Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema mashambulizi mawili yaliyowauwa watu zaidi ya 60 kisiwani Lamu hivi karibuni hayajafanywa na kundi la Al Shabab bali na mtandao wa wanasiasa waliopo nchini humo na wahalifu.
Akiongea
wakati wa hotuba yake kuhusiana na mashambulizi hayo, Rais Kenyatta
amesema kuna ushahidi unaoonesha mashambulizi yalipangwa na baadhi ya
wanasiasa wanaotaka kuanzisha mapigano ya kikabila dhidi ya wakenya.(MC)
Ameongeza
kuwa katika siku za hivi karibuni wakenya wameshuhudia siasa chafu
ambazo zinalengo la kuwafanya watu wavunje sheria pamoja na kuleta
vurugu katika nchi hiyo. "Hili halikuwa shambulizi la Al Shabab,
ushahidi unaonesha kuwa mtandao wa wanasiasa wa hapa nchini wanahusika
katika kupanga na kutekeleza shambulizi hili la kutisha" alisema Rais
Kenyatta.
Sehemu ya eneo la Mpeketoni iliyaoharibiwa na shambulizi ambalo kundi la Al-Shabaab lilidai kuhusika nalo.
Wapinzani wakosoa matamshi ya rais
Kufuatia
kali hiyo ya Rais Kenyatta, baadhi ya wanasiasa hususani wale wa vyama
vya upinzani wameikosoa kauli yake hiyo. Anyang Nyon'go ambaye ni Katibu
Mkuu wa chama cha upinzani CORD, amemkosoa rais Kenyatta kwa kusema huu
sio wakati wa kunyosheana vidole vya lawama bali ni wakati wa kuungana
kama wakenya kuhakikisha usalama dhabiti unapatikana nchini humo.
Nyon'go
hata hivyo amesema matamshi yaliyotolewa na rais Kenyatta kwa sasa
yamekosa muelekeo na kumtaka kutoa ushahidi alionao dhidi ya madai ya
wanasiasa kuhusika katika mashambulizi.
Kauli
hiyo ya Rais Kenyatta kuyahusisha mashambulizi hayo ya hivi karibuni na
mtandao wa wanasiasa nchini humo inakuja wakati ambapo kundi la Al
Shabab kukiri kuhusika katika mashambulizi hayo kutokana na Kenya
kushindwa kuondoa majeshi yake nchini Somalia ambayo yanaisaidia
serikali ya nchi hiyo kupambana na kundi hilo la kaigaidi.
"Shambulizi
la pili lilikuwa na mafanikio" alisema mmoja wa wapiganaji wa kundi la
Al Shabab wakati alipokuwa anaongea na kituo cha Andalus ambacho huwa
kinatumiwa mara kwa mara na kundi hilo la kigaidi.
Lakini
baadhi ya wachambuzi wa masuala ya usalama wanaelezea wasiwasi wao kama
ni kweli mashambulizi hayo yametekelezwa na kundi hilo, Matt Bryden
ambaye ni mkuu wa zamani wa kundi la uangalizi la Umoja wa Mataifa
nchini Somalia na sasa akiwa ni mkuu wa kituo cha utafiti cha Sahan
anasema kuwa Al Shabab haijawahi kukiri kuhusika katika shambulizi
lolote ambalo imeshawahi kufanya huku pia hakuna ushahidi wa kundi
lolote la Kenya ambalo lina uwezo wa kufanya shambulizi kubwa na lenye
mbinu kama zilizotumika katika mashambulizi hayo.
Raia wajawa na wasiwasi
Raia
wengi wa Kenya wameonesha kuwa na wasiwasi na mbinu ambazo zinatumiwa
na serikali katika kupambana na matukio ya kigaidi tokea litokee
shambulizi katika jengo la biashara la Westgate mwaka jana.
Serikali
ya nchi hiyo imeanzisha mikakati mbalimbali ya usalama ikiwemo ule wa
uangalizi kati ya watu wanaoishi katika maeneo ya majirani, upigwaji
marufuku wa matumizi ya magari yanayosafirisha abiria yenye vioo ambavyo
havioneshi ndani lakini pia kampeni ya utoaji taarifa.
"
Kenyatta anajaribu kutuambia kuwa suala la usalama ni jukumu letu, sio
kweli usalama ni jukumu la serikali" alisema mmoja wa wanaharakati
nchini humo Boniface Mwangi.
Kumekuwepo
pia na taarifa ya kufukuzwa kazi au kuhamishwa kwa maafisa wa polisi wa
Mpeketoni ambako ndipo shambulizi moja lilitokea na kufuatiwa na lile
la kijiji cha Poromoko, lakini baadhi ya raia wa Kenya wanakasirishwa na
kitendo cha serikali ya nchi hiyo kuwaacha maafisa wa juu wa polisi
ambao wameteuliwa kisiasa.
CHANZO DW...............Mathias Cana
No comments:
Post a Comment