Na Mathias Canal
Kama
unaweza kushiriki maombi haya pamoja nami, Mungu akukumbuke, na kama
upo kwa ajili ya kuhukumu, pia Mungu akukumbuke. Math7:1 Msihukumu msije
mkahukumiwa ninyi, kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayo
hukumuwa; na kipimo kile mpimiacho ndicho mtakacho pimiwa.
Math5:44 Lakini mimi nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi.
'
Mungu wewe ni Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu. wewe ni Mkuu sana, wewe
ni mwanzo tena mwisho zaidi yako hakuna na hatakuwepo. umesema
ktk 1wathesalonike5:18 shukuruni kwa kila jambo maana hayo ni mapenzi
ya Mungu kwenu ktk kristo Yesu. ahsante Mungu maana wewe uliijua jana
yangu, leo na kesho itakuwaje.Mungu wa amani unitakase kabisa nafsi
yangu, mwili wangu na roho yangu unihifadhi, wewe BWANA ni mwaminifu.
Ktk Isaya43;19 umesema,Tazama nitatenda neno jipya: sasa litachipuka je hamtalijua sasa? nitafanya njia hata jangwani na miito ya maji nyikani. BWANA mapenzi yako yatimizwe, tenda lililo kusudi lako juu yangu. ktk Math14:14 umesema, mkiniomba neno lolote kwa jina langu nitalifanya. ukasema ktk Marko10:27 Yesu akawakazia macho akasema, kwa wanadamu haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo: maana yote yanawezekana kwa Mungu.

Maombolezo3:31-32
Kwa kuwa BWANA hatamtupa mtu hata milele, maana ajapo mhuzunisha
atamrehemu kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.
Mungu inua moyo wangu sasa, wewe ndiyo msaada pekee wa kweli. Ninaamini utatenda makuu kama ilivyoandikwa ktk Zaburi 108;13 Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, maana yeye atawakanyaga watesi wetu. Bwana wewe ni mtu wa vita, Bwana ndilo jina lako,pigana sasa ninakuachia wewe.
ninashuka
mbele zako ninaungana na wenye uhai wanne ktk Ufunuo4;6-11 kukuabudu
wewe nikisema, 11 Umestahili wewe BWANA wetu na MUNGU wetu,kuupokea
utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwwe uliyeviumba vitu
vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako navyo vikaumbwa.Mungu inua moyo wangu sasa, wewe ndiyo msaada pekee wa kweli. Ninaamini utatenda makuu kama ilivyoandikwa ktk Zaburi 108;13 Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, maana yeye atawakanyaga watesi wetu. Bwana wewe ni mtu wa vita, Bwana ndilo jina lako,pigana sasa ninakuachia wewe.
Zab23;4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja nami.
AMEN
AMEN
No comments:
Post a Comment