Wednesday, 2 July 2014

BALOZI WA LIBYA NCHINI TANZANIA AFARIKI KWA KUJIPIGA RISASI


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania leo imepokea taarifa kutoka ubalozi wa Libya hapa nchini ikieleza kuwa aliyekuwa Kaimu Balozi wa Libya Bw. Ismail Nwairat, amefariki dunia jana kwa kujipiga risasi.


Taarifa hiyo ya ubalozi imeeleza kuwa kifo hicho kimetokea majira ya saa saba mchana ofisini kwa kaimu balozi huyo katika jengo la ubalozi wa Lbya ambapo imeelezwa kuwa marehemu alijifungia ofisini na kujifyatulia risasi kifuani upande wa kushoto.

Maafisa ubalozi walivunja mlango waliposikia mlipuko wa bunduki na kumkuta Kaimu Balozi Nwairat ameanguka chini na kuamua kumkimkimbiza hospitali ya AMI Oysterbay ambako alitangazwa kuwa amekwisha fariki, kifo ambacho kimethbitishwa pia na jeshi la polisi

Maiti imehamishiwa hospitali ya taifa Muhimbili na kwamba ubalozi unafanya maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu Nwairat kwenda nchini Libya kwa mazishi na kwamba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeuhakikishia Ubalozi wa Libya ushirikiano wake katika kipindi hiki kigumu.

No comments:

Post a Comment