Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma
HOJA ya
kusitisha Bunge Maalum la Katiba imehitimishwa rasmi Kisheria kwa
Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutamka kwamba bunge
hilo linaweza kuendelea na shughuli zake.
Taarifa
hiyo imetolewa jana 15 Septemba, 2014 na Mjumbe wa Kamati namba Tano,
Mhe. Dkt. Asha-Rose-Migiro wakati wa mjadala wa jioni bungeni hapo.
Akisoma
taarifa hiyo, Dkt. Migiro amesema kuwa mjadala wa kusitisha bunge
umefungwa rasmi hapo jana licha ya kuwepo kwa madai kuwa bunge hilo
halina uhalali wa kisiasa.
"Kwaajili
ya kuondoa shaka yoyote ningependa kuwaambieni takwimu tulizonazo hivi
sasa, bunge hili lina jumla ya Wajumbe 630, kati ya hao waliotoka ni
wajumbe 130 ambao ni sawa na asilimia 21% tu ya wajumbe wote, wajumbe
waliobaki ndani ya bunge ni 500 hii ni sawa na asilimia 79% ya wajumbe
wote na tukizichambua takwimu hizi, ningeomba kutambua wingi wa Kundi la
201", alisema Dkt. Migiro.
Akikanusha
juu ya kuwepo kwa dhana iliyojitokeza ya kwamba wajumbe waliobaki ndani
ya bunge hilo ni wa aina moja, Dkt. Migiro alisema kuwa taarifa hizo si
za kweli, kwani kati ya wajumbe 500 walioko ndani ya bunge hilo wajumbe
wanaotokana na kundi la 201 ni wajumbe 189 ambapo wajumbe wanaotoka
Tanzania bara jumla yao ni 348 na kati ya hao, 125 ni wajumbe wanaotoka
katika kundi hilo la 201.
"Ukitazama
takwimu hizi kwa jicho lolote lile basi wajumbe wa 201 ni sehemu kubwa
na ni sehemu muhimu ya wajumbe hawa waliobaki", alisema Dkt. Migiro.(Martha Magessa)
No comments:
Post a Comment