Saturday, 28 June 2014

KONDORO AKERWA NA WAPENDA POROJO BADALA YA KAZI


 Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, akipimwa shinikizo la damu, kisha akaenda kupima wingi wa sukari mwilini. Zoezi hilo lilifanyika katika Hospitali ya mkoa wa Mbeya, ambako kulikuwa na Mkutano wa viongozi, ulioandaliwa na Bima ya Afya.


 Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, Charles Kajege, akizungumza neno mbele ya viongozi waliokuwa wamehudhuria, wakiwemo wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Mbeya.
 Baadhi ya wenyeviti wa Halmashauri za mkoa wa Mbeya, wakisikiliza.
 Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, Charles Kajege.
 Wakuu wa wilaya za Ileje na Kyela mkoani Mbeya, wakisikiliza na kufurahia...
 Mkuu wa wilaya ya Rungwe, akifurahia jambo baada ya kutaniwa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, ambaye aliuwa mgeni rasmi.
 Wakuu wa wilaya za Mbarali na Mbozi.
 Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Dr. Norman Sigalla.
 Picha ya pamoja kati ya viongozi wa Bima ya Afya, Mkuu wa mkoa wa Mbeya na wakuu wa wilaya za Mbeya. Kisha zikafuata picha zingine za pamoja.



 Meneja wa NHIF Mkoa wa Mbeya, Dr. Mohamed Kilolile(kushoto), wakiwa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro baada ya kufungua mkutano huo.
 Baadhi ya waganga wakuu wa Hospitali za wilaya za mkoa wa Mbeya.
 Meneja Matekelezo wa NHIF makao makuu, Grace Lobulu, ambaye alimwakilisha Naibu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, akitoa mada.
 Afisa wa NHIF Mbeya.
  Meneja wa NHIF Mkoa wa Mbeya, Dr. Mohamed Kilolile, akizungumza jambo katika mkutano wa CHF kwa viongozi wa mkoa wa Mbeya wakiwemo Wakuu wa wilaya za Mbeya, Wakurugenzi, waganga wakuu, Wenyeviti wa Halmashauri na wenyeviti wa bodi za afya za halmashauri, ulioandaliwa na Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa,  (NHIF).
 
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, akifungua mkutano wa CHF kwa viongozi wa mkoa wa Mbeya wakiwemo Wakuu wa wilaya za Mbeya, Wakurugenzi, waganga wakuu, Wenyeviti wa Halmashauri na wenyeviti wa bodi za afya za halmashauri, ulioandaliwa na Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa,  (NHIF).
Na Gordon Kalulunga, Mbeya
MKUU wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, amewataka watanzania kuacha maneno badala yake waheshimu muda na kufanya kazi kama wananchi wa nchini China.
Hayo aliyasema jana katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya mkoa wa Mbeya, wakati akifungua mkutano wa CHF kwa viongozi wa mkoa wa Mbeya wakiwemo Wakuu wa wilaya za Mbeya, Wakurugenzi, waganga wakuu, Wenyeviti wa Halmashauri na wenyeviti wa bodi za afya za halmashauri, ulioandaliwa na Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa,  (NHIF).
Alisema aliposafiri kwenda nchini China, alikutana na hali tofauti na hapa nchini, ambapo wananchi wa China wanajali zaidi muda na kazi na uchaguzi ukiisha hawashughuliki na siasa.
“Ndugu zangu hatutafika tukiendekeza siasa kwa kila jambo na kwa kila wakati. Tuanze sasa kufanya kazi ili kusonga mbele kimaendeleo. Sisi tunapenda sana kusema sema, jambo la dakika mbili mtu anasema kwa dakika kumi’’ alisema Kondoro.
Mbali na jambo hilo, alisema katika kutekeleza lengo la kufikia asilimia 30 ya watanzania kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF), ni lazima yapigwe vita manung’uniko na ubaguzi kutoka kwa watoa huduma kwenda kwa waliojiunga na CHF.
Alisema wananchi wanaonekana kana kwamba wanapata huduma hizo bure bila kugharamia, dawa hazipatikani na zile wanazopaswa kupatiwa hazitolewi.
Kuhusu vifaa tiba, alisema wananchi waliojiunga na mfuko huo wa bima ya afya ya jamii na ile ya Taifa, wanapopata matatizo hawapati huduma na wanapotoka katika hospitali huwa hawawi mabalozi wazuri wa mfuko huu.
“Lengo la kukutana leo hapa ni kuondoa malalamiko ya wananchi kwa kutekeleza vema utaratizu wa bima ya afya kwa kuboresha huduma na kutoa elimu kwa wananchi ili wajiunge na CHF huku tukihakiksha huduma bora zinatolewa kwa walijiunga ili wawe mabalozi wazuri kwa ambao bado hawajaingia’’ alisema.
Kuhusu mfuko wa KfW, alisema ni mradi mzuri ambao unalenga kupunguza vifo vya mama na mtoto ili kutekeleza malengo ya milenia kufikia mwaka 2015 na kwamba tayari kwa mkoa wa Mbeya, wanawake 70,000 wamejiunga.
Aliwaagiza viongozi wa mkoa na wilaya kufanya ajenda ya kujiunga na CHF kuwa ya kudumu katika vikao vyote, watoa huduma kutoa huduma bila ubaguzi kwa wanachama wa bima ya afya ambao wanalalamika kuwa ni kama wanapata tiba bure na ni watu wa daraja la tatu na kupeleka mipango hiyo ngazi za chini za serikali ili wananchi wapate elimu.
Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, Charles Kajege, alisema lengo la mkutano huo na viongozi hao, ni kuhakikisha viongozi hasa wakuu wa wilaya kupanga mipango ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma zkiwemo dawa kwa wanachama wa CHF.
“Fedha zipo nyingi kwenye mfuko wetu kwa ajili ya dawa na vifaa tiba, leteni maombi ya mahitaji, tutawapeni ili wananchi wapate huduma’’ alisema Kajege.
Meneja Matekelezo wa NHIF makao makuu, Grace Lobulu, ambaye alimwakilisha Naibu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, alisema kuwa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ulianza rasmi jukumu la kusimamia mfuko wa Afya ya Jamii(CHF), Kitaifa mwezi Julai 2009.
Meneja wa NHIF Mkoa wa Mbeya, Dr. Mohamed Kilolile, alizitaja sababu za kuanzishwa kwa CHF kuwa ni Kushirikisha jamii kutoa mawazo yao ili kuboresha huduma za afya kupitia mikutano na kamati mbalimbali watakazozichagua wao wenyewe.
“Kuiwezesha jamii kumiliki hudum za Afya zinazowahusu katika maeneo wanayoishi na kuboresha huduma za matibabu kupitia utaratibu rahisi na nafuu wa uchangiaji kwenye mifuko ya bima ya jamii’’ alisema Dr. Kilolile.

No comments:

Post a Comment