
Mshambuliaji
wa Uholanzi na Bayern Munich Arjen Robben, 30, amekataa 'ofa' ya
kujiunga na meneja wake Louis van Gaal, Old Trafford (Daily Telegraph).
Meneja
wa Arsenal, Arsene Wenger ana matumaini ya kukamilisha usajili wa kipa
wa Colombia David Ospina, 25, kutoka klabu ya Nice wiki hii (Daily
Mirror).
Chelsea
wameanza mazungumzo kuhusu kumrejesha Didier Drogba, 'Darajani' kuwa
mshambuliaji wa akiba na kocha (Daily Mail), mshambuliaji wa Liverpool
Iago Aspas, 26, anajiandaa kujiunga na Sevilla kwa mkopo msimu wote ujao
(Liverpool Echo), mipango ya uhamisho ya Tottenham imekwama kwa sababu
kiungo Gylfi Sigurdsson, 24 na beki Michael Dawson, 30, hawataki
kuondoka (Daily Mirror), wakala wa beki wa Spurs Jan Vertonghen, 27,
amekiri kuwa mchezaji huyo huenda akaondoka White Hart Lane (Evening
Standard), Liverpool wameanza tena kumfuatilia beki wa kushoto wa
Sevilla Alberto Moreno (Daily Express)(P.T)
Kocha wa
Marekani Jurgen Klinsmann amesema amekataa 'ofa' kibao kutoka Ulaya,
ikiwemo Galatasaray (Le Figaro), mshambuliaji wa Monaco, James
(inatamkwa Hamez) Rodrigues, 23, amesisitiza kuwa anataka kuichezea Real
Madrid, akisema ni juu ya rais wa klabu hiyo kufanya uamuzi (Marca),
Lazar Markovic atafanya vipimo vya afya Liverpool Jumatatu, kabla ya
kukamilisha uhamisho wake wa euro milioni 25. Brendan Rodgers anataka
kumchukua pia Wilfried Bony kuziba nafasi ya Luis Suarez (Daily
Telegraph)
Boss wa
Chelsea Jose Mourinho anataka kumchukua Sami Khedira. Arsenal walikuwa
wakimtaka mchezaji huyo, lakini sasa wataanza kumfuatilia zaidi Lars
Bender (Daily Mail), Liverpool huenda ikaingia Southampton tena, safari
hii wakimtaka Jay Rodriguez kuchukua nafasi ya Iago Aspas (Daily Mail),
Manchester United inakaribia kumsajili kiungo kutoka Chile, Arturo Vidal
anayechezea Juventus.
United
wamekubaliana ada ya uhamisho ya euro milioni 40, na kuhama kwa Patrice
Evra kwenda Juve (Marca), Juventus watamfuatilia Paulinho kutoka
Tottenham iwapo watamuuza Arturo Vidal (Daily Express), Manchester
United watakabiliwa na ushindani kutoka Barcelona kumsajili beki wa kati
wa Borussia Dortmund Mats Hummels. Luis Enrique anamtaka Hummels baada
ya mazungumzo ya kumsajili Marquinhos kuvunjika (Daily Star).
Share
tetesi hizi na wapenda soka wote. Tetesi nyingine kesho. Uhamisho wowote
ukithibitishwa nitakufahamisha. Kesho tukijaaliwa-Cheers!
Kutoka kwa Salim Kikeke
No comments:
Post a Comment