Habari ya kusikitisha kwa mashabiki wa
shindano la Big Brother Africa, Jumba linalotumika kufanyia shindano
hilo lililoko Johannesburg, Afrika Kusini limeteketea kwa moto September
2.
Kutokana na tukio hilo, M-Net na Endemol
South Africa wameeleza kuwa wamelazimika kubadili ratiba ya shindano
hilo msimu huu lililopewa jina la ‘Big Brother Hotshots’ na halitaanza Jumapili, September 7 kama ilivyotarajiwa hapo awali.
Chanzo cha moto huo hadi sasa hakijajulikana na makampuni hayo yameeleza kuwa uchunguzi wa kina utaanza mara moja.
Makampuni hayo yamepata changamoto kubwa
kutokana na tatizo hilo kwa kuwa vifaa vinavyotumika kufanyia
uzalishaji ni vya aghali na adimu sana hivyo wameeleza kuwa ni vigumu
kupata vifaa mbadala hivi punde.
“Kila juhudi itafanywa kutafuta ufumbuzi
wa tatizo haraka iwezekanavyo kuhakikisha kuwa reality show hii kubwa
zaidi Afrika inaendelea.” Wameeleza katika tamko lao.
Hakuna mtu aliyejuruhiwa katika tukio hilo.
Haya ni maelezo waliyoweka kwenye website yao:
M-Net
and Endemol SA advise that due to a devastating fire at the Big Brother
house on 2 September 2014, Big Brother Hotshots will not launch this
Sunday (7 September) as schedule. The cause of the fire at this stage is
unknown and investigations will commence as soon as it is safe to do
so.
At
this stage M-Net and Endemol are urgently looking for an alternative
Big Brother house in which to film the production, however as this
production has highly technical infrastructure, camera and edit
requirements an alternative is not immediately available. Every effort
will be made to find a solution as quickly as possible to ensure that
Africa’s biggest reality show will continue.
No comments:
Post a Comment