Familia
moja kutoka Australia imekanusha kumtelekeza mtoto waliomlipa mama mmoja
nchini Thailand kuwabebea kufuatia ripoti za daktari kuwa alikuwa na
upungufu wa kiakili.
Pattharamon
Chanbua, 21, aliingia mkataba wa kuwasaidia Waaustralia hao kupata
mtoto baada ya mwanamke huyo kushindwa kubeba mimba mwenyewe.
Hata
hivyo alipojaaliwa akazaa mapacha wazazi hao walikuja wakamchukua mmoja
ambaye akili zake zilikuwa timamu na wakamuacha nyuma mtoto Gammy baada
ya ripoti ya daktari kuonesha kuwa alikuwa na akili taahira.
Chanmbua
anasema kuwa punde baada ya madaktari kugundua kulikuwepo na hitilafu
wazazi hao wa Gammy walimshauri aavye mimba hiyo lakini akkataa kwani
haiambatani na dini yake ya Kibudhaa.
Wazazi
hao wa Gammy wamejitetea wakisema kuwa walimchukua mtoto mmoja baada ya
madaktari kutarajia kuwa Gammy angekuwa na matatizo ya ugonjwa wa moyo
na maambukizi ya mapafu.
Baba ya
mapacha hao wawili aliwatembelea wote wakiwa hospitalini punde baada ya
kuzaliwa lakini haijulikani kwanini alimtelekeza Gammy.
Mama huyo ambaye tayari yuko na wanawe wawili sasa anasema hatamtupa Gammy bali atamlea kama mwanawe.
Matukio hayo yamepelekea watu kote nchini Australia wanakotoka wazazi wake kufoka wakiwalaumu kwa kumnyima haki zake Gammy .
Aidha
wengi wanakashifu matukio hayo wakidai kuwa huo ni ukoloni mamboleo kwa
watu wenye hela lakini wanamatatizo ya kuwapata watoto wao wenyewe
wanasafiri kuelekea nchi za mbali na kukodisha wanawake maskini kwa niya
ya kujitoa mzigo wa ukosefu wa watoto.
Mtoto aliyezaliwa na akili taahira kwa mama wa kupanga .
Lakini wakipata watoto hao wanakasoro fulani wanatoroka na kuwaachia wale wazazi maskini na mzigo wa kuwalelea watoto wao.
Waziri
mkuu wa Australia Tony Abbott na waziri wa maswala ya uhamiaji nchini
humo Scott Morrison wamehuzunishwa na tukio hilo wakisema ni la kushtua
sana.
Wazazi wa
Gammy wamenukuliwa katika mjadala na runing moja ya Channel 9 wakisema
kuwa wanamtoto mwenye umri wa miezi 6 lakini hawana mtoto mwengine na
kukanusha habari kuwa walimtelekeza ndugu ya mtoto wao wa kike.
Wazazi hao wanaoishi mjini Perth, vilevile wameiambia runinga ya taifa kuwa hawajui analosema bi Chanbhua .
Chanbua
aliiambia jarida la Fairfax Media kuwa babake Gammy anaumri wa miaka
Hamsini hivi na kuwa aliwahi kuja hospitalini na alionekana kumjali sana
msichana wake na kumpuuza kabisa Gammy licha ya kuwa alikuwa hapo
kitandani.
''Alikataa hata kumtizama usoni mwanaye''
Mtoto aliyezaliwa na akili taahira kwa mama wa kupanga .
''sasa nitafanya nini ilinipate kumlea ?
Labda itanibidi niwashtaki mahakamani ilinipate hela za kuwatunzia mtoto wao ''.
Waziri wa
uhamiaji hata hivyo amesema kuwa serikali ya Australia ikishirikiana na
ile ya Thailand zinashirikiana kutafuta suluhu ya mkasa huo .
Bwana
Morris alisema kuwa mtoto Gammy ni raiya wa Australia na kuwa anastahili
kupata msaada wa kimatibabu kutoka kwa serikali ya Australia.
Ni haramu
kumlipa mtu iliakubebee mimba nchini Australia kwa hivyo wazazi ambao
hawana uwezo wa kupata mtoto hukimbilia mataifa ya nje na kufanikisha
azimio la kuwa wazazi.
Tayari wasamaria wema wamechangisha dola laki mbili kumsaidia mama huyo kumlea mtoto Gammy.
Tuma Maoni
Tafuta Habari
Nafasi za Kazi & Masomo
Prev
Next
Video Gallery
Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.
No comments:
Post a Comment