![]() |
Samuel Sitta, Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba |
![]() |
Jaji Warioba jana kabla ya kufanyiwa vurugu na watu wanaodaiwa kupangwa na watu wasiofurahishwa na msimamo wake wa kutetea wananchi baada ya kuchakachuliwa kwa maoni yao kupitia Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyoiongoza. |
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta amesema kilichomkuta
aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba jana ni sawa na
kujitakia mwenyewe.
Akihojiwa na Redio Voice of Tabora, inayomilikiwa na Mbunge wa Jimbo la Tabora, Ismail Aden Rage kuhusu maoni yake kwa
vurugu kubwa iliyoongozwa na Paul Makonda jana, Mzee Sitta amesema
kimsingi wananchi walio wengi wanaunga mkono Katiba pendekezwa.
Mzee
Sitta amesema Jaji Warioba anapaswa kutulia kwani akiendelea anaweza
kuaibishwa kuliko aliyofanyiwa jana pale Ubungo blue pearl.
Mzee Sitta amemtaka Warioba awaachie wananchi Katiba pendekezwa waamue wenyewe kwa njia ya kura.
Sitta ameendelea kusema watanzania wa sasa siyo wajinga na wakikuona unawadanganya watakuvamia hapohapo.
Amedai uelewa wa wananchi kwa sasa ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote.
Alipoulizwa
swali kuhusu Uvumi kwamba yeye ndiye anamfadhili na kumtuma Paul
Makonda kupambana na yeyote anayempinga Mzee Sitta amecheka na kusema
hatajibu hilo swali.
(MALUNDE)
(MALUNDE)
Kuvamiwa
kwa Jaji Warioba kuleta hisia kwamba ni 'chuki' dhidi yake katika
kueneza ukweli juu ya kilichofanywa na wajumbe wa Bunge la Katiba Maalum
katika Katiba Pendekezwa ambayo imeachja baadhi ya maoni ya wananchi na
kuwekwa mawazo ya wajumbe hao ambao wengi wao ni wa chama tawala (CCM).
Kadhalika
watu wamekuwa wakihoji inakuwaje Waziri Mkuu Mstaafu anaweza kufanyiwa
uhuni kama ule uliofanyika Blue Pearl kama HAKUNA NGUVU nyuma ya vijana
WALIOHUSIKA?!
MICHARAZO
ina HAMU kubwa ya kuisikia SERIKALI itatoa TAMKO gani juu ya UHUNI
aliofanyiwa WAZIRI MKUU MSTAAFU, Jaji Joseph Warioba kwani siyo kitu cha
kawaida kwa wananchi waliostaarabika na wenye kudumisha udugu, umoja na
mshikamano hata kama watu WANATOFAUTIANA mawazo. Ngoja tuone.
No comments:
Post a Comment