Friday, 20 June 2014

RAS INNOCENT AKONGA NYOYO ZA WANZIBARI ...



DSC_0397
Mkali wa muziki wa rege nchini, Innocent Nyanyagwa na bendi yake wakitumbuiza kwenye tamasha la 17 la ZIFF 2014 linaloendelea kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
DSC_0438
Na. Mwandishi wetu, Zanzibar
MKALI wa muziki wa rege nchini Innocent Nganyagwa anajiandaa kutoa filamu inayohusu maisha yake kama sehemu ya kufunza kizazi kijacho kuhusu muziki huo.
Filamu hiyo ambayo itabeba maisha yake ya kuishi katika muziki wa rege inatolewa kama ile ya Jimmy Clief The hader they Come.
Nganyagwa mwenye albamu nne na tuzo tano za hapa nyumbani alisema pamoja na kukaa kimya kwa muda mrefu alikuwa hajaondoka katika muziki wa rege lakini alikuwa anafundisha vijana ili rege iwe na undelevu nchini.
Nganyagwa ambaye alitumbuiza kwenye viunga vya Mambo Club iliyopo Ngome Kongwe amesema kwamba amekuja katika tamasha la ZIFF akiwa na mpya nyingi kuonesha wazi kwamba hakuwa mkaa bure.
Akijibu swali kuhusu mahadhi ya muziki wake na imani yake ya kirastafarian amesema kwamba muziki wa rege japo upo ndani ya imani ya kirasta, unasimama wenyewe ndio maana mtu kama yeye hapigi rege ya Jamaica kama ilivyokuwa kwa Jimmy Clief, Burning Spear au Bob Marley.
Amesema muziki wake ni wa kitanzania kwa sababu taifa hili lina vionjo vingi vya kufanya katika kuuza utamaduni wake nje kupitia muziki.
Amesema japo miondoko ya mfumo wa Babylon bado ipo kuna mstari mwembamba sana kati ya dini ya rasta na muziki wa rege na mwitikio wa muziki wa ukombozi.Hata hivyo amesema kwamba sasa hivi anapiga muziki ‘mtamu’ (sweetie reggae) muziki wa mapenzi.
Innocent Nyanyagwa na Back Vocalist wake wakishambulia kwenye tamasha la 17 la ZIFF 2014 ndani ukumbi wa Mambo Club-Ngome Kongwe.
Akizungumza uuzaji wa muziki wa Tanzania nje, amesema ipo haja ya wasanii kuacha kukopi na kupest (kunakiri) kwani kwa kufanya hivyo hawauzi utamaduni na hivyo wanainyima nchi fursa ya kujulikana mwisho.
“Ipo haja ya kutangaza utamaduni wetu” alisema Nganyagwa.
Aidha aliitaka serikali kuwekeza katika muziki kwa kuingilia usambazaji wa bidhaa hizo ili wasanii waweze kunufaika zaidi kuliko sasa.

Ras Inno akiwapa mzuka mashabiki wake kwa kuruka na wamasai ndani ya Ngome Kongwe alipotoa show ya aina yake baada ya kuhudhuria tamasha la ZIFF miaka nane iliyopita.

DSC_0475
Watu weweeee....Haire rastafarai.....full mzuka babaake.!

No comments:

Post a Comment