Baraza la
Wawakilishi Zanzibar (BLW) limekwama kukaa kama kamati ya matumizi na
vikao kwa mara ya tano tangu kuanza kujadili bajeti za mwaka wa fedha
2014/15 Mei 14 mwaka huu kutokana na tatizo la wajumbe kuwa watoro wa
kuhudhuria vikao.
Hali hiyo
imekuwa ikimlazimu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho,
Naibu Spika Ali Abdallah Ali na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mgeni Hassan
Juma kushindwa kuitisha Kamati ya Matumizi kutokana na kutotimia akidi
ya asilimia 50 ya wajumbe 40 kati ya wajumbe 82.
Tukio la
aina hiyo lililotokea mwishoni mwa wiki baada ya Naibu Spika Ali
Abdallah Ali kujikuta akiahirisha Baraza hilo kutokana na uchache wa
wajumbe wakati wakijadili bajeti ya Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na
Nishati iliyowasilishwa na Waziri Ramadhan Abdallah Shaaban.(P.T)
No comments:
Post a Comment