Mbeya/Moshi.
Rais Jakaya Kikwete amesema msimamo wa wajumbe wa Bunge la Katiba
wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umemweka njiapanda sawa na
Watanzania wengine wanaoshangaa.
Rais
Kikwete aliyasema hayo jana alipohutubia waumini wa Kanisa la Tanzania
Assemblies Of God (TAG) waliokusanyika kwenye Uwanja wa Sokoine jijini
hapa kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo nchini. (MWANANCHI)(FS)
“Kwa sasa
matumaini pekee ya Ukawa kurejea bungeni ni mazungumzo yanayoendelea,
yanayovihusisha vyama vinne vikubwa nchini chini ya Msajili wa Vyama vya
Siasa, Jaji Francis Mutungi,” alisema Rais Kikwete.
Kauli ya
Rais Kikwete ni ya pili kwa kiongozi wa juu kuwazungumzia Ukawa kuiweka
Serikali njiapanda baada ya ile ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyoitoa
Juni 26 mkoani Tanga.
Pinda
alisema hatima ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu utategemea
uamuzi wa wajumbe wa Ukawa kurejea bungeni. Alikuwa akizungumza na
mameya na wenyeviti wa halmashauri za wilaya na miji nchini ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Serikali za Mitaa.
Awali
Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Dk Barnabas Mtokambali akizungumza wakati wa
kumkaribisha Rais alimwomba kuingilia kati kuhakikisha Bunge la Katiba
linatimiza matakwa yaliyokusudiwa.
Askofu
Mtokambali alimsihi Rais kukwamua mgogoro uliopo kwa kuhakikisha wajumbe
wa Bunge la Katiba wanaungana na kutekeleza matakwa ya sheria, kanuni
ya kupata Katiba Mapya.
Akijibu,
Rais Kikwete alisema masikitiko ya Askofu huyo na Watanzania wengine ni
sawa na masikitiko yake na kwamba rai yake ni kuwasihi wajumbe hao
wajipange kurejea kwenye mkutano ujao wa Bunge la Katiba.
Hata
hivyo, alifafanua kwamba hatua pekee ambayo inatoa mwanga wa kuleta
suluhu ni ile aliyoichukua msajili wa vyama vya siasa nchini kuwaita
viongozi wakuu wa vyama vya CUF, Chadema, CCM na NCCR-Mageuzi hivi
karibuni ambako viongozi hao wameonyesha ukomavu katika mazungumzo
mazuri na yenye mwelekeo wa matumaini.
“Nampongeza
msajili wa vyama vya siasa kwa hekima aliyoitumia kwa kuanzisha
mazungumzo hayo na nawashukuru sana viongozi wa vyama vya siasa husika
kwa kujadili kwa busara yenye mwelekeo wa kutatua tatizo hilo,” alisema.
Alisema
vyama vinavyoshiriki kwenye mazungumzo hayo ndiyo vikubwa nchini na kwa
vyovyote vile mambo yatakwenda vizuri hata hivyo alifafanua kuwa
mazungumzo ya aina hiyo pia yanatarajiwa kuwashirikisha wadau wengine.
Nawaomba
maaskofu, masheikh, wachungaji, maimamu, manabii kuwaombea wajumbe wa
Bunge Maalumu la Katiba Mpya warudi bungeni Agosti 5 kukamilisha kazi
ndani ya siku 60 nilizowaongezea bila kuomba nyingine tena,’’ alisema.
No comments:
Post a Comment