Monday, 28 July 2014

UYOLE YAIBUKA KIDEDEA KOMBE LA BODABODA


 Kwanza Mbeya, Mgeni rasmi Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harisson Mwakyembe akimkabidhi kombe nahodha watimu ya Boda boda uyole 


Waziri Mwakyembe alitimiza ahadi yake kwa chama cha Waendesha bodaboda Mkoa wa Mbeya kwa kuwakabidhi pikipiki mbili mpya pamoja na jezi mbili za mpira wa miguu kwa ajili ya timu ya jiji itayoundwa baada ya kumaliza ligi hiyo.

Timu ya Uyole

Timu ya Kabwe


Mgeni rasmi Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harisson Mwakyembe akiongea na waendesha bodaboda wa mkoa wa Mbeya mara baada ya kufunga mashindano yao




TIMU ya soka ya Waendesha pikipiki maarufu kwa jina la Bodaboda ya Uyole imeibuka kidedea katika fainali ya Kombe la Bodaboda dhidi ya timu ya Kabwe katika kipute kilichopigwa juzi katika uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge Soweto jijini Mbeya.
Katika fainali hizo ambazo zimedhaminiwa na Kampuni ya vinywaji baridi ya Cocacola Kwanza Mbeya, Mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harisson Mwakyembe aliyekabidhi zawadi mbali mbali kwa washindi.
Timu ya Uyole aliibuka kidedea baada ya kuwafunga timu ya Kabwe kwa magoli mawili kwa nunge magoli yaliyopatikana kupitia kwa Miraji Juma aliyefunga goli dakika ya 41 kipindi cha Kwanza baada ya piga ni kupige katika lango la Kabwe.
Baraka Agogo aliandikia goli la pili na la ushindi timu yake ya Uyole baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa timu ya Kabwe dakika ya 75 na kufanya hadi mwisho wa mchezo Uyole 2 na Kabwe 0 katika mpambano ulioamuliwa na Mwamuzi Ngole Mwangole.
Awali katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu ulizikutanisha timu za Soweto na Iyunga ambapo timu ya Iyunga ilijinyakuliwa nafasi ya Msindi wa tatu baada ya kuifunga timu ya Soweto magoli matatu kwa bila.
Magoli ya timu ya Iyunga yalifungwa na Salim Mvungi dakika ya 30, na magoli mawili yakifungwa na mshambuliaji hatari Pinto Iman katika dakika za 70 na 76 na kuwaacha wapinzani wao wakiishia katika nafasi ya nne hadi kipenga cha mwisho kilichopulizwa na mwamuzi Kefa Kayombo.
Ligi hiyo iliyoandaliwa na kampuni ya City Sign Promotion & marketing Agency ya jijini Mbeya ilianza kutimua vumbi Juni 14, Mwaka huu baada ya kufunguliwa na Waziri Mwakyembe kabla ya kuifunga tena Julai 26, Mwaka huu.
Dk. Mwakyembe alikabidhi zawadi kwa washindi ambapo mshindi wa Kwanza ambao ni timu ya Uyole alikabidhiwa Kombe pamoja na mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi Milion mbili kwa ajili ya ununuzi wa Pikipiki mpya aina ya Boxer, pamoja na mpira mmoja.
Mshindi wa pili timu ya Kabwe ilikabidhiwa mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi lai saba(700,000) pamoja na mpira mmoja huku mshindi wa tatu timu ya Iyunga ikikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Laki tatu(300,000) pamoja na mpira mmoja huku mshindi wa nne  timu ya Soweto ikiambulia mpira mmoja.
Aidha Dk. Mwakyembe pia alikabidhi zawadi kwa mfungaji bora ambaye alikuwa ni Emanuel Luole kutoka Timu ya Stendi ya Umalila Mbalizi aliyejinyakuliwa mfano ya hundi ya shilingi laki moja baada ya kufikisha magoli saba, Goli kipa bora alitoka tiku ya Kabwe Zakaria Lugano aliyepata Shilingi Laki Moja pamoja na timu yenye nidhamu ambayo ni Ilomba iliyojipatia shilingi laki moja.
Hata hivyo Waziri Mwakyembe baada ya kumaliza kukabidhi zawadi zilizotolewa na wadhamni ambao ni Kampuni ya Cocacola pia alijitolea zawadi kwa ajili ya mwamuzi bora na mshika kibendera bora ambao aliwapa shilingi laki moja kila mmoja.
Wakati huo huo Waziri Mwakyembe alitimiza ahadi yake kwa chama cha Waendesha bodaboda Mkoa wa Mbeya kwa kuwakabidhi pikipiki mbili mpya pamoja na jezi mbili za mpira wa miguu kwa ajili ya timu ya jiji itayoundwa baada ya kumaliza ligi hiyo.
Mwisho.

Na Mbeya yetu

Sunday, July 27, 2014

MKUU WA MKOA MBEYA ABBAS KANDORO AZINDUA BARABARA YENYE UREFU WA KILOMETA 2 JIJINI MBEYA

Mkuu wa Mkoa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi  wa barabara  akiwa pamoja na Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga  wa kwanza kushoto pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dr.  Norman Sigalla wa Pili kushoto na  Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Dr.  Samuel Lazaro wa kwanza kulia 

Wakishangilia kwa pamoja mara baada ya kukata utepe


Mkuu wa Mkoa akipeana Mkono wa pongezi na Mkurugenzi wa miradi wa Kampuni ya CICO Ndugu Meng Yuan kampuni ambayo imejenga barabara hiyo.


Hii ndiyo Barabara iliyozinduliwa
Baadhi ya viongozi toka MUST  wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi

 Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya wakiwa katika eneo la Uzinduzi wa barabara hiyo 

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro akizungumza katika ufunguzi wa barabara mpya kutoka eneo la Meta hadi Stendi kuu ya Mabasi jijini Mbeya yenye urefu wa kilomita 2

Dr Norman Sigalla Mkuu wa wilaya ya Mbeya akimkaribisha mgeni rasmi

Meya wa Jiji la Mbeya ,Athanas Kapunga akiongea na wananchi katika uzinduzi wa barabara hiyo


 Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Dkt.Samweli Lazaro amesema kuwa  ujenzi wa barabara hiyo umemalizika kwa mkataba wa grama ya sh. Bil.1,553,437,275.00 alipokuwa akisoma taarifa fupi kwa mgeni rasmi


Waheshimiwa Madiwani








Na Mbeya yetu

 
 
offline
Click here to leave a message
Gmail

No comments:

Post a Comment