Monday, 30 June 2014

WANARIADHA WA TANZANIA WAENDELEA KUFANYA KUFURU



RTE1
RTE3
Wanamichezo waahidi kuleta medali katika mashindano ya Olympic yanayotarajia kuanza tarehe 23 Julai jijini Glasgow Scotland.
Akizungumza mara baada ya kuwasili nchini jana wakitokea Ethiopia Kocha wa Timu ya Riadha aliyeambatana na wachezaji 8 Bw. Shaban Hiiti alisema kuwa ana imani kubwa na wachezaji wake walioteuliwa katika Timu ya Taifa kuwa watailetea heshima Taifa kwa kuwa mazoezi waliyoyapata wakiwa nchini Ethiopia yamewajengea uwezo mkubwa.
Hiiki aliongeza kuwa walipokuwa nchi Ethiopia kwa mazoezi wamejifunza mbinu mbalimbali kutokana na kuwa na program za kuwajengea uwezo wachezaji wake.
“Nimatumaini yangu wachezaji hawa walioteuliwa kujiunga na wenzao waliokuwa mazoezini katika nchini zingine ambapo wanamichezo wetu walienda kwa ajili ya mazoezi wataliletea Taifa letu heshima kubwa kwani wamepikwa wakapikika”. Alisema Kocha huyo.
Aidha kocha huyo amesema kuwa uwepo mazingira mazuri na vifaa bora vya mazoezi kumechangia kwa kiasi kikubwa kuinua ubora wa wanariadha hao ambao wamefanya mazoezi kwa takribani miezi miwili nchini Ethiopia.
Kwa upande wake mmoja wa wanariadha ambaye amebahatika kuitwa kwenye kikosi kitakachoshiriki mashindano hayo Bw. Alphonce Felix amesema kuwa anajisikia faraja kuwa miongoni mwa wanamichezo watakao iwakilisha nchi katika mashindano ya Olympic kupitia mchezo wa riadha.
Alphonce amesema kuwa atatumia ujuzi alioupata nchini Ethiopia walipokuwa wameweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo.
Jumla ya wanariadha 9 na kocha wao waliweka kambi nchini Ethiopia ikiwa ni jitihada zinazofanywa na Serikali za kukuza na kuendeleza Sekta ya Michezo nchini kupitia mpango wa Diplomasia ya Michezo, ambapo wanamichezo mbalimbali wameweka kambi ambao wanamichezo wengine waliweka kambi katika nchi za Uturuki, China na New Zealand.(A.I).

HIZI NDIZO ATHARI ZA KUTAZAMA TV



Watu wanaotazama runinga kwa saa tatu au zaidi kila siku wako katika hatari ya kuaga dunia
mapema kuwaliko wale wanaotazama kwa muda mchache.
Hii ni kwa mujibu wa uchunguzi uliochapishwa katika jarida la the American Heart Association nchini Marekani.
"Utazamaji sana wa wa runinga ni tabia ya watu wasio na kazi ya kufanyatu na kuna ongezeko la mienendo ya kila aina ya tabia za kukaa tu," mtafiti mkuu Miguel Martinez-Gonzalez, profesa wa chuo kikuu cha Navarra iliyoko Pamplona, nchini Uhispania, alisema katika taarifa ya shirika hilo.
"Matokeo ya utafiti wetu ni sambamba na utafiti tuliowahi kufanya, ambapo muda unaotumiwa kutazama runinga uliolinganishwa na idadi ya vifo vinavyotokea kwa sababu hiyo."
Watafiti hao waliwachunguz vijana wachanga 13,284 kutoka Uhispania wenye afya na waliohitimu chuo kikuu kuhusu aina tatu ya tabia za kukaa tu na hatari ya kuaga dunia kutokana na sababu zote:muda wa kutazama runinga, muda wa kutumia tarakilishi na muda wa kuendesha gari.
'Sababu nyinginezo'
Vijana hao walioshiriki, ambao walikuwa na umri wa wastani wa miaka 37 na ambao asilimia 67 walikuwa wanawake, walifuatiliwa kwa takriban miaka 8.2. mwishowe, vifo 97 viliripotiwa, vikiwemo vifo 19 vilivyotokana na mishipa na moyo, 46 kutokana na saratani na mengine 32 vilivyotokana na sababu nyinginezo.
Utafiti huo ulionyesha hatari kubwa ya kuaga dunia ilikuwa mara mbili zaidi kwa washiriki walioripoti kutazama runinga kwa saa tatu au zaidi kwa siku ikilinganishwa na wale waliotazama kwa saa moja au chini ya saa.

Watu 19 waliripotiwa kufariki kutokana na kutizama TV kwa muda mrefu
Hatari hii mara mbili zaidi ilidhihirishwa pia baada ya kutoa hesabu ya safu kubwa ya vigezo vingine vinavyohusiana na hatari kubwa ya kuaga dunia.
Watafiti hao hawakupata ushirikiano kati ya muda unaotumiwa na mtu anapotumia tarakilishi au kuendesha gari na hatari kubwa ya kuaga dunia mapema kutokana na sababu zote.
Pia waliongezea kuwa utafiti zaidi unapaswa kufanywa ili kudhibitisha ni athari zipi zilizopo kati ya kutumia tarakilishi na kuendesha gari katika viwango vya vifo, na pia kutathmini taratibu za kibayolojia zinazoweza kueleza uhusiano huo.
"Watu wanapoendelea kuzeeka, tabia za kukaa tu zitaenea zaidi, hasa kutazama runinga, na hili litasababisha mzigo mkubwa katika ongezeko la matatizo ya kiafya yanayoambatana na kuzeeka," Martinez-Gonzalez alisema.
"Matokeo ya utafiti wetu yanapendekeza watu wazima wajihusishe katika mazoezi ya viungo, waache kukaa tu kwa muda mrefu, na wapunguze kutazama televisheni kwa zaidi ya saa mbili kila siku."
BBC

FACEBOOK YALALAMIKIWA NA WATUMIAJI WAKE



Mtandao wa Facebook umelaumiwa kwa kuwafanyia wateja wake utafiti wa kisaikolojia bila ya kuwajulisha.
Nia ya utafiti huo ilikuwa kujua kama wateja wake wamebadili tabia ya kuweka
picha na mawazo yao katika mtandao huo kutokana na kukasirishwa na tabia za baadhi ya watumiaji wenzao.
Utafiti huo uliohusisha takribani watumiaji 700,000 unaonyesha kuwa Facebook inacheza na taarifa za watumiaji wake ili kupata hisia zao katika kile wanachokiweka kwenye mtandao huo.
Hata hivyo mtandao wa Facebook umekanusha madai hayo na kwamba hakuna mtumiaji binafsi aliyelengwa na utafiti huo uliofanywa na mtandao huo kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Cornell na California.
"Ngoja tuuite utafiti kama Facebook wenyewe wanavyouita, lakini ni dalili za wazi za kushindwa kuzingatia maadili na nguvu ya kulinda haki za watumiaji wake" amesema Kate Crawford katika ukurasa wake wa Twitter.
Waziri wa kazi Jim Sheridan mjumbe wa bodi ya mawasiliano ameagiza uchunguzi kufanyikadhidi ya mtandao huo wa Facebook katika tuhuma hizi.
Hata hivyo Katherine Sledge Moore, Profesa wa Saikolojia katika chuo cha Elmhurst , Illinois amesema kwa jinsi ambavyo Facebook wamekuwa wakishughulika na taarifa za wateja wake makubaliano yaliyopo katika utafiti huo hadhani kama yapo nje ya hali ya kawaida.
Adam Kramer kutoka Facebook mmoja kati ya walioandaa taarifa ya utafiti huo anasema wanadhani kuwa ilikuwa mhimu kwao kutafiti mashaka yanayowakumba watumiaji hasa katika mawazo yanayowekwa na marafiki zao na jinsi yanavyowafanya wafikirie tofauti .
BBC
(MNYAMA)

ANGALIA ALICHOFANYIWA LUIS SUAREZ



WAZILI NYARANDU AZINDUA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII YA (SITE)



2a
4a
5a
Wageni wlikwa mbalimbali wakiangalia jinsi mabanda yatakayotumiwa na washiriki wa maonyesho yatakavyokuwa. 
(A.I).

Brazil yaponea kuaga mashindano

NEY_1343e.jpg
Brazil imeponea kung'olewa kutoka mashindano ya kombe la dunia yanayoendelea nchini humo.
Hii ni baada ya mechi ya kwanza ya mkondo wa muondoano kati yake na Chile kumalizika kwa mikwaju ya Penalti baada ya timu hizo mbili kwenda sare ya bao moja baada ya kipindi kizima cha mechi.
Na pia baada ya kucheza muda wa ziada.
Wakati wa mikwaju ya Penalti, Brazil iliingiza tatu huku Chile ikiingiza mbili.
Wakati wa mechi , Brazil iliingiza bao la kwanza la mechi ndani ya kipindi cha kwanza, lakini Chile ilileta jibu kabla ya kipindi cha kwanza cha mechi kukamilika.
Brazil ilikuwa na kibarua kigumu na shinikizo tele kutoka kwa mashabiki wa Brazil ambao walijaa uwanjani na pia kwa kuwa Brazil ni mwenyeji wa michuano hiyo ,matarajio ya wengi nchini Brazil ni kuwa wanatafanya vyema katika mashindano hayo.(E.L)

Wachezaji 7 wa Costa Rica hawana doa



Wachezaji 7 wa Costa Rica hawakutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini
Wachezaji saba wa Costa Rica waliolazimishwa na maafisa wa FIFA kupimwa mkojo punde baada ya ushindi wa kihistoria dhidi ya Italia wamedhibitishwa kuwa hakutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini.

Maafisa wa Afya na wale wa kuchunguzi utumiaji wa madawa ya kututumua misuli yaliyopigwa marufuku walliwavamia wachezaji punde baada ya ushindi huo mkubwa na kuwatenga hadi pale walipochukua mkojo kwa ajili ya kupima chembe chembe za damu .
Tukio hilo lilikuwa la kustaajabisha kwani timu hiyo ilikuwa baadhi ya timu zilizokuwa zimeshukiwa kutokana na mchezo wao mzuri.

Awali wachezaji kadha walilazimika kupimwa punde baada ya mechi ambayo Costa Rica iliizaba Uruguay mabao 3-1.
Mfumo huu wa kupima mkojo wa wachezaji punde baada ya mechi imeiwacha FIFA ikishtumiwa kwa kupendelea timu fulani kushamiri katika kombe la dunia huku timu ambazo hazikutarajiwa kunawiri zikishurutishwa kupimwa dawa za kututumua misuli zilizopigwa marufuku.
Aliyekuwa mchezaji wa wa Argentina Diego Maradona aliiunga shirikisho la soka la Costa Rica kuikashifu FIFA akisema mbinu hiyo mpya inalenga kuwazonga wachezaji na mawazo kabla ya kipute hicho kumalizika nchini Brazil.(A.I).

Sunday, 29 June 2014

Utoro BLW wakwamisha bajeti Z’bar



670_bd867.png
Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) limekwama kukaa kama kamati ya matumizi na vikao kwa mara ya tano tangu kuanza kujadili bajeti za mwaka wa fedha 2014/15 Mei 14 mwaka huu kutokana na tatizo la wajumbe kuwa watoro wa kuhudhuria vikao.
Hali hiyo imekuwa ikimlazimu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, Naibu Spika Ali Abdallah Ali na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mgeni Hassan Juma kushindwa kuitisha Kamati ya Matumizi kutokana na kutotimia akidi ya asilimia 50 ya wajumbe 40 kati ya wajumbe 82.
Tukio la aina hiyo lililotokea mwishoni mwa wiki baada ya Naibu Spika Ali Abdallah Ali kujikuta akiahirisha Baraza hilo kutokana na uchache wa wajumbe wakati wakijadili bajeti ya Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati iliyowasilishwa na Waziri Ramadhan Abdallah Shaaban.(P.T)

Watu zaidi 130 wahofiwa kufukiwa na kifusi


130927102302_indiamumbaibuildingapartmentcollapse_304x171_bbc_nocredit_82b33.jpg

Jengo la makazi laporomoka Mumbai, India
Maafisa nchini India wamesema wanahofu kuwa zaidi ya watu 130 wamenasa kwenye kifusi cha jengo lililoporomoka kusini mwa India,takriban Watu watano wameripotiwa kupoteza maisha katika tukio hilo mjini Porur.wengi wa walionasa wanaaminika kuwa wafanyakazi waliokuwa wakijenga jengo la ghorofa 11.

Kikosi ha uokoaji kinafanya jitihada za kuokoa walioathiriwa na ajali hiyo. siku ya jumamosi, watu 10 ,miongoni mwao watoto watano, walipoteza maisha mjini Delhi,baada ya jengo la makazi ya watu kuporomoka.

India imekua ikikumbwa na matukio ya kuporomoka kwa majengo, sababu ikielezwa kuwa usalama usio madhubuti na ujenzi usiozingatia viwango bora.

Mwezi Januari mwaka huu, takriban watu 14 walipoteza maisha baada ya jengo lililokuwa kwenye hatua za ujenzi kuporomoka katika jimbo la Goa.

Takriban watu 42 walipoteza maisha baada ya kuangukiwa na Jengo la ghorofa nne mjini Mumbai mwezi Septemba mwaka jana.CHANZO BBC,(A.I)

Van Gaal; Kopo la maji uwanjani ?


 
140623151406_van_gaal_wc2014_512x288_afp_nocredit_b590c.jpg
140618182130_van_persie_gaal_wc2014_512x288_afp_nocredit_74b89.jpg
Van Gaal kiwango cha joto ni juu mno
Kocha wa Uholanzi Louis van Gaal anatarajia shirikisho la soka duniani FIFA litawaruhusu wachezaji wake kunywa maji katika mechi yao ya raundi ya pili dhidi ya Mexico itakayochezwa katika uwanja wa Castelao ulioko katika eneo la Fortaleza.
Fortaleza ni eneo linaloshuhudia viwango vya juu vya nyuzi joto.
Kocha huyo wa Manchester United ya Uingereza anasema kuwa utafiti uliofanywa kabla ya mashindano haya yanasema kuwa wachezaji wanapoteza maji lita nne ama zaidi kwa kila mechi wanayocheza katika jimbo hilo la Fortaleza.
Ni dhahiri kuwa mwili wa binadamu yeyote unastahili maji kwa hivyo hawa wachezaji naamini kuwa wanastahili kunywa maji ilikuzuia wasishikwe na kisunzi .
Van Gaal alitishia kuwapa wachezaji wake maji kwa wingi kando kando mwa uwanja iwapo FIFA haitahalalisha kuwepo kwa dakika moja au mbili ambapo mechi zitasimamishwa iliwachezaji wake wapige kopo la maji.
Kiungo wao Leroy Fer, ambaye anauguza jeraha la goti anasema kuwa Uholanzi ilipata kionjo tu cha kucheza katika hali ya kiwango cha juu mno cha joto baada ya kuwasili huko wakitoka Rio de Janeiro.
Fer anasema kuwa japo Uholanzi imezoea kucheza katika maeneo ya Uropa yenye baridi kali,Uholanzi itajikaza kisabuni kwani ni hali ileile itakayoikumba timu pinzani ya Mexico.(A.I).

BARUA TOKA KWA MUME WA FROLA MBASHA KWENDA KWA MCHUNGAJI


Topic: Barua kutoka kwa mume wa
flora mbasha kwenda kwa mchungaji
gwajima
Page 1 of 2 1
BONGOLALA 20:54 Today
"Mchungaji ...yapata kama wiki mbili
zilizopita nilihoji kupitia vyombo vya
habari juu ya ‘utajiri' wa ghafla wa
mkewangu Mara baada ya mgogoro
kutokea kati yangu na yeye, bila
kupoteza muda mkewangu akanijibu
kupitia gazeti moja la udaku kuwa
amechangiwa fedha kiasi cha milioni 9
na waumini kanisani kwako.
Mchungaji, naomba uelewe kuwa
nafahamu juu ya mipango yote
mnayoipanga kuliko unavyodhani!!
Kwanza ni kweli kuwa mlipitisha
harambee ya kumchangia mkewangu,
lakini kiwango kilichopatikana kilikuwa ni
milioni 2 na laki tatu na si milioni tisa
kama mlivyotangaza!! Lakini mlitangaza
uongo huo makusudi iwe rahisi kutimiza
malengo yenu ya kidhalimu
mliyoyapanga juu yangu!!
Mnamo tarehe 3 mwezi juni mwaka
huu, mlifungua akaunti mpya kwa jina la
mkewangu katika benki ya crdb
morogoro, na siku nne baadae
mkewangu aliingiziwa fedha kiasi cha
milioni 18 kutoka akaunti ya
MWANAMAPINDUZI FOUNDATION
ambayo hyo accnt ipo nmb mwanza!
Ambapo asasi hii inamilikiwa na
mchungaji wako msaidizi Maximilian
Machumu pamoja na mbunge wa viti
maalumu kutoka mikoa ya kaskazini!
Nashukuru kama ulimpa fedha hizi kwa
nia ya kumsaidia, lakini hofu yangu ni
kuwa kwanini kitendo hiki kifanyike kwa
kificho?? Kwanini mtumie njia za siri
ambazo si rahisi watu kujua kama
mmempa fedha??
Pia napatwa na mashaka zaidi kwani siku
moja baada ya fedha hizi kuingizwa
taarifa ya benki inaonyesha kuwa kiasi
cha milioni sita cash zilitolewa na siku
hiyo hiyo wapo waandishi watatu wa
magazeti ya udaku ambao wanaonekana
waliingiziwa fedha kiasi cha milioni moja
kila mtu na aliyedeposit hizo fedha ni
moja ya viongozi wako hapo kanisani!!
Kuna nini hapo??
Mchungaji, naomba tusizunguke mbuyu!
Ni dhahiri shahiri kuwa umekuwa na
uhusiano wenye utata na mkewangu
kwa muda mrefu sasa!
Binafsi nilianza kupata wasiwasi mwaka
jana mwezi desemba tulipoenda katika
mkutano wako wa injili pale morogoro!
Mimi na mkewangu tulifikia hoteli ya
kingsway msamvu na wewe ulifikia
Nashera Hotel maeneo ya forest hill!!
Baada ya siku tatu za mahubiri mkutano
wako ulipigwa marufuku na serikali
kwasababu ya maneno yakichochezi
uliyokuwa unahubiri, hvyo ikatulazimu
waimbaji wote turejee dar es salaam!!
Lakini uliniomba mkewangu abaki na
wewe kwani ulipanga uwe unawafanyia
watu maombi pale kanisani kwako
kihonda kwa muda wa siku nne!!
Nilikubali na nikamuacha mkewangu
nyumbani kwa dada yako pale
mazimbu!! Lakini kesho yake dada yako
alisafiri kwenda mwanza na ikabidi
mkewangu arudi hotelini kingsway!!
Kwaa taarifa nilizonazo na
nimezithibitisha kupitia wahudumu wa
pale hotelini ni kuwa mkewangu
hakuwahi kulala pale hata siku moja
ingawa chumba kililipiwa kwa siku zote
zile!! Unaweza kunijibu alikuwa analala
wapi?? Je unaweza kunieleza kwanini
mkewangu alikuwa analetwa nashera
hoteli na taxi kila siku usiku!!
Sibahatishi katika hili kwani hata namba
ya dereva taxi ninayo!!
Yote haya nilivumilia, na hapa kati kati
kuna mengi sana yametokea lakini
nikajifanya mjinga nikajishusha
nikavumilia kwa lengo la kulinda ndoa
yangu isiharibike lakini naona wenzangu
hambadiliki wala hamjishitukii sana sana
mapenzi ndio yanzidi kuwa motomoto
kati yenu!! Ulikuwa unategemea
nivumilie mpaka lini, nijishushe kiasi
gani, niwe mjinga kiasi gani Nilikuvumilia
sana mchungaji lakini sasa imefika point
hapana, imetosha lazima nikuondelee
uvivu watanzania na dunia ikufahamu
jinsi ulivyo na kitendo ulichonifanyaia na
unataka kuniziba mdomo kwa kunitishia
jela miaka 30!!!
Wewe ni mpuuzi na shetani anaishi
ndani yako... na nataka nikuahidi kitu
kimoja kuwa NITAKUSHINDA! Najua
utanisumbua sana kutokana na hela
zako but at the end, I will be the last
man standing!! Narudia tena,
nitakushinda.!!
Bila kusahau naomba niongee na wewe
pia mkewangu, hivi ni nini kilichokukuta
ndani ya moyo wako How did we get
here?? Je ni fedha zilizokufanya
ukengeuke kiasi hicho au kuna kingine??
Kama unanichukia mimi kiasi hiki je,
uwahurumii hata watoto wetu?? Mbona
tunawatengenezea mikosi wakiwa
wadogo hivi?? Hivi unadhani watoto
wanajisikiaje watakaposikia kuwa baba
ameenda jela kwa kosa la kubaka lakini
aliyechongesha muvi yote hiyo ni
mama?? Hivi kisaikolojia hawa watoto
watakuwaje Si watakuwa huku
wanatuchukia sisi wote wawili kwa aibu
na mikosi hii tunayowatengenezea
Kwanini tunataka kuwataabisha watoto
kwa dhambi ambayo hawajaitenda
Yes nafahamu nimekukosea mengi and
am very sory for that, lakini basi embu
kumbuka mkewangu nimekuvumilia
mambo mangapi mkewangu, kumbuka
makosa mazito uliyonifanyia lakini
nikakusamehe ni sijamsimulia hata
ndugu yako ama ndugu yangu ili kulinda
heshima yako!! Kumbuka jinsi
tulivyopogana na changamoto
mbalimbali mpaka leo hii umefikia kuwa
moja ya icons wa muziki wa injili hapa
nchini?? Kumbuka shida, manyanyaso,
dhuluma, kuchekwa na kudharauliwa
ambako tumepitia mpaka leo hii tuko
hapa!!!
Mkewangu, kwa miaka yote hii
nimekubali nionekane bushoke tu huku
watu hawajui kuwa mimi ndiye
ninayechora ramani ya kila ishu yako!!
Mimi ndiye nimekuwa nafatilia na
kufanikisha kila kitu chako from
scratch!!!
Lakini nimekubali jamii inione bushoke
kwani nilikuwa najua nini mimi na wewe
tunatengeneza kwa maisha yetu ya sasa
na baadae!!! Nini kilichokubadilisha
mkewangu Fedha Au huyo mchungaji
mwanamazingaombwe
Hivi kweli kabisa umefikia hatua ya
kulipa waandishi wa habari ili
wanikandamize nionekane sifai katika
jamii Ni nini kilichokuoata mkewangu??
Naomba uelewe kuwa binafsi siogopi
kwenda jela kwasababu ya hiyo muvi
mliyonizushia, kwani ni bora nikakae jela
kuliko kuishi huru huku mkininyanyasa
kiasi cha kuondoa utu wangu kama
bidamu, lakini kinachoniuma ni familia
yetu!! Kwanini watoto wateseke kwa
sababu ya tamaa zetu binafsi!! Nikifikiria
hilo naumia sana!
Najua kwa sasa inaonekana kama vile ni
impossible kwa mimi na wewe
kurudiana tena, lakini binafsi naamini
tunaweza!! Najua haitakuwa rahisi
kwani tumeharibu mno, lakini ni heri ya
kujaribu kuliko kuendelea kufanya huu
upuuzi tunoufanya sasa!!
Kumbuka hiki tunachokifanya sasa
hatujajipaka matope sisi tu pekee, bali
mziki wote wa injili Tanzania, na
tusipotubu tukajirudi Mungu
atatuhukumu kwa dhambi hii!!
Kumbuka kuwa hakuna kati yenu
atakayeshinda katika hii vita, vyombo
vya habari pekee ndivyo vitakavyo
nufaika lakini mimi, wewe na mchungaji
wote tuta loose!!
Mwisho nimalizie na wewe mchungaji,
tulipokutana mara ya kwanza
nilikuchukulia kama kaka na kama mlezi
wetu wa kiroho!! Lakini umegeuka
shetani mwenye pembe saba,
umeparaganyisha familia yangu,
umeleta maumivu makali kwenye
ukoo!!
Nakuonya tena kwa mara nyingine,
muache mkewangu!! Huyo ni
mkewangu, nilimtolea mahali mimi
mwenyewe na wazazi wake waliniamini
na kunikabidhi!!! Nasema niachie
mkewangu!!
Wewe ni nyoka, imefika time
watanzania wakujue ukweli wako wewe
mbwa mwitu mkali uliyevaa ngozi ya
kondoo!!!
Umedanganya watu vya kutosha na
umefarakanisha ndoa nyingi sana kwa
sababu ya kiburi cha pesa zako chafu za
sembe!! Umeudhalilisha ulokole kiasi
cha kutosha imefika time tuwaeleze
watanzania ukweli na wakufahamu kuwa
wewe ni nyoka!!
Sitakubali kuona ukiendelea kuitesa
familia yangu, nitapambana na
nitakushinda!!! Siogopi fedha zako wala
connection ulizonazo, ni bora nife
nikiwa nimesimama kuliko kuishi
nimepiga magoti!
Nitapambana na wewe mpaka mwisho
ili historia isomeke vizuri ili hata
wanangu wakiwa wakubwa wajue kuwa
baba yao sikuwa lofa kiasi cha kupiga
magoti na kuelekeza shingo kibla
kuruhusu mdhalimu kama wewe
uichinje familia yangu, bali licha ya
umasikini wangu nilisimama kiume na
kupigana kutetea familia yangu!!!
Narudia tena mchungaji, nitapambana
na nitakushinda.."

Saturday, 28 June 2014

KONDORO AKERWA NA WAPENDA POROJO BADALA YA KAZI


 Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, akipimwa shinikizo la damu, kisha akaenda kupima wingi wa sukari mwilini. Zoezi hilo lilifanyika katika Hospitali ya mkoa wa Mbeya, ambako kulikuwa na Mkutano wa viongozi, ulioandaliwa na Bima ya Afya.


 Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, Charles Kajege, akizungumza neno mbele ya viongozi waliokuwa wamehudhuria, wakiwemo wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Mbeya.
 Baadhi ya wenyeviti wa Halmashauri za mkoa wa Mbeya, wakisikiliza.
 Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, Charles Kajege.
 Wakuu wa wilaya za Ileje na Kyela mkoani Mbeya, wakisikiliza na kufurahia...
 Mkuu wa wilaya ya Rungwe, akifurahia jambo baada ya kutaniwa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, ambaye aliuwa mgeni rasmi.
 Wakuu wa wilaya za Mbarali na Mbozi.
 Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Dr. Norman Sigalla.
 Picha ya pamoja kati ya viongozi wa Bima ya Afya, Mkuu wa mkoa wa Mbeya na wakuu wa wilaya za Mbeya. Kisha zikafuata picha zingine za pamoja.



 Meneja wa NHIF Mkoa wa Mbeya, Dr. Mohamed Kilolile(kushoto), wakiwa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro baada ya kufungua mkutano huo.
 Baadhi ya waganga wakuu wa Hospitali za wilaya za mkoa wa Mbeya.
 Meneja Matekelezo wa NHIF makao makuu, Grace Lobulu, ambaye alimwakilisha Naibu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, akitoa mada.
 Afisa wa NHIF Mbeya.
  Meneja wa NHIF Mkoa wa Mbeya, Dr. Mohamed Kilolile, akizungumza jambo katika mkutano wa CHF kwa viongozi wa mkoa wa Mbeya wakiwemo Wakuu wa wilaya za Mbeya, Wakurugenzi, waganga wakuu, Wenyeviti wa Halmashauri na wenyeviti wa bodi za afya za halmashauri, ulioandaliwa na Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa,  (NHIF).
 
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, akifungua mkutano wa CHF kwa viongozi wa mkoa wa Mbeya wakiwemo Wakuu wa wilaya za Mbeya, Wakurugenzi, waganga wakuu, Wenyeviti wa Halmashauri na wenyeviti wa bodi za afya za halmashauri, ulioandaliwa na Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa,  (NHIF).
Na Gordon Kalulunga, Mbeya
MKUU wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, amewataka watanzania kuacha maneno badala yake waheshimu muda na kufanya kazi kama wananchi wa nchini China.
Hayo aliyasema jana katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya mkoa wa Mbeya, wakati akifungua mkutano wa CHF kwa viongozi wa mkoa wa Mbeya wakiwemo Wakuu wa wilaya za Mbeya, Wakurugenzi, waganga wakuu, Wenyeviti wa Halmashauri na wenyeviti wa bodi za afya za halmashauri, ulioandaliwa na Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa,  (NHIF).
Alisema aliposafiri kwenda nchini China, alikutana na hali tofauti na hapa nchini, ambapo wananchi wa China wanajali zaidi muda na kazi na uchaguzi ukiisha hawashughuliki na siasa.
“Ndugu zangu hatutafika tukiendekeza siasa kwa kila jambo na kwa kila wakati. Tuanze sasa kufanya kazi ili kusonga mbele kimaendeleo. Sisi tunapenda sana kusema sema, jambo la dakika mbili mtu anasema kwa dakika kumi’’ alisema Kondoro.
Mbali na jambo hilo, alisema katika kutekeleza lengo la kufikia asilimia 30 ya watanzania kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF), ni lazima yapigwe vita manung’uniko na ubaguzi kutoka kwa watoa huduma kwenda kwa waliojiunga na CHF.
Alisema wananchi wanaonekana kana kwamba wanapata huduma hizo bure bila kugharamia, dawa hazipatikani na zile wanazopaswa kupatiwa hazitolewi.
Kuhusu vifaa tiba, alisema wananchi waliojiunga na mfuko huo wa bima ya afya ya jamii na ile ya Taifa, wanapopata matatizo hawapati huduma na wanapotoka katika hospitali huwa hawawi mabalozi wazuri wa mfuko huu.
“Lengo la kukutana leo hapa ni kuondoa malalamiko ya wananchi kwa kutekeleza vema utaratizu wa bima ya afya kwa kuboresha huduma na kutoa elimu kwa wananchi ili wajiunge na CHF huku tukihakiksha huduma bora zinatolewa kwa walijiunga ili wawe mabalozi wazuri kwa ambao bado hawajaingia’’ alisema.
Kuhusu mfuko wa KfW, alisema ni mradi mzuri ambao unalenga kupunguza vifo vya mama na mtoto ili kutekeleza malengo ya milenia kufikia mwaka 2015 na kwamba tayari kwa mkoa wa Mbeya, wanawake 70,000 wamejiunga.
Aliwaagiza viongozi wa mkoa na wilaya kufanya ajenda ya kujiunga na CHF kuwa ya kudumu katika vikao vyote, watoa huduma kutoa huduma bila ubaguzi kwa wanachama wa bima ya afya ambao wanalalamika kuwa ni kama wanapata tiba bure na ni watu wa daraja la tatu na kupeleka mipango hiyo ngazi za chini za serikali ili wananchi wapate elimu.
Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, Charles Kajege, alisema lengo la mkutano huo na viongozi hao, ni kuhakikisha viongozi hasa wakuu wa wilaya kupanga mipango ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma zkiwemo dawa kwa wanachama wa CHF.
“Fedha zipo nyingi kwenye mfuko wetu kwa ajili ya dawa na vifaa tiba, leteni maombi ya mahitaji, tutawapeni ili wananchi wapate huduma’’ alisema Kajege.
Meneja Matekelezo wa NHIF makao makuu, Grace Lobulu, ambaye alimwakilisha Naibu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, alisema kuwa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ulianza rasmi jukumu la kusimamia mfuko wa Afya ya Jamii(CHF), Kitaifa mwezi Julai 2009.
Meneja wa NHIF Mkoa wa Mbeya, Dr. Mohamed Kilolile, alizitaja sababu za kuanzishwa kwa CHF kuwa ni Kushirikisha jamii kutoa mawazo yao ili kuboresha huduma za afya kupitia mikutano na kamati mbalimbali watakazozichagua wao wenyewe.
“Kuiwezesha jamii kumiliki hudum za Afya zinazowahusu katika maeneo wanayoishi na kuboresha huduma za matibabu kupitia utaratibu rahisi na nafuu wa uchangiaji kwenye mifuko ya bima ya jamii’’ alisema Dr. Kilolile.

Magazeti leo Jumamosi


01_293fb.jpg
1_6bf02.jpg
2_17cca.jpg
3_b3f7e.jpg
4_c29bd.jpg
5_79cc9.jpg
6_9e021.jpg
7_3c499.jpg
8_bb8a2.jpg
10_4ea23.jpg
11_6f628.jpg
12_dcd24.jpg
13_50ae0.jpg
14_bc0b4.jpg
15_44a03.jpg
16_17d06.jpg
017_a0d29.jpg
17_515f5.jpg
18_0ef9f.jpg
IMG-20140628-WA0007_e7603.jpg
IMG-20140628-WA0009_f1a30.jpg
IMG-20140628-WA0010_8a005.jpg
IMG-20140628-WA0016_9d41a.jpg
IMG-20140628-WA0020_3ff5a.jpg