Jaji Maneto
Wakati
matukio ya milipuko ya mabomu yakiendelea katika baadhi ya mikoa nchini,
aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji
Mstaafu Amir Manento amelinyooshea kidole jeshi la polisi kwa madai kuwa
linahusika na baadhi ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika
vipindi tofauti nchini.
Akizungumza
katika mahojiano maalumu na waandishi wa Mwananchi nyumbani kwake
Oysterbay juzi, alisema ingawa matukio hayo yalianza taratibu, Polisi
ilishindwa kuchukua uamuzi wa haraka wa kuyazuia yasiendelee.
Aidha,
alisema kuwa wakati akiwa katika Tume ya Haki za Binadamu na Utawala
Bora, walifanya utafiti wa matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu,
ambapo walibaini kuwa polisi walishiriki kumpiga bomu mtu mmoja na
mwingine risasi katika matukio tofauti.(P.T)
"Jeshi linapofanya hayo madhambi nani ataliambia, maana polisi ni wakala wa dola (state agency)," alifafanua.
Alieleza
kuwa kinachotokea hivi sasa nchini ni sawa na hadithi ya kinyonga na
inzi, ambapo kinyonga huanza kumtishia inzi kwa kumshtua huku akiendelea
kumsogelea taratibu na kisha hutoa ulimi haraka na kummeza.
"Tusiendelee
kubaki kusema kwenye majukwaa kuwa hiyo amani itapotea, inaanza kidogo
kidogo yule kinyonga alianza kurusha mguu mmoja akauweka pale chini pu!
Akasikiliza, je, anaondoka? Akarusha mguu wa pili...," alifafanua zaidi.
Baadhi ya
matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yaliyowahi kutokea hivi
karibuni ni pamoja na milipuko ya mabomu, watu kumwagiwa tindikali,
uchomaji wa makanisa, utekaji nyara na mauaji ya raia kwenye mikusanyiko
na kwenye maandamano ya kisiasa.
Akitoa
mfano, Jaji Manento alisema katika tukio la kwanza la mlipuko wa bomu
kwenye mkutano wa Chadema jijini Arusha, Jeshi la Polisi lilishindwa
kutekeleza wajibu wake kutokana na kusikiliza kauli za viongozi wa
kisiasa.
"Viongozi
fulani wa siasa wakasema wamejipiga wenyewe, badala ya kuangalia kama
kuna haki za binadamu zimekiukwa. Kuna binadamu wamekufa, wamepigwa
bomu, kwa hiyo inawezekana hao watu wanaoshughulikia usalama wakaacha
kufanya wajibu wao wa kuangalia nani kapiga hili bomu. Wakaona
imekubalika kwa sababu imeongelewa kwenye vyombo vya habari kuwa
wamejipiga wenyewe.
"Kwa
hivyo, siasa kwa kiasi fulani inaingizwa ingizwa...lakini sasa unakuta
vile vyombo ambavyo vinatakiwa kuchunguza na kupeleleza haki za binadamu
havifanyi kazi inavyopaswa ifanywe. Vyombo hivyo ni hivi vya usalama
vinavyopaswa kulinda watu na mali zao," alisema.
Jaji
Manento aliyewahi kuwa Jaji Kiongozi, alisema kutokana na polisi
kutokuwa wazi katika kushughulikia vitendo vya ukiukwaji wa haki za
binadamu, wananchi wengi wanaamini kuwa chombo hicho cha ulinzi
kinahusika na matukio hayo.
"Sisemi
kwamba linahusika moja kwa moja ila wananchi wataendelea kuwa na mawazo
hayo, kwa sababu ya kutoelezwa ukweli. Hatua zikichukuliwa haraka, watu
watafarijika, kama watu wanasema wewe ndiyo mwizi wala hukanushi, kwa
hivyo watu wanaamini wewe unahusika," alisema Jaji na kuongeza:
Chanzo:Mwananchi
No comments:
Post a Comment