Kikosi cha Dmct Fc wakiomba Dua |
Kocha wa Kimataifa Lucas Kulwa akitoa maelezo kwa wachezaji wa timu zote mbili DMCT Fc na Loyal of Africa |
Timu ya DMCT Fc ya yaichapa timu Loyal of Africa, bao moja
kwa sifuri katika mchezo uliochezwa saa kumi na nusu na kumalizika saa kumi na mbili kamili jioni ya
leo katika viwanja vya nanenane John Mwakangale jiji mbeya.
Timu DMCT FC ilijipatia goli hilo katika dakika ya 35, kwa
kupitia mshambuliaji wake hatari
Emmanuel Mwinuka kupitia krosi kali
iliyopigwa na msambuliaji Emmanuel Balotel huku goli kipa wa Loyal of
Africa akiwaamebaki hana la kufanya hadi dakika ya tisini, refa wa kimataifa
Lucas Kulwa kupuliza kipenga dmct fc moja Loyal of Africa sifuri.
Mashabiki wa Loyal
of Africa wakiongea na mtandao wetu walisema kuwa refa amechezesha mchezo
vizuri bila kupendelea na kukiri mapungufu ya kipa wao na wachezaji wao.
Pia mashabi wa DMCT
hawakubaki nyuma na kusema wanafurahia ushindi wao wa goli moja dhidi ya watani
wao Loyal Fc.
Na Habaritalk
No comments:
Post a Comment