Watoto wawili wenye umri wa miaka 12 na
mwingine 13, wamepandishwa kizimbani wakituhumiwa kufanya jaribio la
kuiba Bankwakitumia Bastola bandia.
Haikuwa movie, hii ni kweli kutoka Israel.
Mmoja wao alikuwa amebeba begi la
daftari mgongoni, huku wakiwa na bastola za toy halafu wakaingia benki
na kuwatisha wateja waliokuwemo ndani ya Benki hiyo mitaa ya Tel Aviv.
Msemaji wa Polisi huko Israel Micky
Rosenfeld amethibitisha tukio hilo kuytokea na kusema kuwa waliwakamata
watoto hao baada ya kupata picha za kwenye camera za CCTV.
Mwanasheria Gil Gabay amekosoa namna
ambavyo watoto hao walihudumiwa wakiwa kituo cha Polisi, waliwekwa kama
watuhumiwa watu wazima huku wakiwafuatilia kwenye camera maalum huku
wakiwa wamekaa kwenye viti ambapo Gabay amesema haki za Watoto hao
zimekiukwa.
Tayari wamefikishwa Mahakamani na kusomewa mashtaka huku wakiwa wameficha sura zao.
Tumia Sekunde 46 kutazama Video ya tukio hilo la aina yake.Unahitaji kupata story zote kali zinazonifikia? Ni rahisi sana mtu wangu.. Niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook
No comments:
Post a Comment