Wasanii
wa muziki wamemtumia salamu za pole Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi dume
(prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo
la Maryland nchini Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania, Rais Kikwete amefanyiwa
upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya yake
kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo.
Upasuaji huo ulikuchukua kiasi cha saa moja unusu ambapo inaelezwa kuwa umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa.
Taarifa hiyo inasema hali ya Rais
Kikwete inaendelea vizuri japo bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya
uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.
Hizi ni baadhi ya salamu za pole kutoka kwa wasanii kwenda kwa Rais Kikwete:
HemedyPHD :UGUA POLE MR.PRESIDENT JAKAYA MRISHO….INSHALLAH MUNGU AKUPE AFYA TENA NA URUDI KATIKA HALI YA KAWAIDA!
Diamondplatnumz :Get well Soon Mr Prezident.
Shettatz :Get well soon Boss….!Inshallah Tunakuombea
Mhtemba :Nakutakia afya njema mh Jk
Lameck Ditto :Rais Wangu Hon: Jakaya M Kikwete nakutakia afya njema na uponaji wa haraka.
Shilolekiuno :Inshaallah!! Mwenyezi Mungu ataleta kher zake Na utakuwa mpya kama zaman!
Mwanafa :Mungu asaidie upone haraka baba..tunaumwa nawe!
Mrishompoto:”NENO NINGEJUA, HUJA MWISHO WA SAFARI” nini tafsiri yako kwenye neno hilo, na picha unayoiona. Jadili bila matusi.
Peter_msechu :POLE SANA MR PRESIDENT JAKAYA MRISHO KIKWETE… tunakuombea upone haraka
Linex Sundaymjeda:Get well soon Mr president…. #Mh Mrisho Jakaya kikwete..
Orijino Komedi: Tunakutakia upate nafuu na kupona haraka Mr. President @jmkikwete
No comments:
Post a Comment