Friday, 29 August 2014

WATU ZAIDI YA KUMI WAFARIKI KATIKA AJALI MBALIZI MBEYA

li>

Hivi ndivyo ambavyo Daladala hiyo ilivyojibamiza muda mchache uliopita 

Eneo hili la ubavuni ndipo eneo ambalo Daladala hiyo iliingia na Kujigonga 
Gari hilo aina ya Tata likiwa limepaki pembeni Muda mchache baada ya kupata ajali hiyo
Askari wa usalama wa Barabarani akiwa anatazama na kuchunguza zaidi ajali hiyo
Eneo ambalo Daladala hiyo iliyofumuka 
Viti vikiwa vimeharibika baada ya ajali kutokea 

Hivi ndivyo Daladala hiyo iliyokuwa ikitoka Mwanjelwa kuja Mbalizi ilivyo  Haribika Baada ya ajali hiyo

Mashuhuda wakiwa wamelizunguka daladala hiyo kushuhudia kllichotokea 
 Hapa ndipo eneo ambapo ajali imetokea , Askari wa usalama wa barabarani wakiendelea kufuatilia ajali hiyo
 Ilikuwa ni Ajali mbaya 

Mashuhuda 
Baadhi ya Majeruhi wakiwa wanatolewa katika Hospitali ya Ifisi kuelekea Hospitali ya Rufaa Mbeya 

WATU kumi wakiwemo watoto wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari mawili.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa nne asubuhi ikihusisha gari ndogo ya abiria maarufu daladala lenye namba za usajili T 237 BFB aina Toyota Hiace  na gari kubwa aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158 CSV.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo ilitokea maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea Mbeya mjini kuelekea Mbalizi kulivaa Fuso ilikuwa ikiingia barabarani.
Walisema inasemekana dereva wa Hiace gari yake ilimshinda kutokana na kutelemka mlima mkali wa Mbalizi inagawa pia walimtupia lawama dereva wa Fuso ambaye alikuwa akiingia barabarani bila kuchukua tahadhari.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali teule ya Ifisi Mbalizi, Sikitu Mbilinyi, ambako Majeruhi na marehemu walikimbizwa hapo alithibitisha kupokea majeruhi 7 ambapo alisema kati yao ni wanawake 3 na wanaume 4.
Alisema kati ya majeruhi hao wawili wamepewa rufaa kwenda hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na kuhitaji msaada zaidi huklu wengine wakiendelea kupatiwa msaada wa haraka ili kunusuru hali zao.
Mbilinyi aliongeza kuwa pia wamepokea miili ya marehemu 10 wakiwemo watoto wawili na Wanawake wanne na Wanaume wanne.
Hata hivyo majina ya majeruhi na marehemu hayajaweza kupatikana mara moja kutokana na kuwa katika hali mbaya ambapo Dereva wa Fuso akitokomea mara baada ya tukio.
NA MBEYA YETU BLOG

DMCT FC YA MCHAPA LOYAL OF AFRICA KICHAPO CHA BAO MOJA (1) KWA BILA

Kikosi cha Dmct Fc wakiomba Dua

Kocha wa Kimataifa Lucas Kulwa akitoa maelezo kwa wachezaji wa timu zote mbili DMCT Fc na Loyal of Africa

Timu ya DMCT Fc ya yaichapa timu Loyal of Africa, bao moja kwa sifuri katika mchezo uliochezwa saa kumi na nusu  na kumalizika saa kumi na mbili kamili jioni ya leo katika viwanja vya nanenane John Mwakangale jiji mbeya.
   Timu DMCT FC  ilijipatia goli hilo katika dakika ya 35, kwa kupitia mshambuliaji  wake hatari Emmanuel  Mwinuka kupitia krosi kali iliyopigwa  na msambuliaji  Emmanuel Balotel huku goli kipa wa Loyal of Africa akiwaamebaki hana la kufanya hadi dakika ya tisini, refa wa kimataifa Lucas Kulwa kupuliza kipenga dmct fc moja Loyal of Africa sifuri.
   Mashabiki wa Loyal of Africa wakiongea na mtandao wetu walisema kuwa refa amechezesha mchezo vizuri bila kupendelea na kukiri mapungufu ya kipa wao na wachezaji wao.
   Pia mashabi wa DMCT hawakubaki nyuma na kusema wanafurahia ushindi wao wa goli moja dhidi ya watani wao Loyal Fc.   
Na Habaritalk

Wednesday, 27 August 2014

ETO'O ATUA EVERTON

ETOO_a2f4b.jpg
Everton wamemsajili Samuel Eto'o kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kuondoka Chelsea msimu uliopita.
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Cameroon, 33, amejiunga kama mchezaji huru na anaungana na Romelu Lukaku waliokuwa pamoja Chelsea.
Boss wa Everton Roberto Martinez amesema: "Nilikutana naye na tukawa na mazungumzo mazuri. Nilivutiwa sana na njaa ya kucheza soka ambayo bado anayo.
"Tumefurahishwa sana na nadhani Everton ni makazi yake mazuri."..(E.L)

Kikwete uso kwa uso na Ukawa

Dodoma/Dar. Wakati wowote wiki hii, Rais Jakaya Kikwete anatarajia kukutana na viongozi wa Vyama vya Siasa vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) ili kuzungumzia mchakato wa Katiba.
Katika mkutano huo, Rais Kikwete atakutaka 'kiaina' na wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao unaundwa na vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema na CUF..(E.L)..
Aprili 16, mwaka huu wajumbe wa Ukawa na baadhi kutoka Kundi la 201, walisusia vikao vya Bunge hilo wakitaka msingi wa mapendekezo ya Rasimu ya Katiba usibadilishwe, wakipinga uamuzi wa CCM kutaka kuingiza mfumo wa serikali mbili badala ya tatu zilizopendekezwa katika Rasimu.
TCD inaundwa na vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni ambavyo ni CCM, CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi, UDP na TLP, huku vyama visivyo na uwakilishi bungeni vikiwakilishwa na UPDP kinachoongozwa na Fahmi Dovutwa.
Jana, kwa nyakati tofauti wenyeviti wenza wa Ukawa, Freeman Mbowe (Chadema) na Profesa Ibrahim Lipumba (CUF) na James Mbatia (NCCR Mageuzi), walisema wako tayari kukutana na Rais, ila msimamo wao wa kutaka ijadiliwe rasimu iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Kimekuwa ni kilio cha muda mrefu kwa Ukawa kuomba wakutane na Rais Kikwete kwa ajili ya kujadiliana namna bora ya kuendesha mchakato wa kupata Katiba Mpya.
Akizungumza na waandishi wa habari bungeni Dodoma jana, Mwenyekiti wa TCD, John Cheyo alisema Rais atafanya kikao hicho wakati wowote ndani ya wiki hii na kwamba viongozi wa vyama wakiwamo wa Ukawa, wamethibitisha kushiriki.
Cheyo alisema, katika kikao walichokutana Dar es Salaam Agosti 23, wanachama wa TCD walikubaliana kwamba upo umuhimu wa kukutana na Rais Kikwete kwa mazungumzo na maridhiano.
Kukutana kwa viongozi hao, kunakuja huku wajumbe wa Bunge Maalumu wakiwa wamemaliza kujadili sura zote 15 zilizokuwa zimesalia na tayari baadhi ya kamati zimemaliza kupiga kura wakisubiri kuingia bungeni Septemba 2 kwa kazi ya kupigia kura sura kwa sura.
Kuhusu viongozi wa Ukawa, alisema wanazo taarifa na baadhi yao walikuwapo katika kikao cha kujadili kukutana na kiongozi huyo wa nchi, hivyo akasema lazima watashiriki wakati wowote wakiitwa.
Lipumba
Akizungumzia mkutano huo na Rais, Profesa Lipumba alisema: "Tunakutana na Rais Kikwete kwa sababu sisi ni wanachama wa TCD." Alipoulizwa juu ya msimamo wa Ukawa, alisema lengo ni kutafuta mwafaka ili mchakato wa kupata Katiba Mpya uendeshwe kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.
"Kikubwa tunachokitaka ni maoni ya wananchi yaliyokusanywa na Tume ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Warioba kuheshimiwa na siyo kuchukuliwa maoni mengine kama inavyofanyika sasa huko bungeni," alisema Profesa Lipumba.
Mbowe
Mbowe alisema Katiba Mpya ni kwa masilahi ya Watanzania wote na Taifa lao, hivyo inapotokea mikutano kama hiyo na kwa hali ilivyo sasa, hakuna mtu mwenye nia njema atakayekataa kushiriki. Kikubwa ni kwamba hatuwezi kubadili msimamo wetu na huo ndiyo ukweli," alisema.
Kuhusu Bunge hilo kupokea maoni ya makundi mbalimbali wakati tayari ukusanyaji wa maoni umeshafanywa na Tume ya Jaji Warioba, Mbowe alisema, "Ndiyo maana tulisusia vikao vya Bunge la Katiba, nadhani sasa Watanzania wamejua kwa nini tulitoka nje."
Mbowe alisema kuwa mchakato wa Katiba unaendeshwa kwa mujibu wa sheria, lakini hivi sasa Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samwel Sitta analiendesha Bunge hilo kinyume na sheria hiyo... "Ukusanyaji wa maoni unaofanyika sasa ni fedheha kwa CCM na Serikali, ni utoto na aibu wa CCM. Kwa sasa Ukawa tumetulia tunatazama hali inavyokwenda na tuna mipango yetu ambayo tunapanga. Kama hali ikiendelea kuwa hivi tutachukua uamuzi mgumu ili dunia nzima ijue."
James Mbatia
Alisema wako tayari kukutana na Rais Kikwete kwa ushauriano kwa sababu suala la maridhiano ni la msingi na viongozi wote wa TCD walikubaliana Agosti 23.
"Mwaliko tumeupata na tutashiriki. Bunge linaweza kuendelea kwa taratibu zake za kisheria, lakini suala la mashauriano, lazima tukae tuangalie ni jinsi gani Taifa letu linaweza likavuka kwa maridhiano kwa amani na utulivu," alisema.
Kauli ya Ikulu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Salva Rweyemamu alisema Rais Kikwete yuko tayari kukutana na viongozi wa vyama vya siasa muda wowote... "Wao wafuate utaratibu tu, Rais hawezi kukataa kukutana nao na hilo amekuwa akilisema mara nyingi tu."
UKAWA_f2ba2.jpg

Tuesday, 26 August 2014

ANGALIA KIFO CHA KUJINYONGA KILIVYO KIBAYA

Mwili wa Rashid Athuman ukiwa unaning’inia katika kitanzi ambacho alikifunga chooni kabla ya kujinyonga kasha kujifungia chooni.

Mwili wa Rashid Athuman ukishushwa na wasamaria wema kutoka kwenye kitanzi kwa kwa kushirikiana na Jeshi la polisi.

Mwili wa Rashid Athuman ukiwa unahifadhiwa katika chumba cha kuhifadhiwa maiti katika hospital ya Peramiho.
Hiki ni chumba  ambacho marehemu alikuwa amepanga na kinachoonekana ni kitanda ambacho alikuwa anatumia kulala yeye na mke wake .
Mke wa marehemu Lucy Adam (24) akiwa amembeba mtoto wake Yoweri Rashid (02) mgongoni.
--------------------------------
Na Oswad Ngonyani wa demashonews. Peramiho - Songea
Ikiwa imepita siku moja tangu mazishi ya Fundi maabara mstaafu wa Hospitali ya Peramiho Bwana Frederick Mgaya (60) ambaye alifariki kwa  kujinyonga alhamisi iliyopita hapa Peramiho, mtu mwingine tena aliyetambulika kwa jina la Rashid Athuman (32) amekutwa amejinyonga katika  choo cha nyumba aliyokuwa akiishi.

Bwana Rashid Athuman ambaye ni mkazi wa Usangu Jijini Mbeya amejinyonga kwa kutumia shuka majira ya saa Saba za usiku baada ya kumuaga mke wake Bi Lucy Adam (24) kuwa anakwenda chooni kujisaidia ambapo alikwenda kukamilisha mpango wake huo.
Taarifa kutoka kwa mke wake huyo zinaeleza kuwa enzi za uhai wake Bwana Rashid Athuman alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua kikuu, tatizo lililowafanya wachukue uamuzi wa kuja Peramiho kwa ajili ya matibabu.
Bi Lucy anazidi kutanabaisha kuwa walifika Peramiho tarehe 19 Mwezi Julai  2014 na kupata chumba cha kupanga katika Kitongoji cha Namihoro jirani na Stendi Kuu ya Peramiho katika nyumba ya Cosmas Chidumule ambapo tangu wakati huo waliendelea na maisha yao wakiwa wakisaidiwa chakula na majirani waliokuwa na mapenzi mema.
“Tangu jana asubuhi nilishinda vizuri tu na marehemu mume wangu ambapo mishale ya saa tatu za usiku tulienda kulala. Muda mchache baadaye nilipitiwa na usingizi mpaka majira ya saa saba za usiku ambapo marehemu aliniamsha na kunieleza kuwa alikuwa anakwenda uani kujisaidia ambapo baada ya yeye kuelekea uani mimi niliendelea kulala” Alisema mke huyo wa marehemu.

“Baada ya muda mrefu kupita pasipo marehemu kurudi nikaamua kuamka na kutaka kuufungua mlango wa chumbani lengo hasa likiwa kwenda uani kujua sababu ya mume wangu kuchelewa kurudi. Nilishangaa kuona mlango umefungwa kwa nje na ikanibidi nitumie kisu ili kuweza kuufungua mlango huo ambapo nilifanikiwa na kwenda uani ambapo nilikuta mlango wa uani ukiwa umefungwa kwa ndani kitu kilichonifanya niusukume kwa nguvu na kumkuta mume wangu akiwa ananing’inia huku akiwa amekwishafariki” Alimalizia mjane huyo.

Mjane huyo ameishi na marehemu kwa muda wa miaka mitatu na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume, Yoweri Rashidi (2) ambapo uchunguzi zaidi kuhusu chanzo cha kifo hicho bado unaendelea.

SOURCE;demashonews

TUKIO LA KUSHANGAZA NYANYA YENYE SURA YA BINADAMU ENEO LA DUMILA

Saturday, 23 August 2014

KIJANA MOJA ANUSURIKA KIFO AKIJARIBU KUIBA PIKIPIKI KAHAMA

 Haya twendeni vizuri sasa angali huko kwako ana nguvu huyu mtu hunaona  halivyokaaa
 Baada ya kufikishwa hospital ya wilaya ya kahama kwa matibabu ana baada ya wasamaria wema wakimsaidia nesi kumpeleka kwa dakitali kwa huduma .
 Nes nisaindieni jaamani nipo pekee yangu ndiyo maneno ya nes naosema na  kumuweka katika kiti cha wangonjwa .
 Njamaaa muinueni huko tumuweke kwenye kiti kwa ajili ya huduma hospitali ya wilaya ya kahama
 jaamani hajakaa vizuri mshikilieni vizuri kwanza 
Kijana mmoja anayekadiriwa kwa na umri wa miaka 30-32 ambaye hajafahamika majina wala makazi yake ameuawa kwa  kupigwa mawe, kisha kuchomwa moto na wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira, baada ya kumtuhumu kutapeli pikipiki.

Tukio hilo limetokea jana  majira ya saa tano asubuhi katika mtaa wa Nyihogo, eneo la Mnazi Mmoja, Barabara ya Tabora Karibu na Ofisi za halmashauri ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga.

 Mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa ni marehemu inadaiwa alikodisha Pikipiki hiyo  zaidi ya Miezi mitatu iliyopita katika eneo la Maegesho ya Daladala za Pikipiki katika Lango kuu la hospital ya Wilaya hiyo.

Aidha Mmiliki wa Pikipiki hiyo ambaye hajafahamika mara moja wala namba ya  pikipiki, inadaiwa alimkamata  maeneo ya mtaa wa Shunu Kata ya Nyahanga ambapo aliamua kumpeleka katika kituo cha polisi  akiwa amemfunga kamba.

 Baada ya wananchi kuona mtuhumiwa amefungwa kamba ndipo wakamuuliza mmiliki huyo ambaye aliwaeleza, na ghafla wananchi wakaanza kumshambulia kwa mawe na kisha kumchoma Moto.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa shinyanga Justus kamugisha Amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa ni kweli tukio hilo limetoka jana majira ya asubuhi saa 5 kijana moja ambaye jina lake alikuweza kufahamika mara moja alikuwa amekamatwa na mwanachi moja ambapo alikuwa ametoloka na pikipiki yake maeneo ya nyahanga wilayani kahama .

Aidha kamanda kamugisha alizidi kuelezea kuwa pamoja na tukio hilo kutokea kwa kijana huyo  jeshi la polisi linawatafuta watu wote walifanya mauji hayo

MATUKIO KATIKA PICHA:

 Hapa ni baadhi ya mwananchi wakijalibu kumtambua kijana huyo.
 Twendeni sasa
 Jamaani nakufa hayo ni maneno ya huyo kijana hakisema kwa tabu sana

 Haya kaa vizuri kaka umekwisha fika hapa hospitali
 Haya twende sasa
CHANZO KIJUKUU BLOG