Thursday, 16 April 2015

ACT NA UKAWA SASA NGOMA INOGILE,HII IMETAMKWA NA ZITTO

Zitto akiwahutubia wananchi Manyoni Mjini
Mkazi wa Manyoni Mjini Mzee ambaye jinalake halikupatikana maramoja akichukua picha za video kwa kutumia simu mkutano wa ACT-Wazalendo.
CHAMA cha ACT-Wazalendo kimesema kinaweza kuunganisha nguvu na yama vingine vya upinzani ili kukiondoa chama cha mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu ujao ambapo alisema shauku kubwa ya wananchi ni kutaka kujua msimamo wa ACT Wazalendo katika kushirikiana na vyama vingine vya siasa ili kufanikisha malengo ya kuiondoa CCM katika madaraka.
Kauli hiyo ilitolewa LEO mjini Singida na Kiongozi wa ACT wazalendo Zitto Kabwe wakati akihutubia mamia ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi ukombozi.
"Tumedhamiria kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kuubomoa mfumo  unaonyonya wananchi. Msimamo wetu upo wazi na tumeueleza mara kadhaa"alisema na kuongeza
“ACT- Wazalendo tunaunga mkono juhudi zozote za kushirikiana kwa vyama na hili linathibitishwa na jina letu Alliance na msimamo wetu kuhusu mabadiliko ya Katiba. Kubwa tunataka ushirikiano utakaonufaisha wananchi na sio ushirikiano wa kugawana nafasi za uongozi,” alisema Zitto.
Wakazi wa Mji wa Singida wakishangilia viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo wakati waa mkutano huo jijini humo leo.
 Kiongozi huyo wa ACT alisema chama hicho hakina tatizo na kipo tayari kushirikiana na chama chochote kilichokuwa  tayari kushirikiana nao ikiwemo Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), 
Alisema umoja huo ni lazima uwe na malengo ya kujenga uchumi shirikishi wenye kuzalisha ajira nyingi na bora, wenye mfumo wa hifadhi ya jamii kwa wananchi wote na wenye kutokomeza umasikini.
Alikanusha chama hicho kutoa  kauli yeyote dhidi ya UKAWA kama inavyoaminishwa na baadhi ya watu, bali wameweka wazi kuwa lazima misingi ya kiitikadi na kifalsafa izingatiwe katika ushirikiano wowote
"Tupo tayari kwa umoja kwani ni moja ya misingi mikuu 10 ya chama chetu na umoja ni nguvu,” alisema Zitto.
Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, akisalimiana na mzee ambaye alitumia muda mwingi kuwapiga picha za ideo viongozi hao wakiwa kwenye mkutano Manyoni mjini.
 Akizungumzia hali ya umaskini kwa mkoa wa Singida, Zitto alisema pamoja na hali ya umaskini Serikali ya CCM, imeshindwa kupunguza umasikini, nchini kwa kiasi kikubwa na kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Alisema ripoti ya maendeleo ya binadamu imeonyesha kuwa Tanzania imeshuka kufikia daraja la chini la nchi zenye kiwango kidogo zaidi cha maendeleo ya binadamu.
“Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya UNDP kuhusu Maendeleo ya Binadamu duniani ya mwaka 2014 ambayo imeiweka Tanzania katika kundi la nchi zenye maendeleo ya binadamu ya kiwango cha chini.  Lakini kinachoshitusha ni kushuka kwa nafasi saba zaidi katika Kipimo cha maendeleo ya binaadamu, (HDI), ukilinganisha na mwaka 2013.
“Ushahidi mzuri wa jambo hili ni ule unaotolewa na kipimo cha Maendeleo ya Binadamu (HDI), ambacho hupima maendeleo ya binadamu katika nchi kwa kuzingatia mkusanyiko wa vigezo vya umri wa kuishi, elimu na kipato,” alisema Zitto
Zitto akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kintintu mara baada ya kuzindua tawi la chama hicho
Viongozi wa ACT -Wazalendo wakishangilia na wananchi wa wilayani Manyoni baada ya kuzindua tawi la Manyoni Mjini.


 Amesema katika ngazi ya mikoa, ripoti hiyo  inaonyesha tofauti kubwa ya viwango vya maendeleo ya binadamu ndani ya Tanzania.
Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Iringa, Ruvuma, Mbeya, na Tanga ndiyo mikoa yenye kiwango cha juu cha maendeleo ya binadamu.
“Singida inazalisha alizeti na sasa hivi tunajua kwamba watu wanaojali afya zao, wanapenda kula mafuta ya alizeti na ukiongelea mafuta ya alizeti, basi yale yaliyo bora yanatokana katika mkoa huu. Lakini pamoja na fursa hiyo ambayo inaweza kuitumia ili kuinua hali ya maisha ya wananchi,” alisema
Alisema Mkoa wa Singida una madini lakini jambo la kushangaza bado umekuwa mkoa wa kwanza kwa umaskini huku madini hayo yakishindwa kuwanufaisha wananchi hasa wanaozunguka vijiji vya Sambaru na Londoni.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Anna Mghwira,  alisema sasa umefika wakati ni lazima nchi iwe huru kwa kuwa na misingi imara itakayoimarisha demokrasia nchini.
“Rais aitishe Bunge maalumu ili kufanya marekebisho madogo ya Katiba kuruhusu uchaguzi huru na wa haki lakini pia Wajumbe wa Tume waombe kazi na wawe wataalamu.
Alisema ACT inashauri kuitishwa kwa Bunge Maalumu ni kutokana Bunge la sasa la 10 lina uhai wa mkutano mmoja kabla ya kuvunjwa.
“… hivyo Katibu wa Bunge atangaze nafasi za wajumbe wa Tume, kamati ya Bunge ya Katiba Sheria na Utawala itafanya mahojiano ya wazi na kupata majina 22 yatakayopelekwa bungeni,” alisema Anna.PICHA ZOTE ZA MKUTANO ZIPO CHINI
Zitto akisalimiana na wakazi wa Manyoni Mjini
Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe na Mwenyekiti wa Chama hicho Anna Mghwira wakizindua tawi la chama hicho kwenye Kijiji cha Kintintu wilayani Manyoni mkoani Singida.

Wednesday, 15 April 2015

RIPOTI YA POLISI KUHUSU AJALI ZILIZOUA WATU 969 KWA SIKU 102



Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani DCP Mohammed Mpinga
Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani DCP Mohammed Mpinga
WAKATI Rais Jakaya Kikwete akiungana na Watanzania kuomboleza vifo vya watu 19 walioteketea katika ajali ya basi lililoungua moto baada ya kugongana na lori juzi mjini Morogoro, imefahamika kuwa, ajali za barabarani zimegharimu maisha ya watu 969 kati ya Januari Mosi na Aprili 12 mwaka huu.
Aidha, watu 2,500 wamejeruhiwa katika kipindi hicho, wengine wakisababishiwa ulemavu wa kudumu kutokana na ajali hizo. Hii ina maana kwamba, kwa wastani, watu 10 walipoteza maisha katika ajali za barabarani kila siku kati ya Januari na Aprili 12 mwaka huu, ilhali waliojeruhiwa ni wastani wa watu 25 katika muda kama huo.
Hayo yalibainishwa jana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Mohammed Mpinga aliyesema hayo yametokea katika ajali za barabarani 2,224 za kati ya Januari na mwanzoni mwa Aprili.
Alisema watu 866 walikufa na wengine 2,363 kujeruhiwa kati ya Januari na Machi, wakati wengine 103 wamepoteza maisha na 138 kujeruhiwa kati ya Machi 11 na Aprili 12 mwaka huu.
Alisema katika ajali zote hizi chanzo kikubwa ni mwendokasi wa madereva bila kuzingatia alama na michoro ya barabarani na abiria kushabikia mwendo kasi na kumtetea dereva pindi anapofanya makosa.
"Dereva akifanya makosa akikamatwa abiria wanachangia kumlipia faini dereva jambo ambalo linawapa madereva kiburi wakiamini akifanya makosa abiria wanamsaidia," alisema Mpinga.
Aliongeza kuwa kwa upande mwingine wamiliki wa vyombo vya usafiri wanachangia ajali kwani wamekuwa wakiwadhibiti na kuwaamrisha madereva wao kwenda mwendo kasi na pale anapokosea anamlipia faini jambo ambalo linapelekea kutokea kwa ajali zinazopoteza maisha ya watu wengi na kuwaachia wengine vilema vya maisha.

AJALI YA BASI BWAWANI LIKIELEKEA MKOANI MBEYA.




Pichani ni basi aina ya Costa likitoka Dar es Salaam kuelekea Mbeya limepata ajali na kupinduka kama lionekavyo pichani juu baada ya kuyumba na kuacha njia eneo la Bwawani muda wa saa 12.30 jana jioni . Hakuna aliyepoteza maisha, ila Kuna majeruhi kadhaa ambao wanapatiwa matibabu katika kituo cha Afya cha Magereza ya Bwawani. Chanzo cha ajali kinasadikiwa kuwa ni mwendo kasi na utelezi kutokana na mvua iliyokuwa inanyesha wakati huo.Chanzo Mdau wa Blog ya Jamii.(Muro)

Tuesday, 3 February 2015

BONDIA FRANCIS CHEKA AHUKUMIWA JELA MIAKA 3


 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgb6tN_Yztflt9xmznGAMENYMD4mRW9na4TaIRD0TcGaKaAYP1p9ernAA2azXfnZpmfu-LetT8joGS-WPlctoiDlo67_nLHiNk3Giug23s-439QB-5iw4kLnVH-BbW7MVSfkICiTm3xhag/s640/Bondia-Francis-Cheka.jpg
Bondia Francis Cheka leo February 2 2015 amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu na faini ya Milioni moja laki sita kwa kosa la kumpiga mmoja kati ya wafanyakazi wake
kwenye bar yake iliyopo Morogoro.

cheka

Muda mfupi uliopita Francis Cheka ameongea na millardayo.com na kusema ndio alikua anajiandaa kuachia simu yake na vitu vingine muhimu ili achukue karandinga kuelekea gerezani ambapo namnukuu akisema ‘imeshakua hivi tayari ila hamna noma, niko na wanangu wengine wamepigwa miaka 10 nitakua nao fresh tu ila hamna noma ni miaka mitatu tu mimi’

Hukumu imetolewa na Hakimu Mkazi Said Msuya ambapo baada ya hayo upande wa Francis Cheka unasemekana kujiandaa kukata rufaa.

Unaweza kubonyeza play hapa chini kumsikiliza Ahmad Machaku akiripoti kutoka Morogoro.

HATIMAYE OMEGA MEDIA PRODUCTION YATUA ARUSHA NA BAHATI BUKUKU

Kilio cha wengi jijini Arusha hatimaye kimepata mfuta machozi ni Omega Media Production ni baada ya kufanya matamasha mengi mikoani sasa ni zamu ya Arusha katika kuiweka wakfu albam ya mtoto Miriam Paul mwenye umri wa miaka  8 akiwa na uwezo wa ajabu wa kumwimbia Mungu na kulitawala jukwaa kwa kutumia talanta alizopewa na Mungu wa mbinguni.

Tamasha hili litafanyika jumapili ya tarehe 8/02/2015 katika kanisa la katoliki kijenge Arusha mjini kuanzia saa 8 mchana na kuendelea wakati huo huo atasindikizwa na waimbaji mbalimbali kama Bahati Bukuku Tumsifu Rufutu (mzee wa mwambie farao),Fred Ndumbaro,Redemption Tarimo,Mary Masonga,Beatrice Mwakalinga, Joseph Roma na Rose Paul bila kusahau  ENG.Carlos Mkundi na wengineo wengi.

Saturday, 31 January 2015

UNYAMA, UDHALILISHWAJI MTALAKA WA ISHA MASHAUZI UKWELI NI HUU


Stori: Musa Mateja/Risasi
HATIMAYE ukweli wa kutekwa, kuteswa kwa kudhalilishwa kwa aliyekuwa mume wa mwimba  taarab mahiri Bongo, Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’, Jumanne Hassan ‘Tevez’, umejulikana, Risasi Jumamosi limechimba.
Mfanyabiashara, Jumanne Hassan ‘Tevez’ akiwa amefungwa kamba na watesi wake.
Januari 28, mwaka huu, picha za Tevez akiwa ametoka kuteswa kwa kudhalilishwa zilisambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii huku wengine wakidai kisa ni kukutwa na mke wa  mtu, wengine wakisema ni dhuluma.
RISASI LAINGIA MTAANI KUCHIMBA
Risasi Jumamosi halikufanya haraka kuichapisha habari hiyo mpaka kuichimba kwanza ili kujua kisa na mkasa kamili ndipo iwapelekee wasomaji wake. Na ndivyo ilivyofanyika!
ENEO LA TUKIO
Risasi Jumamosi lilichimba na kubaini kuwa, tukio la Tevez kufanyiwa ukatili huo lilitokea kwenye mji wa Durban nchini Afrika Kusini ambako alikwenda kibiashara.
“Tukio si la Dar kama wanavyosema wengine, limetokea mjini Durban, Afrika Kusini. Si unajua jamaa (Tevez) ni mtu wa tripu za kibiashara!” alisema mtoa habari mmoja akiomba hifadhi ya jina lake.
Jeraha likiwa mgongoni mwa Jumanne Hassan ‘Tevez’ baada ya kuteswa.
WALIOFANYA UKATILI
Kwa mujibu wa chanzo hicho, watu waliomtenda Tevez ni jamaa zake anaofanya nao biashara ambayo Risasi Jumamosi halijaijua vizuri (ingawa kwenye mitandao ya kijamii wanadai ni madawa ya kulevya).
YATAJWA DHULUMA
Chanzo kikaanza kuanika historia nzima tangu Tevez hajafanyiwa utekaji na udhalilishwaji huo.
“Siku za nyuma Tevez alipewa mzigo nchini Tanzania ili awapelekee hao jamaa wa Afrika Kusini. Aliondoka jijini Dar kwenda Nairobi, Kenya kwa basi akiwa na begi.
“Alipofika Nairobi, ilidaiwa begi hilo alilisahau kwenye basi lakini wengine wanasema aliuuza Nairobi na kwenda Afrika Kusini akiwa na begi feki.”
TEVEZ AWASILI AFRIKA KUSINI, AKUMBANA NA MSALA
Habari zaidi zikachimbuka na kudai kwamba, Tevez aliwasili mjini Durban na kukutana na jamaa zake ambapo aliwaambia mzigo  aliusahau kwenye basi.
“Kumbe inasemekana jamaa aliyemuuzia mzigo Nairobi anafahamiana na jamaa wa Sauz na aliwapigia simu kuwaambia kwamba, ameuziwa mzigo na Tevez.
“Kwa hiyo mpaka Tevez anawasili kule, jamaa walikuwa wanajua hana mzigo kwa kuwa aliuuza Nairobi,” kilisema chanzo.
‘Tevez’ akiwa na moja ya wadau wenzake katika biashara anazofanya huko Durban.
ATEKWA, ADHALILISHWA
Ikaendelea kudaiwa kuwa, madai ya Tevez yaliwakera jamaa kwa vile walijua kila kitu, hivyo walimteka na kuanza kumtesa kwa kumvua nguo zote, wakamfunga kamba za manila za rangi ya bluu na kuanza kumtesa kwa adhabu mbalimbali ili kumkomesha.
Inadaiwa katika adhabu hiyo, jamaa hao walimpiga na kitu chenye ncha kali hali iliyosababisha Tevez atokwe na damu na ngozi kuchubuka eneo la mgongoni.
MADAI WAKATI WA UDHALILISHWAJI
Inadaiwa wakati udhalilishaji huo ukiendelea, jamaa hao walikuwa wakisema wanachotaka ni mzigo wao na si kitu kingine.
MARAFIKI, JAMAA WA DAR
Kufuatia kusambaa kwa picha hizo mtandaoni, marafiki na jamaa wa Tevez waliopo Bongo walilazimika kufanya mpango kwa kuwasiliana na watu wa karibu waliopo Durban kumnusuru Tevez kwa kumpeleka hospitali ambako anapata matibabu hadi juzi, Alhamisi.
Risasi Jumamosi: “Kuna habari alikatwa sehemu za siri ni kweli?”
Chanzo: “Si kweli.”
Risasi Jumamosi: “Inasemekana alifanyiwa kitu mbaya cha mambo ya Sodama, ni kweli?”
“Si kweli. Watu wanasema tu. Ila walimtesa sana kwa kweli.”
Bw. Jumanne Hassan ‘Tevez’ akiwa na moja ya jamaa zake sauzi.
RISASI LATINGA DUKANI KWA MKEWE WA SASA
Ili kuzidi kupata habari zaidi, Januari 28, mwaka huu,  usiku Risasi Jumamosi lilikwenda Kinondoni Kwamanyanya, Dar kwenye duka la mke wa sasa wa Tevez ili kumsikia anasema nini kuhusu tukio hilo.
Paparazi wetu hakumkuta mke huyo lakini alibahatika kuongea na msichana aliyekuwa nje ya duka hilo na kumuuliza aliko Tevez.
Msichana: “Tevez yupo safarini Morogoro.”
Risasi Jumamosi: “Mbona hapatikani hewani? Nipe namba zake nyingine.”
Msichana: “Nilizonazo ndiyo hizohizo ulizonazo wewe, ni…(akazitaja).”
Kweli namba hizo ndiyo alizokuwa nazo paparazi wetu.
MAMA MKWE WA TEVEZ
Kesho yake, Risasi Jumamosi lilimsaka kwa simu mama mkwe wa zamani wa Tevez (mama wa Isha)  lengo ni lilelile, kutaka kujua kama naye ana taarifa hizo na anasemaje.
“Ni kweli nimesikia na nimeona picha zake yaani nimesikitika sana kiasi kwamba nikawa siamini kama ni  kweli yeye anaweza kufanyiwa ukatili wa aina hiyo.
“Kikubwa namshukuru Mungu kusikia yupo hai na kwa maana hiyo namuombea zaidi ili arudi katika afya yake,” alisema mama mkwe huyo aitwaye Rukia Juma.
Bw. Jumanne Hassan ‘Tevez’akiwa na mkewe.
MTU WA KARIBU NA TEVEZ
Risasi Jumamosi liliendelea kutafuta undani zaidi wa tukio la Tevez kwa kuongea na watu wake wa karibu waliopo Durban, ndipo likapenyezewa ishu mpya kuwa, baadhi ya ndugu na wafanyabiashara wenzake na Tevez wamechanga na kurudisha mali zilizokuwa zikidaiwa na jamaa hao.
“Nilikuwa Durban muda si mrefu na hapa ndiyo narejea nyumbani (Bongo). Kiukweli tukio la Tevez ndiyo habari ya mjini Sauz, maana jamaa wamemfanyia mbaya kinoma lakini kusema kweli hajakatwa nyeti kama mitandao ya kijamii inavyoandika, wamempiga sana.”
“Kingine ambacho ninajua tayari ameshatolewa kwenye jengo alilokuwa ametekewa na sasa yupo hospitali maalum ambayo siwezi kukutajia, ila huenda hali yake ikawa nzuri kama kweli atakuwa chini ya uangalizi wa madaktari,” alisema jamaa huyo.