Thursday, 27 November 2014

RIPOTI YA CAG ILIYOWASILISHA BUNGENI NA ZITTO KABWE HII HAPA


Latest NewsKatika kikao cha Bunge kilichokaa leo Novemba 26 Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe na Makamu wake Deo Filikunjombe waliwasilisha Ripoti ya ishu ya Escrow ambapo kama hukupata kusikiliza wakati Ripoti hiyo ikiwasilishwa hii ni sehemu ya uwasilishwaji wa Ripoti hiyo.
…Katika fedha ambazo zimelipwa kwa watu binafsi katika Benki hizi yapo majina ya viongoozi wa kisiasa, viongozi wa madhehebu ya dini, Majaji na watumishi wengine wa Serikali..“– Zitto Kabwe.
Kwa upande wa Viongozi wa Kisiasa walioingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; Mheshimiwa Andrew Chenge Mbunge, ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, shilingi Bil. 1.6, mheshimiwa Anna  Tibaijuka Mbunge na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, shilingi Bil. 1.6, Mheshimiwa William Ngeleja Mbunge na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini, shilingi milioni 40.4, ndugu Daniel Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini shilingi milioni 40.4, ndugu Paul Kimiti, ambaye ni Mbunge mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga shilingi milioni 40.4 na ndugu Enos Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCo aliingiziwa shilingi milioni 161.7…“– Zitto Kabwe.
Kwa upande wa Majaji,  Profesa Eudis Ruangisa aliingiziwa shilingi milioni 404, Mheshimiwa Mujulizi milioni 40.4.
Kwa upande wa Viongozi wa madhehebu ya Kidini walioingiziwa fedha ni Askofu Methodius Kilain shilingi Milioni 80.9, Askofu Nzigirwa milioni 40.4 na Mchungaji Alphonce Simon milioni 40.4..”– Zitto Kabwe.
… Kamati imependekeza kuwa uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali utenguliwe mara moja na kisha afikishwe Mahakamani kwa matumizi mabaya ya Ofisi yaliyopelekea Serikali kupoteza mabilioni ya fedha za umma…“– Deo Filikunjombe.
Kwa upande wa Waziri Mkuu kuhusiana na suala hili baada ya kupitia vielezo vilivyomo kwenye ripoti ya CAG kamati imejiridhisha pasipo mashaka kuwa Waziri Mkuu  alikuwa ana taarifa zote kuhusiana na mchakato mzima wa kuchota  fedha kwenye akaunti ya Escrow, ushahidi ulioletwa mbele ya kamati  za ofisi ya CAG ulionyesha kuwa Waziri Mkuu alikuwa akipata taarifa juu ya jambo hili na kamati imethibitishwa kuona kuwa Waziri Mkuu hakuchukua hatua yoyote kuzuia mhamala huu usifanyike…“– Deo Filikunjombe.
Kamati kwa kuzingatia kielelezo namba 22 inathibitisha kwamba bila shaka Waziri Mkuu alikuwa analijua jambo hili vizuri sana na kwamba aliridhia mhamala huu usifanyike, ndio maana katika maelezo yake  ya Bungeni mara kadhaa Waziri Mkuu alilithibitishia Bunge kuwa fedha za ESCROW hazikuwa fedha za umma…”– Deo Filikunjombe.

Wednesday, 19 November 2014

Barua iliyoandikwa na Meda kwa Diamond Platnumz


Screen Shot 2014-11-19 at 5.34.00 PMNi dakika mbili na sekunde 59 ambazo zimetumika na mwimbaji huyu mpya kwenye bongofleva ambapo barua hii imesimamiwa na producer Silley kutoka Sampamba Music (Iringa) na video ya barua hii imepigwa hukohuko Iringa.
 https://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=6dNT5kzMIvY

DARAJA LA KISASA KUJENGWA BAHARINI ENEO LA AGHA KHAN HADI BARABARA YA KENYATA


Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akionesha sehemu ambazo daraja hilo jipya litakapojengwa pembezoni mwa daraja la Selander kuanzia hospitali ya Aghakan hadi barabara Kenyata. Sehemu ya Daraja hilo pekee litakuwa na urefu wa km 1.03
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile akiwa na ujumbe kutoka Serikali ya Korea Kusini pamoja na Wizara ya Ujenzi mara baada ya kusaini Mkataba wa Muhtasari wa Majadiliano leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile kulia akimshukuru Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli mara baada ya hafla ya utiaji sahihi wa Muhtasari wa Majadiliano.
Tukio la utiaji sahihi likiendelea kama inavyoonekana pichani.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Eng. Patrick Mfugale akionesha mchoro wa nguzo kubwa za daraja hilo litakalopita baharini pembezoni mwa daraja la Selander huku Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe wakifatilia kwa makini.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akifafanua kuhusu ujenzi wa daraja hilo. Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (GCU) Wizara ya Ujenzi.

Thursday, 13 November 2014

PICHA ZA MAZISHI YA GEEZ MABOVU YALIYOFANYIKA LEO

Mazishi ya msanii Geez Mabovu ambaye alikuwa maarufu kwenye muziki wa Hiphop Tanzania, yamefanyika leo nyumbani kwao Iringa katika makaburi ya Mlolo.
Mabovu amefariki dunia kwenye hospitali alikokua amelazwa nyumbani kwao Iringa alikokwenda wiki mbili zilizopita kutokea Dar es salaam akisumbuliwa na maradhi ya kifua.
Ndugu, jamaa marafiki, wasanii na watu mbalimbali wamejitokeza kushiriki katika mazishi hayo.
Hizi ni baadhi ya picha za mazishi ya msanii huyo.
image-13-11-14-06-32-2
IMG_3073
IMG_3076 IMG_3081
Msafara wa Mazishi

image-13-11-14-06-32-3
image-13-11-14-06-32

Kaburi
Marafiki Mazishi
image-13-11-14-06-32-1
Baba wa GeezPicha: Francis Godwin

BREAKING NEWS:ALI KIBA NA DIAMOND WAMALIZA TOFAUTI ZAO




















 Taasisi ya utoaji mikopo VICOBA TANZANIA imemaliza ugomvi kati ya msanii Ali Kiba na Diamond na kuwaunganisha kua kitu kimoja na kutegemewa kufanya kazi kwa pamoja.

Uongozi wa vicoba umesema kua sababu ya kumaliza ugomvi wa Ali Kiba na Diamond ni kutaka kuwaweka pamoja ili waweze kufanya TANGAZO la pamoja kuhusu Taasisi hii ya utoaji mikopo kupitia mfuko wa Utoaji mikopo wa Online uitwao FOCUS VICOBA unaopatikana katika mtandao kupitia tovuti yao www.vicobatanzania.wapka.mobi kuanzia mwezi wa 12 Tangazo hilo litakua tayari na kuanza kurushwa katika vituo mbali mbali vya TV.


BY Habaritalk blog

Tuesday, 11 November 2014

CHUO FEKI CHA KILIMO MBEYA CHAFUNGIWA


Jamaa walivyo matapeli wametumia jina la Mh. Sumae Waziri mkuu mstaafu kuwa ndiyo alizinduo chuo hicho kumbe ni uongo mtupu
 Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya Bi Quip Mbeyela aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Daktari Norman Sigala akitoa tamko la kufunga chuo hicho

Kulia ni Richard Mchomvu mkuu wa Polisi wilaya ya Mbeya akiwa na jalada la uchunguzi kuhusiana na chuo hicho

Baadhi ya wanafunzi wakiwa hawaamini tamko lililotolewa na Selikari juu ya kufungwa chuo chao



Hakika ilikuwa huzuni kubwa kwa wanachuo hao


Wakazi wa ilemi wakiomboleza na wanachuo hao




Serikal imekifunga chuo cha Kilimo na Mifugo cha Nice Dream kilichopo mtaa wa Mapelele Kata ya Ilemi Jijini na kuwataka wanachuo wa chuo hicho kuondoka chuoni hapo baada ya siku tatu.
Agizo hilo lilitolewa na Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya Bi Quip Mbeyela aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Daktari Norman Sigala na kwamba Serikali itagharamia chakula kwa siku tatu ambapo Serikali ilikabidhi shilingi laki tatu kwa Mtendaji Kata Bi Gladness Sapuka kwa ajili ya kununua chakula kwa wanachuo 48 waliokuwa wakisoma katika chuo hicho ambacho hakina usajili kutoka Baraza la Vyuo(NACTE).
Tamko hilo lilamsha kilio chuoni hapo kutoka kwa wanachuo na wakazi wa Ilemi kutokana na wanachuo hao kutakiwa kuwasiliana na wazazi wao na walezi ili watumiwe nauli za kuwasafirisha makwao na wengi wao wakitokea mkoa wa Kagera na Mara na kwamba wanachuo hao wamekwisha lipa kila mmoja zaidi ya shilingi laki tano na elfu hasini.
Mbali ya chuo hicho kutosajiliwa na NACTE pia mmiliki wake hafahamiki vema na jalada la uchunguzi ili akamatwe kujibu tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kutumia kivuli cha chuo na kuwatapeli wanachuo 48 waliokuwa na nia ya kusomea taaluma ya kilimo.
Kauli hiyo ilikuwa mwiba kwa wanachuo hao pale Kaimu Katibu Tawala aliposema kwamba Serikali haina chuo cha kuwapeleka kwa kuwa hakuna nafasi katka Vyuo vya Kilimo Mkoani Mbeya na muda wa usajili wa wanavyuo vya kilimo umemalizika.
Kaimu Katibu Tawala aliambatana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mbeya Richard Mchumvu ambaye alisema kuwa Jeshi la Polisi linamtafuta mtuhumiwa na kwamba pindi atakapopatikana atafikishwa mahamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili.
Kwa upande wa wakazi wa Ilemi wameiomba Serikal kuangalia upya suala hilo kwa kuwa mtuhumiwa hajakamatwa hivyo serikali iwasaidie usafiri wa kuwaridisha wanachuo hao makwao ili kuwapunguzia makali kutokana na umbali wanaotoka.
Wazo hilo liliungwa mkono na Diwani wa Kata ya Ilemi Furaha Mwandalima ambaye alisema serikali ione hilo kama janga la moto au mafuriko il kuwasaidia kuwasafirisha makwao kwani wengi wa wanachuo hawana uwezo wa kupata nauli ya kuwafikisha makwao ambapo mwanachuo mmoja anahitaji kutumia zaidi ta shilingi laki moja na zaidi ya shilingi milioni sita zinahitajika kuwafikisha makwao.
Pamoja na kauli ya Serikali kutoa tamko wakazi wa Ilemi walibaki ili kujadiliana mustakabali wa wa wanachuo hao kutokana na wengi kutoka katika familia duni na wengi kuonekana kukata tamaa ya kuishi kwa kile walichodai kuwa mmoja wao alikuwa ni pacha na mwenzake ambapo nduguye aliozwa ndipo zikapatikana fedha za karo.

MGOGORO WA KANISA LA MORAVIA JIMBO LA KUSINI MAGHARIBI WAIBUKA UPYA OFISI ZA MAKAO MAKUU JIMBO ZAFUNGWA KWA MINYORORO






Aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo Mchungaji Nosigwe Buya akiongea na waandishi wa habari nyumbani kwake jimboni hapo akisema sielewi naona tu wakitoa vyombo vyangu nje na kuvuja mabada yangu ya mifugo


Aliyeyeongoza zoezi hilo  Frank Phili Mtunza hazina wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Bethelehem ulioko Mama John Jijini amesema sis tunachotaka Sinodi iitishwe tumechoka na malumbano ya kila kukicha

Mchungaji wa kanisa la moraviani ushirika wa jakaranda akiongea na waandishi wa habari


Baadhi ya Wachungaji na Waumini wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Oktoba 10 majira ya saa 11 jioni walifunga ofisi zote za Makao makuu ya Kanisa hilo zilizopo Jacaranda Jijini Mbeya na kumzuia aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo Mchungaji Nosigwe Buya kuhama kwenye eneo hilo kwenda nyumba nyingine eneo la Saba saba.
Aliyeyeongoza zoezi hilo ni pamoja na Frank Phili Mtunza hazina wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Bethelehem ulioko Mama John Jijini Mbeya akiwa na Mchungaji Mwilgumo pamoja na Mchungaji Mwakyoma.
Ofisi zilzofungwa kwa kutumia minyoro na mbao ni pamoja na ofisi ya Askofu Alinikisa Cheyo,Ofisi ya Katbu Mkuu,Ofisi ya Mtunza Hazina Mkuu na lango kuu la kuingilia makao makuu ya Kanisa hilo.
Hatua hii ya kufunga ofisi za Kanisa ni la pili kwa mwaka huu awali ilikuwa mwezi Julai mwaka huu ambapo waumini hao walifunga hivyo hivyo kabla ya Serikali kuingilia kati na kufanya suluhishi kupitia Kamati ya ulinzi na Usalama ya Wilaya na kuweka makubaliano.
Hata hivyo Phili alidai maagizo yaliyotolewa na Kamati ya Ulinzi na Usalama hayakutekelezwa ikiwa ni pamoja na kumrudisha kazini Mchungaji Nosigwe Buya na kuacha kumhamisha kituo cha kazi.
Aidha waumini hao walichukua hatua ya kuzuia kuhamishwa kwa Mchungaji Buya ambapo alikuwa amefunga mizigo yake huku mkewe akishindwa kupika na kuwahudumia watoto kwa siku nzima na banda la mifugo limeezuliwa na mtu aliyetumwa kutoka ofisi kuu.
Pamoja na juhudi za Kanisa kujaribu kumhamisha Mchungaji Nosigwe Buya ziligonga ukuta baada ya ya waumini hao wasiozidi ishirini kumuondoa kijana aliyekuwa akiondoa mabati na mabanzi ya banda la mifugo kuondoka mara moja na kumtaka mke wa Mchungaji Buya Edda Kabuka kuendelea na shughuli zake.
Kwa upande wake Mchungaji Buya alisema kuwa hapingi kuondoka katika nyumba hiyo na kukataa kwenda kituo kingine cha kazi lakini ameshangazwa na kwenda kinyume na makubaliano ya kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya lakini kukiukwa maazimio ya yaliyofanyika mwezi Julai mwaka huu.
Pia alidai mgogoro huu umeligawanya Kanisa na kwamba hivi sasa mahubiri yanayofanyika kanisani yamekuwa ya kutpiana maneno kwa pande mbili zinazopingana na kufanya waumini kushindwa kupata ufumbuzi wa kudumu na kudai kuwa suluhu pekee iwe ni kuitisha mkutano mkuu wa Kanisa(Sinodi).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi alisema amesikitishwa na pande hizo zinazopingana na kwamba ni kwa nini mgogoro huo haupati ufumbuzi licha ya Kamati ya ulinzi na usalama kusuluhisha na kwamba Jeshi la Polisi litamkamata yeyote atakayevunja amani kwani kazi ya Jeshi la Polisi ni kulinda usalama wa Raia na mali zake.

WANANCHI MKOANI IRINGA WAMETAARUKI BAADA YA MOSHI MZITO KUTANDA ANGANI

Eneo moto ulikotokea

Wananchi wakishuhudiatukio hilo la moto

Asikari zima moto wakijitahidi kuzima moto huo.


eneo lililo nusurika kuungua



       







Wananchi wa manispaa ya Iringa kata ya Makorongoni wamekumbwa na taharuki baada ya  moshi mzito kutanda angani baada ya watu wasiojulikana kuchoma matairi yaliyokuwa yamerundikwa kwenye jalala hilo lisilo rasmi.
Akizungumza na Habaritalk blog diwani wa kata ya hiyo Bw.Tadeus Tesha amesema eneo hilo hutumiwa na wachongaji wa viatu vijulikanavyo kama Kobasi                 kutupa mabaki ya matairi ambapo inasemekana kuna watoto wa mtaani hulala kwenye jalala hilo.

Aidha kwa upande wake fundi wa gereji iliyopo jirani na tukio hilo Bw.Lazaki Wihaa amekana kuhusika kuwa chanzo cha moto huo na kusema kuwa wachongaji matairihuenda wakawa chanzo.

Mpaka Habaritalk blog inaondoka katika eneo la tukio chanzo cha moto huo hakikuweza kujulikana kwani uchunguzi wa kina unaendelea.

By Habaritalk blog

Monday, 10 November 2014

WASANII WAMTUMIA SALAMU ZA POLE RAIS KIKWETE BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI

rais

Wasanii wa muziki wamemtumia salamu za pole Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland nchini Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania, Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo.

Upasuaji huo ulikuchukua kiasi cha saa moja unusu ambapo inaelezwa kuwa umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa.

Taarifa hiyo inasema hali ya Rais Kikwete inaendelea vizuri japo bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.
Hizi ni baadhi ya salamu za pole kutoka kwa wasanii kwenda kwa Rais Kikwete:
HemedyPHD :UGUA POLE MR.PRESIDENT JAKAYA MRISHO….INSHALLAH MUNGU AKUPE AFYA TENA NA URUDI KATIKA HALI YA KAWAIDA!
Diamondplatnumz :Get well Soon Mr Prezident.
Shettatz :Get well soon Boss….!Inshallah Tunakuombea
Mhtemba :Nakutakia afya njema mh Jk
Lameck Ditto :Rais Wangu Hon: Jakaya M Kikwete nakutakia afya njema na uponaji wa haraka.
Shilolekiuno :Inshaallah!! Mwenyezi Mungu ataleta kher zake Na utakuwa mpya kama zaman!
Mwanafa :Mungu asaidie upone haraka baba..tunaumwa nawe!
Mrishompoto:”NENO NINGEJUA, HUJA MWISHO WA SAFARI” nini tafsiri yako kwenye neno hilo, na picha unayoiona. Jadili bila matusi.
Peter_msechu :POLE SANA MR PRESIDENT JAKAYA MRISHO KIKWETE… tunakuombea upone haraka
Linex Sundaymjeda:Get well soon Mr president…. #Mh Mrisho Jakaya kikwete..
Orijino Komedi: Tunakutakia upate nafuu na kupona haraka Mr. President @jmkikwete

WASANII WAMTUMIA SALAMU ZA POLE RAIS KIKWETE BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI

rais

Wasanii wa muziki wamemtumia salamu za pole Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland nchini Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania, Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo.

Upasuaji huo ulikuchukua kiasi cha saa moja unusu ambapo inaelezwa kuwa umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa.

Taarifa hiyo inasema hali ya Rais Kikwete inaendelea vizuri japo bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.
Hizi ni baadhi ya salamu za pole kutoka kwa wasanii kwenda kwa Rais Kikwete:
HemedyPHD :UGUA POLE MR.PRESIDENT JAKAYA MRISHO….INSHALLAH MUNGU AKUPE AFYA TENA NA URUDI KATIKA HALI YA KAWAIDA!
Diamondplatnumz :Get well Soon Mr Prezident.
Shettatz :Get well soon Boss….!Inshallah Tunakuombea
Mhtemba :Nakutakia afya njema mh Jk
Lameck Ditto :Rais Wangu Hon: Jakaya M Kikwete nakutakia afya njema na uponaji wa haraka.
Shilolekiuno :Inshaallah!! Mwenyezi Mungu ataleta kher zake Na utakuwa mpya kama zaman!
Mwanafa :Mungu asaidie upone haraka baba..tunaumwa nawe!
Mrishompoto:”NENO NINGEJUA, HUJA MWISHO WA SAFARI” nini tafsiri yako kwenye neno hilo, na picha unayoiona. Jadili bila matusi.
Peter_msechu :POLE SANA MR PRESIDENT JAKAYA MRISHO KIKWETE… tunakuombea upone haraka
Linex Sundaymjeda:Get well soon Mr president…. #Mh Mrisho Jakaya kikwete..
Orijino Komedi: Tunakutakia upate nafuu na kupona haraka Mr. President @jmkikwete