Saturday, 31 January 2015

UNYAMA, UDHALILISHWAJI MTALAKA WA ISHA MASHAUZI UKWELI NI HUU


Stori: Musa Mateja/Risasi
HATIMAYE ukweli wa kutekwa, kuteswa kwa kudhalilishwa kwa aliyekuwa mume wa mwimba  taarab mahiri Bongo, Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’, Jumanne Hassan ‘Tevez’, umejulikana, Risasi Jumamosi limechimba.
Mfanyabiashara, Jumanne Hassan ‘Tevez’ akiwa amefungwa kamba na watesi wake.
Januari 28, mwaka huu, picha za Tevez akiwa ametoka kuteswa kwa kudhalilishwa zilisambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii huku wengine wakidai kisa ni kukutwa na mke wa  mtu, wengine wakisema ni dhuluma.
RISASI LAINGIA MTAANI KUCHIMBA
Risasi Jumamosi halikufanya haraka kuichapisha habari hiyo mpaka kuichimba kwanza ili kujua kisa na mkasa kamili ndipo iwapelekee wasomaji wake. Na ndivyo ilivyofanyika!
ENEO LA TUKIO
Risasi Jumamosi lilichimba na kubaini kuwa, tukio la Tevez kufanyiwa ukatili huo lilitokea kwenye mji wa Durban nchini Afrika Kusini ambako alikwenda kibiashara.
“Tukio si la Dar kama wanavyosema wengine, limetokea mjini Durban, Afrika Kusini. Si unajua jamaa (Tevez) ni mtu wa tripu za kibiashara!” alisema mtoa habari mmoja akiomba hifadhi ya jina lake.
Jeraha likiwa mgongoni mwa Jumanne Hassan ‘Tevez’ baada ya kuteswa.
WALIOFANYA UKATILI
Kwa mujibu wa chanzo hicho, watu waliomtenda Tevez ni jamaa zake anaofanya nao biashara ambayo Risasi Jumamosi halijaijua vizuri (ingawa kwenye mitandao ya kijamii wanadai ni madawa ya kulevya).
YATAJWA DHULUMA
Chanzo kikaanza kuanika historia nzima tangu Tevez hajafanyiwa utekaji na udhalilishwaji huo.
“Siku za nyuma Tevez alipewa mzigo nchini Tanzania ili awapelekee hao jamaa wa Afrika Kusini. Aliondoka jijini Dar kwenda Nairobi, Kenya kwa basi akiwa na begi.
“Alipofika Nairobi, ilidaiwa begi hilo alilisahau kwenye basi lakini wengine wanasema aliuuza Nairobi na kwenda Afrika Kusini akiwa na begi feki.”
TEVEZ AWASILI AFRIKA KUSINI, AKUMBANA NA MSALA
Habari zaidi zikachimbuka na kudai kwamba, Tevez aliwasili mjini Durban na kukutana na jamaa zake ambapo aliwaambia mzigo  aliusahau kwenye basi.
“Kumbe inasemekana jamaa aliyemuuzia mzigo Nairobi anafahamiana na jamaa wa Sauz na aliwapigia simu kuwaambia kwamba, ameuziwa mzigo na Tevez.
“Kwa hiyo mpaka Tevez anawasili kule, jamaa walikuwa wanajua hana mzigo kwa kuwa aliuuza Nairobi,” kilisema chanzo.
‘Tevez’ akiwa na moja ya wadau wenzake katika biashara anazofanya huko Durban.
ATEKWA, ADHALILISHWA
Ikaendelea kudaiwa kuwa, madai ya Tevez yaliwakera jamaa kwa vile walijua kila kitu, hivyo walimteka na kuanza kumtesa kwa kumvua nguo zote, wakamfunga kamba za manila za rangi ya bluu na kuanza kumtesa kwa adhabu mbalimbali ili kumkomesha.
Inadaiwa katika adhabu hiyo, jamaa hao walimpiga na kitu chenye ncha kali hali iliyosababisha Tevez atokwe na damu na ngozi kuchubuka eneo la mgongoni.
MADAI WAKATI WA UDHALILISHWAJI
Inadaiwa wakati udhalilishaji huo ukiendelea, jamaa hao walikuwa wakisema wanachotaka ni mzigo wao na si kitu kingine.
MARAFIKI, JAMAA WA DAR
Kufuatia kusambaa kwa picha hizo mtandaoni, marafiki na jamaa wa Tevez waliopo Bongo walilazimika kufanya mpango kwa kuwasiliana na watu wa karibu waliopo Durban kumnusuru Tevez kwa kumpeleka hospitali ambako anapata matibabu hadi juzi, Alhamisi.
Risasi Jumamosi: “Kuna habari alikatwa sehemu za siri ni kweli?”
Chanzo: “Si kweli.”
Risasi Jumamosi: “Inasemekana alifanyiwa kitu mbaya cha mambo ya Sodama, ni kweli?”
“Si kweli. Watu wanasema tu. Ila walimtesa sana kwa kweli.”
Bw. Jumanne Hassan ‘Tevez’ akiwa na moja ya jamaa zake sauzi.
RISASI LATINGA DUKANI KWA MKEWE WA SASA
Ili kuzidi kupata habari zaidi, Januari 28, mwaka huu,  usiku Risasi Jumamosi lilikwenda Kinondoni Kwamanyanya, Dar kwenye duka la mke wa sasa wa Tevez ili kumsikia anasema nini kuhusu tukio hilo.
Paparazi wetu hakumkuta mke huyo lakini alibahatika kuongea na msichana aliyekuwa nje ya duka hilo na kumuuliza aliko Tevez.
Msichana: “Tevez yupo safarini Morogoro.”
Risasi Jumamosi: “Mbona hapatikani hewani? Nipe namba zake nyingine.”
Msichana: “Nilizonazo ndiyo hizohizo ulizonazo wewe, ni…(akazitaja).”
Kweli namba hizo ndiyo alizokuwa nazo paparazi wetu.
MAMA MKWE WA TEVEZ
Kesho yake, Risasi Jumamosi lilimsaka kwa simu mama mkwe wa zamani wa Tevez (mama wa Isha)  lengo ni lilelile, kutaka kujua kama naye ana taarifa hizo na anasemaje.
“Ni kweli nimesikia na nimeona picha zake yaani nimesikitika sana kiasi kwamba nikawa siamini kama ni  kweli yeye anaweza kufanyiwa ukatili wa aina hiyo.
“Kikubwa namshukuru Mungu kusikia yupo hai na kwa maana hiyo namuombea zaidi ili arudi katika afya yake,” alisema mama mkwe huyo aitwaye Rukia Juma.
Bw. Jumanne Hassan ‘Tevez’akiwa na mkewe.
MTU WA KARIBU NA TEVEZ
Risasi Jumamosi liliendelea kutafuta undani zaidi wa tukio la Tevez kwa kuongea na watu wake wa karibu waliopo Durban, ndipo likapenyezewa ishu mpya kuwa, baadhi ya ndugu na wafanyabiashara wenzake na Tevez wamechanga na kurudisha mali zilizokuwa zikidaiwa na jamaa hao.
“Nilikuwa Durban muda si mrefu na hapa ndiyo narejea nyumbani (Bongo). Kiukweli tukio la Tevez ndiyo habari ya mjini Sauz, maana jamaa wamemfanyia mbaya kinoma lakini kusema kweli hajakatwa nyeti kama mitandao ya kijamii inavyoandika, wamempiga sana.”
“Kingine ambacho ninajua tayari ameshatolewa kwenye jengo alilokuwa ametekewa na sasa yupo hospitali maalum ambayo siwezi kukutajia, ila huenda hali yake ikawa nzuri kama kweli atakuwa chini ya uangalizi wa madaktari,” alisema jamaa huyo.

Saturday, 24 January 2015

NITAENDELEZA NDOTO ZA KANUMBA......................

Dar es Salaam. Mama wa aliyekuwa nyota wa filamu nchini, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amesema kuwa kupitia Kampuni ya Kanumba The Great Film inakamilisha uanzishaji wa taasisi itakayoitwa, Kanumba Foundation.
Pia, alikanusha uvumi kuwa kampuni ya Kanumba imekufa, akifafanua jambo hilo alisema kampuni hiyo inaendelea na shughuli zake. Alisema kutakuwapo Kanumba Foundation ili kusaidia jamii wakiwamo wasanii katika masuala mbalimbali.
Akizungumza na gazeti hili, Flora alisema uamuzi wa kuanzisha taasisi hiyo ni kuendeleza na kutimiza ndoto alizokuwanazo mtoto wake, marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake.
"Tunaanzisha Kanumba Foundation. Awali haikuwapo, tulivyojaribu kulikuwa na mlolongo mrefu, marehemu Kanumba alikuwa na mipango mingi, huo ukiwemo. Kanumba alisema akisharejea safari yake ya Marekani kuna vitu atafanya, lakini Mungu akampenda zaidi," alisema Flora na kuongeza:
"Mipango yake ilikuwa ni kuanzisha chuo kikubwa cha kufundisha sanaa ya uigizaji kwa kuwachukua waigizaji chipukizi na kuwafunza ili wawe bora." Kuhusu Kampuni ya Kanumba The Great, Mtegoa ambaye pia ni msanii alisema licha ya kusema kuwa kampuni hiyo imekufa, lakini mpaka sasa imeweza kutengeneza filamu kadhaa.
"Kampuni ipo na bado naendelea kuisimamia. Kwa kipindi chote imetengeneza filamu mbili ambazo zilishapelekwa sokoni tangu mwaka jana. Watu wengi wanaamini kwamba ilifungwa, ila ipo na ina watu kama kawaida, japokuwa ukipita nje unaona kama imefungwa," alisema. Flora maarufu kwa jina la Mama Kanumba, alifafanua kwamba kampuni hiyo imekuwa ikifanya kazi za watu wengine, pia inatengeneza filamu zake yenyewe. Alisema kutokana na uwepo wa kampuni hiyo wameweza kufanya mambo mengi, ikiwamo kutimiza ndoto za marehemu Kanumba za kuwa na mfuko wa jamii.
Akizungumzia kipaji chake cha uigizaji, Mama Kanumba alisema hakufanya hivyo baada ya mwanaye kufariki, bali alikuwa akiigiza wakati alipokuwa kigori, hivyo ameamua kuendeleza kipaji chake.
"Nikiwa sekondari niliigiza, wakati huo mtoto wa kike kupelekwa shule mpaka vikao, zamani binti hakuruhusiwa kusoma, ilikuwa ngumu, kwa hiyo unacheza huku ukifikiria kwamba nyumbani wakijua nimeingia huku itakuwa tatizo, baadaye nikaacha," alisema.
Alisema baada ya Kanumba kufariki, aliamua kuendeleza kipaji chake kwa kutumia rasilimali alizoachiwa na mtoto wake.CHANZO:MWANANCHI

Ziko hapa kurasa za mwanzo na mwisho za Magazeti ya leo January 24, 2015

Ziko hapa kurasa za mwanzo na mwisho za Magazeti ya leo January 24, 2015

.
.
Kama kawaida millardayo.com inakupa vichwa vya habari vya magazeti yote ya kila siku. Leo pia kuna headline mpya kwenye magazeti mbalimbali. Chukua muda wako kupitia kila kilichoandikwa kwenye kurasa za mbele za magazeti ya leo.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

SAFISHA JIJI NDANI YA IRINGA NI KIVUMBI NA JASHO









Friday, 2 January 2015

NAAMA YA UTATUZI WA MSONGO WA MAWAZO


Msongo wa mawazo ama stress kwa kiingereza, ni tatizo ambalo kwa bahati mbaya sana limeendelea kuwa kitu cha kawaida sana kwa wanaadamu katika zama tulizo nazo. Katika miaka hii tuliyo nayo, ni sahihi kabisa kusema kuwa, takriban wanaadamu wote walio hai wamekuwa wakikabiliwa na tatizo hili. 
Msongo wa mawazo unaweza kukufanya ushindwe kufanya shughuli zako za kila siku kwa ufanisi. Jambo la kufurahisha ni kuwa msongo wa mawazi unaepukika, leo nimechambua baadhi ya mambo ambayo yanaweza kukuwezesha kuepuka kupata msongo wa mawazo.
Kuna baadhi ya aina za msongo wa kimawazo, ambazo zinaepukika na nyingine ni ngumu kuziepuka ila unapaswa kujua jinsi ya kukabiliana na shinikizo la msongo wa mawazo pale linapokukabili.



MAMBO 5 YANAYOMKABILI MWANADAMU
1.         Kutojiamini
2.         Kuogopa mabadiliko
3.         Kukosa mpango wa maisha
4.         Kupuuza mahitaji muhimu ya binadamu ya:-
·        Mwili
·        Roho
·        Akili
5.         Kuishi kwa kukata tamaa
·        Kuumwa kichwa
·        Kukosa nguvu za mwili (me+ke)
·        Matatizo makubwa ya familia
·        Kukosa upendo
·        Hasira za mara kwa mara
Waathirika wa msongo na kusambaratika
Kila lika inakubwa na tatizo hili la Msongo wa Mawazo lakini nitajaribu kufafanua watu tofauti ambao hukubwa sana na tatizo hili 
  1. Wazazi – sababu kubwa ni uchumi wa familia: Watoto wanaouwezo wa kukuhoji kwa nini wewe ni masikini, kushindwa kupeleka watoto shule, kushidwa kutatua matatizo hata madogo madogo ya Familia hapo lazima upate Msongo wa Mawazo
  1. Waajiri/Waajiriwa – Watu hawa hupatwa na tatizo hili na huwapelekea kuhamisha mambo ya kazini wanapeleka nyumbani na ya nyumbani wanayapeleka kazini. Mfano mtu amegobwana na wafanyakazi wenzake kwa makosa yake mwenyewe akarudi nyumbani na kuendelea na hali ile na kusababisha matatizo nyumbani kwake. 
  1. Vijana na wanafunzi – Vijana wengi hukubwa na tatizo hili hasa katika maswala ya kiuchumi na kwa wanafunzi wengi kuingia katika Mapenzi wakiwa bado wapo shule huwasababishia msongo wa mawazo kwani tayari anakua kajipa majukum mengine. Mfano jana amegombana na mpenzi wake leo akienda shule hawezi kusoma vizuri atakua mtu mwenye mawazo kutokana na kilichomkuta siku iliyopita. 
  1. Wanandoa – Wanandoa wengi  wana msongo na kukosa faraja.  Wanaamini nje kuna faraja zaidi (nyumba ndogo)
Wakristo wanaweza kusoma vitabu hivi ili kupata maelezo (luka 24),  (matendo 11:28-30),  (yohana 18:14-27)
Mizigo inayochosha
Watu wengi hupata Msongo wa mawazo kutokana na wao kutaka kujitwika mizingo wasiyo weza kuibeba nitataja baadhi
  • Kushindana na jirani
  • Kufanya mambo nje ya uwezo wako
  • Kupata bp, tumbo, kichwa, bila sababu
  • Kuwa na idadi kubwa ya watoto ambao huwezi kuwalea 
Msongo wa mawazo hujitambulisha sana kwa mwili, akili na roho
Akili – ikisikia juu ya jambo gumu inashindwa kulipokea.  Inapeleka kwa tumbo, tumbo linashindwa linaamua kutoa unaharisha ndipo mtu hupata vidonda vya tumbo na tumbo kupata maumivu makali.
Utakabiliana vipi na msongo 
1.      Jifunze Kukubali Changamoto, Katika maisha huwa tunakutana na mambo ambayo hatukutaka kukutana nayo na pia tunashindwa kupata yale tuliyoyataka, karibu kila mtu huwa anapitia hali hii kwa namna moja au nyingine. Jifunze kukabili changamoto na sio kusikitika kwa nini mambo hayajawa kama ulivyotaka na kubaki ukisononeka. Jaribu kukubali mambo kwa busara zaidi, na utulivu huku ukitafakari nini cha kufanya ili kulipata lile ulilo kusudia. Changamoto iwe ni chachu ya wewe kuzidi kukazana na kujaribu zaidi.
2.      Jifunze kusema “hapana” hii ni katika mambo yako binafsi au kazi yako, unaitumiaje hii hapana? Unajua maofisini kuna swala la kupeana vikazi visivyoeleweka hata vimetokea wapi, yaani hujamaliza hili unaletea jingine hata kama sio kazi yako… sasa jifunze kukataa hizi kazi zisizo za kwako ili mradi tu mfurahishe tu. hivyo hivyo vitu vidogo vidogo ndivyo vinavyokuletea msongo wa mawazo.
3.      Jiepushe na watu ambao mara nyingi wanakusababishia Stress, Kunawakati huwa tunakua na kampani ya watu ambao kabisa unajua hawa wananisababishia msongo wa mawazo Mfano:- Upo katika mahusiano na mtu ambaye wewe unampenda lakini haonyeshi kujali upendo wako utajitahidi kupiga simu kutuma sms umweke karibu lakini yeye hajali, si busara ukaendelea kuumiza kichwa kwajili yake ni bora uachane nae mapema sana. Pia hata marafi wapo maadhi ya marafiki wanaweza wakakusababishia msongo wa mawazo kutokana na wanayokufanyia kwa mfano rafiki anayekupenda wakati wa raha tu na anakukimbia ukiwa na shida huyo si mwema kwako atakufanya uwe na Msongo wa mawazo. Tembelea watu wanaokufanya ufurahi na jifunze kucheka na kufurahi. Epuka kakaa na watu ambao kwako ni kikwazo.
4.      Panga kazi zako kwa ratiba usivuruge ratiba kwa vitu visivyo vya lazima ili kumfurahisha mtu mwingine. Mfano:- Umeapanga ratiba yako ya siku nzima anakuja rafiki ako akakuomba umsindikize sehemu ambayo haina umuhimu wala ulazima ukaenda ukapoteza mda mwingi huko, ukirudi tayari unakua umejipa Msongo kwani ratiba yako itakua imevurugika na utajilazimisha hata kuchelewa kulala ili tu umalize uliyo panga. Hiyo inaweza kukupa msongo kwani utakua ukifanya vitu kwa manung'uniko. katika ratiba yako tenganisha ratiba hiyo kwa vitu vya lazima kufanya na vitu vya kawaida ambavyo hata usipovifanya hazitakuharibia ratiba yako. kujua kipi cha lazima ni moja ya njia kubwa ya kupunguza msongo wa mawazo.
5.      Epuka Hasira za haraka, kuna mambo yanayohusu dini,siasa au maisha yako binafsi huwa yanakupa msongo wa mawazo basi jitahidi kuepukana nayo katika mazungumzo yako ya kila siku kwasababu yatakupa hasira na kukufanya ukasirike na hili hupelekea kuwa na msongo wa mawazo, ukiingia sehemu ukakuta watu wanaongelea swala hilo epuka kukaa nao karibu ili usiweze kuchangia na kujikuta unaingia katika mgogoro wa nafsi
6.      Fanya kazi yako ya halali kwa juhudi na maarifa 
7.      Uwe na malengo ya maisha.  Fanya jambo moja kwa wakati wake. Mfano jiulize unataka kufanya nini kwa wakati gani na ili uwe nani?
8.      Wakati unapokula usiwe unaonngea au kukumbuka shida zako.  Pia kula polepole na kwa raha zako.  Ikiwezekana wakati wa kula zima simu. kwasababu tunajua hatuwezi kuishi bila kula tujaribu kuheshimu mda wa kula kwani kunawakati hata simu zetu tunaweza kupokea kitu kikatufanya tuvuruge hata ratiba ya kula na kupoteza hamu na kusababisha Msongo wa mawazo.
9.      Fanya mazoezi kila siku, mara tano angalau kwa juma.  Tofautisha kazi na mazoezi.
10.  Zingatia Muda wa kula
11.  Sikiliza muziki wa injili, bongo flava, lugha yenu ya asili, muziki ni dawa, nchi 2 za afrika ziliponya kwa muziki      (Afrika kusini naKongo)
12.  Tafuta sababu zinazokuletea msongo wa mawazo, zitambue na kuzifahamu ili uziepuke.
13.  Usiweke Jambo Linalokusumbua Moyoni, Pale unapokutana na jambo ambalo umeshindwa kulitatua ni vyema ukamshirikisha mzazi wako au mlezi, rafiki wa karibu, mume au hata mshauri. Jifunze kutokuweka mambo yanayokuumiza moyoni maana katika hali hiyo ni rahisi sana kupata msongo wa mawazo. Uwe na tabia ya kupeleka wasiwasi na hofu zako zote mbele za Mungu kwa maombi na pia kuongea na mtu ambaye unajua atakuwa msaada kwako.
  NB: Msongo wa Mawazo si Ugonjwa na unaepukika ukijitahidi kufuata mambo hayo hautaweza kuwa na Msongo wa Mawazo. Jiamini kwa kila unachokofanya. Fikiri kabla ya kutenda, Kipende kila unachokifanya. Hapo utakua umeepuka msongo wa mawazo. Maamuzi yako ni bora kuliko yakuambiwa. Akili ya Kuambiwa Changanya na yako.