Kaimu
Mkurugenzi Dr. Samwel Lazaro, Meya wa Jiji la Mbeya Atanus Kapunga,
Mkandarasi Nadhra Iqbal Singh wa kampuni ya Nadhra Engineering
&Construction company Limited,Naibu Meya Chieforder Fungo,
Mkandarasi Mshauri
Liberate Materu akiongea
soko Jipya
Hawa ni Madiwani , Wakuu wa Idara na wataalam
Meya wa Jiji Atanus Kapunga akiongea
Mkandarasi
Mkurugenzi akiongea
Naibu Meya akiwa na Mkandarasi
Meya akiwa na Mkandarasi
Waandishi wa Habari
ziara
BAADA
ya kusuasua kwa muda mrefu kukamilika kwa ujenzi wa Soko la Kimataifa
la Mwanjelwa jijini Mbeya,kulikotokana na Mkandarasi aliyekuwa akijenga
kushindwa kukamilisha kutokana na muda aliyopewa na kujitoa, Soko hilo
limepata Mkandarasi mpya.
Umaliziaji wa jengo la soko hilo unatarajiwa kuanza Julai Mosi mwaka huu baada
ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya kushinda kesi dhidi ya mkandarasi wa
awali kutoka Kampuni ya Tanzania Building Works ya jijini Dar es Salaam.
Makabidhiano ya mradi huo kwa mkandarasi mpya kutoka Kampuni ya Nandhra Engineering & Construction Company(MD) na Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, yalifanyika hivi karibuni katika majengo hayo yaliyopo Mwanjelwa jijini hapa.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Kapunga alisema hatua ya Halmashauri kumkabidhi soko
hilo mkandarasi huyo mpya ni baada ya yule wa awali kushindwa
kukamilisha ujenzi wa soko kwa wakati.
Alisema
Julai 2012 soko hilo lilipaswa kukamilika na kukabidhiwa kwa uongozi
wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya jambo ambalo halikufanyika licha ya
kupewa muda wa ziada kwa awamu tatu za wiki 20 ambapo tena alishindwa
kukamilisha hadi Julai 19, mwaka 2013 alipoandika barua ya kuvunja
mkataba.
Alisema
kutokana na changamoto hizo ujenzi wa soko hilo ulisimama kwa zaidi ya
miezi 10 tangu Mkandarasi wa awali asitishe mkataba wake na kwamba
ujenzi huo unatarajia kuanza Julai Mosi mwaka huu na kukabidhi soko
hilo Marchi 2015.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Dk. Samwel Lazaro,
alisema mkandarasi huyo anatarajia kutumia shilingi bilioni 5.0 katika
kukamilisha ujenzi wa soko hilo ambao mpaka sasa umekamilika kwa
asilimia 80 na kutumia zaidi ya shilingi Bilioni 11 kati ya Bilioni 13 .
Alisema
katika kiasi hicho cha fedha cha shilingi bilioni 13 kiasi kilichobakia
ni shilingi Bilioni 1.8 hivyo kuilazimu Halmashauri hiyo kukopa tena
kiasi cha fedha cha shilingi Bilioni 3.5 kutoka Benki ya CRDB kwa ajili
ya kumalizia ujenzi huo.
Kwa
upande wake, Mkandarasi mpya Nadhra Singh alihidi kuwa atahakikisha
kazi hiyo itakamilika katika kipindi walichoandikiana kwenye mkataba
hivyo serikali kuondoa mashaka.
January
25,2010 serikali ilimpa miezi 18 mkandarasi kutoka Kampuni ya Tanzania
Bulding Works Limited ya jijini Dar es Salaam kuhakikisha soko hilo
linakamilika na kukabidhiwa kwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Agosti 24/
2012 lakini alishindwa kwenda na muda wa makubaliano hivyo kusababisha
kuvunja mkataba na halmashauri.
Ujenzi wa Soko hilo ni
kutokana na kuteketea kwa moto kwa soko la awali mwaka 2006 na
kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha kutoka kwa wafanyabiashara
zaidi ya 2000 walionguliwa maduka yao.
Na habari talk
No comments:
Post a Comment