Wednesday, 24 September 2014

UFAHAMU UNDANI WA NABII TB JOSHUA AMBAYE KANISA LAKE LIMEUA WATU WENGI

Kanisa lililoporomoka mjini Lagos wiki jana na kuwaua watu wengi, lilikuwa linamilikiwa na mhubiri anayesifika sana nchini Nigeria, TB Joshua.
Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo anatufichulia haiba ya mhubiri huyu ambaye anadai amewaponya watu wakiwemo vipofu
na waathirika wa HIV.
TB Joshua anadai kuwahi kutabiri matukio mengi kuanzia kwa kifo cha aliyekuwa gwiji wa muziki, Michael Jackson, hadi kupotea kwa ndege ya Malaysia ya MH370.
Anajiita mtume na ni mmoja wa wahubiri mashuhuri sana nchini Nigeria ambako makanisa kama lake ni mengi kupindukia.
Alizaliwa mwaka 1963 tarehe 12 Juni katika familia maskini, akidai kwamba alikaa kwenye tumbo la mamake kwa miezi 15.
Baadaye katika maisha yake, anadai kuona kwenye ndoto yake manabii wakimtaka kuhubiri na kufanya miujiza.
Hapo ndipo alipoanzisha kanisa lake analoiita, 'Church of All Nations (SCOAN),' mwanzoni likiwa na waumini 8.
'Maji ya kuponya'
Watu huja kwake kutoka kote duniani wakitaka kuombewa wapone.Hii leo Jushua kama wahubiri wengine nchini Nigeria, ni tajiri wa kupindukia akishabikiwa sana na watu nchini humo.
Wakati ugonjwa wa Ebola uliporipotiwa katika kanda ya Afrika Magharibi, serikali ya jimbo la Lagos, ilimtambua muhubiri huyo kwa kuambia wagonjwa wa Ebola kwenda kwake akawaponye.
Alikubali kuahirisha baadhi ya programu za kanisa lake za kuponya lakini inaarifiwa alituma chupa 4,000 za maji ya ''uponyo' nchini Sierra Leone anayosema kuwa yanatibu magonjwa mengi tu.
TB Joshua anasema maji hayo ambayo yalitolewa kwa wagonjwa yakiwa ndani ya chupa ndogo, ndogo, yanaweza kuwasaidia wagonjwa kupona na kupata baraka.
'Utabiri'
Katika utabiri wake wa kifo cha Michael Jackson, TB Joshua aliwaambia waumini wake: Katika maeneo yake mwenyewe kuwa yeye ni mashuhuri. "Najulikana kila sehemu." 
Anasifika, kwa unabii wake, TB Joshua anadai kutabiri matukio mbali mbali kuanzia kwa kifo cha marehemu Michael Jackson, hadi kupotea kwa ndege ya Malaysia MH370.
''Kwa sababu mwanzo huwa naona kwamba jambo litamtokea mtu fulani mashuhuri, na kitu hicho kitamalizika, ila huwa sijui tu safari hiyo itakuwa lini. ''
Baada ya kifo cha Michael Jackson, mhubiri huyo alidai kuwa alikuwa amezungumzia kifo cha Jackson miezi sita kabla ya kutokea kwa kifo hicho.
Wakosoaji wake wanasema matamshi na utabiri wake ni wa kubahatisha.
Lakini hili halijawakosesha usingizi waumini wa kanisa lake.
TB Joshua ni mmoja wa wahubiri mashuhuri barani Afrika. Mwanasiasa wa Afrika Kusini, Julius Malema, Rais wa Malawi Joyce Banda, na mwanasiasa wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai na aliyekuwa Rais wa Ghana John Atta Mills, ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao wamemtembelea.
Hata Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Edward Ngoyayi Lowassa, naye alikwenda huko mwaka 2009. 
Baadhi ya waumini wanadai kufaidika pakubwa kutokana na maombi yake, ni wale wanaosema wameweza kufanikiwa kifedha, kupona na hata watu kufufuliwa.
Nabii Joshua pia anajulikana kwa kazi yake kwa jamii ambayo yeye hujitolea.
Wengi nchini Nigeria hata huhofia kumkosoa TB Joshua. (BBC/MAKALA).

(Nyongeza na Daniel Mbega)
Jina lake halisi anaitwa Temitope Balogun Joshua, lakini anafahamika zaidi kama T.B. Joshua. Alizaliwa Juni 12, 1963 uko Arigidi, Nigeria na anafahamika kama miongoni mwa watu 50 mashuhuri na wenye ushawishi wa Afrika.
TB Joshua ni miongoni mwa wahubiri watano matajiri nchini Nigeria, yeye akishika nafasi ya tatu ambapo utajiri wake unakadiriwa kuwa kati ya Dola 10 - 15 milioni (takriban TShs. 16 - 24 bilioni) akiwa anamiliki kituo cha luninga cha Emmanuel TV na kuuza itabu na kaseti nyingi za mahubiri yake kwa njia ya mtandao. Ni rafiki mkubwa wa Rais wa Ghana John Atta Mills.
Mhubiri anayeongoza kwa utajiri nchini humo ni Askofu David Oyedepo wa kanisa la Living Faith World Outreach Ministry, maarufu kama Winners Chapel alilolianzisha mwaka 1981, ambalo linatajwa kuwa ndilo kubwa zaidi barani Afrika kati ya makanisa ya Kipentekoste. 
Hekalu lake la Faith Tabernacle, ambapo huhudumia ibada tatu kila Jumapili, ndilo hekalu kubwa zaidi la ibada barani Afrika likiwa na uwezo wa kuingiza waumini 50,000 kwa wakati mmoja. 
Anamiliki ndege nne za binafsi na ana majumba London na Marekani. Anamiliki kampuni ya uchapaji ya Dominion Publishing House, ambayo uchapisha vitabu yake. Alianzisha na ndiye mmiliki wa Chuo Kikuu cha Covenant, moja ya vyuo maarufu nchini Nigeria, na shule ya Faith Academy. Utajiri wake kwa sasa ni Dola 150 milioni (takriban TShs. 240 bilioni).
Anayemfuatia kwa utajiri ni Chris Oyakhilome wa kanisa la Believers’ Loveworld Ministries, maarufu kama Christ Embassy. Utajiri wake ni kati ya Dola 30 - 50 milioni (takriban TShs. 48 - 80 bilioni). 
Huyu bwana aliwahi kuwa na kesi ya fedha haramu (money laundering) kiasi cha Dola 35 milioni ambapo alituhumiwa kuzoa fedha kutoka kanisani kwake na kuzificha katika benki mbalimbali nje ya nchi. Hata hivyo, baada ya utetezi, aliachiliwa huru. 
Kanisa lake la Christ Embassy lina wanachama 40,000, miongoni mwao wakiwa matajiri wakubwa na wanasiasa. Anamiliki magazeti, majarida, kituo cha luninga, kampuni ya kurekodi, kituo cha teleisheni cha satellite, hoteli na biashara ya majumba. Kituo chake cha Loveworld TV Network ndicho cha kwanza cha Kikristo kutangaza kwa saa 24 katika mataifa mengi ulimwenguni.
Anayeshika nafasi ya nne ni Matthew Ashimolowo wa kanisa la Kingsway International Christian Centre (KICC), ambaye utajiri wake ni kati ya Dola 6 - 10 milioni. 
Mwaka 1992, kanisa la Foursquare Gospel Church la nchini Nigeria, lilimpeleka Ashimolowo akafungue kituo cha satellite jijini London. Lakini Mchungaji Matthew alikuwa na mawazo tofauti kichwani mwaka na badala yake akaamua kuanzisha kanisa lake.
Leo hii kanisa la Kingsway International Christian Center linatajwa kwamba ndilo kanisa kubwa la Kipentekoste nchini Uingereza. Mwaka 2009, kanisa hilo lilipata faida ya karibu Dola 10 milioni na rasilimali zenye thamani ya Dola 40 milioni. 
Mshahara wake ni Dola 200,000, lakini utajiri wake hasa unatokana na biashara zake nyingine, zikiwemo kampuni yake ya habari iitwayo Matthew Ashimolowo media, ambayo inachapisha habari za Kikristo na vipindi vya aina hiyo.
Mchungaji wa tano kwa utajiri nchini Nigeria ni Chris Okotie wa kanisa la Household of God Church, ambaye utajiri wake unakadiriwa kuwa kati ya Dola 3 - 10 milioni. 
Huyu bwana alipata umaarufu katika miaka ya 1980 wakati alipokuwa mwanamuziki wa miondoko ya pop. Akashukiwa na neema, akaijua Biblia na kuanzisha kanisa la Household of God Church, mojawapo ya makanisa maarufu Nigeria likiwa na washirika 5,000 wakiwemo nyota wengi wa filamu kutoka Nollywood, wanamuziki na watu wengine maarufu katika jamii. 
Aliwahi kuwania urais mara tatu lakini akashindwa kupitia kwenye chama chake alichokianzisha cha Fresh Party. Anapenda matanuzi na anamiliki magari ya kifarahi kama Mercedes S600, Hummer na Porsche

No comments:

Post a Comment