwa jamii ambayo yeye hujitolea.
Wengi nchini Nigeria hata huhofia kumkosoa TB Joshua. (BBC/MAKALA).
(Nyongeza na Daniel Mbega)
Jina lake halisi anaitwa Temitope Balogun Joshua,
lakini anafahamika zaidi kama T.B. Joshua. Alizaliwa Juni 12, 1963 uko
Arigidi, Nigeria na anafahamika kama miongoni mwa watu 50 mashuhuri na
wenye ushawishi wa Afrika.
TB Joshua ni
miongoni mwa wahubiri watano matajiri nchini Nigeria, yeye akishika
nafasi ya tatu ambapo utajiri wake unakadiriwa kuwa kati ya Dola 10 - 15
milioni (takriban TShs. 16 - 24 bilioni) akiwa anamiliki kituo cha
luninga cha Emmanuel TV na kuuza itabu na kaseti nyingi za mahubiri yake
kwa njia ya mtandao. Ni rafiki mkubwa wa Rais wa Ghana John Atta Mills.
Mhubiri anayeongoza kwa utajiri nchini humo ni Askofu David Oyedepo wa kanisa la Living
Faith World Outreach Ministry, maarufu kama Winners Chapel
alilolianzisha mwaka 1981, ambalo linatajwa kuwa ndilo kubwa zaidi
barani Afrika kati ya makanisa ya Kipentekoste.
Hekalu
lake la Faith Tabernacle, ambapo huhudumia ibada tatu kila Jumapili,
ndilo hekalu kubwa zaidi la ibada barani Afrika likiwa na uwezo wa
kuingiza waumini 50,000 kwa wakati mmoja.
Anamiliki
ndege nne za binafsi na ana majumba London na Marekani. Anamiliki
kampuni ya uchapaji ya Dominion Publishing House, ambayo uchapisha
vitabu yake. Alianzisha na ndiye mmiliki wa Chuo Kikuu cha Covenant,
moja ya vyuo maarufu nchini Nigeria, na shule ya Faith Academy. Utajiri
wake kwa sasa ni Dola 150 milioni (takriban TShs. 240 bilioni).
Anayemfuatia
kwa utajiri ni Chris Oyakhilome wa kanisa la Believers’ Loveworld
Ministries, maarufu kama Christ Embassy. Utajiri wake ni kati ya Dola 30
- 50 milioni (takriban TShs. 48 - 80 bilioni).
Huyu bwana
aliwahi kuwa na kesi ya fedha haramu (money laundering) kiasi cha Dola
35 milioni ambapo alituhumiwa kuzoa fedha kutoka kanisani kwake na
kuzificha katika benki mbalimbali nje ya nchi. Hata hivyo, baada ya
utetezi, aliachiliwa huru.
Kanisa lake
la Christ Embassy lina wanachama 40,000, miongoni mwao wakiwa matajiri
wakubwa na wanasiasa. Anamiliki magazeti, majarida, kituo cha luninga,
kampuni ya kurekodi, kituo cha teleisheni cha satellite, hoteli na
biashara ya majumba. Kituo chake cha Loveworld TV Network ndicho cha
kwanza cha Kikristo kutangaza kwa saa 24 katika mataifa mengi
ulimwenguni.
Anayeshika
nafasi ya nne ni Matthew Ashimolowo wa kanisa la Kingsway International
Christian Centre (KICC), ambaye utajiri wake ni kati ya Dola 6 - 10
milioni.
Mwaka 1992,
kanisa la Foursquare Gospel Church la nchini Nigeria, lilimpeleka
Ashimolowo akafungue kituo cha satellite jijini London. Lakini Mchungaji
Matthew alikuwa na mawazo tofauti kichwani mwaka na badala yake akaamua
kuanzisha kanisa lake.
Leo hii
kanisa la Kingsway International Christian Center linatajwa kwamba ndilo
kanisa kubwa la Kipentekoste nchini Uingereza. Mwaka 2009, kanisa hilo
lilipata faida ya karibu Dola 10 milioni na rasilimali zenye thamani ya
Dola 40 milioni.
Mshahara
wake ni Dola 200,000, lakini utajiri wake hasa unatokana na biashara
zake nyingine, zikiwemo kampuni yake ya habari iitwayo Matthew
Ashimolowo media, ambayo inachapisha habari za Kikristo na vipindi vya
aina hiyo.
Mchungaji wa
tano kwa utajiri nchini Nigeria ni Chris Okotie wa kanisa la Household
of God Church, ambaye utajiri wake unakadiriwa kuwa kati ya Dola 3 - 10
milioni.
Huyu bwana
alipata umaarufu katika miaka ya 1980 wakati alipokuwa mwanamuziki wa
miondoko ya pop. Akashukiwa na neema, akaijua Biblia na kuanzisha kanisa
la Household of God Church, mojawapo ya makanisa maarufu Nigeria likiwa
na washirika 5,000 wakiwemo nyota wengi wa filamu kutoka Nollywood,
wanamuziki na watu wengine maarufu katika jamii.
Aliwahi
kuwania urais mara tatu lakini akashindwa kupitia kwenye chama chake
alichokianzisha cha Fresh Party. Anapenda matanuzi na anamiliki magari
ya kifarahi kama Mercedes S600, Hummer na Porsche