Monday, 10 November 2014

GARI LA GAZETI LA MWANANCHI LANASWA NA MADAWA YA KULEVYA



Watu wa tatu wanashikiriwa na Jeshi la polisi mkoani wa Iringa kwa tuhuma ya kusafirisha madawa ya kulevya  aina ya mirungi gunia mbili zenye uzito wa kilogram 121.
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi Ramadhani Mungi amesema watuhumiwa hao waliotambulika kwa majina ya Mohamed Ruambo miaka 27 Adam Komba miaka 33 wakazi wa Dares salam na Ayubu Gwalugano miaka 33 makazi wa Mbeya  wamekamatwa leo saa kumi na moja na nusu alfajiri katika barabara kuu ya Iringa Mbeya eneo la Igumbilo wakiwa kwenye gari lenye namba T360 SVR mali ya Mwananchi Communication likitokea Jijini Daers salam kwenda Mbeya .
Aidha Kamanda Mungi amesema kuwa watuhumiwa wanashikiriwa na Jeshi la polisi kwa uchunguzi.

No comments:

Post a Comment