Familia
moja ya Uturuki inawapasua kichwa wanasayansi, kutokana na wanandugu
watano kutokuwa na uwezo wa kutembea kama binadamu, na badala yake
wanatembea mithili ya wanyama, wakitumia miguu na mikono.
Hata hivyo, katika
uchunguzi wao wa awali, wanasayansi hao wameeleza kuwa, hali
iliyowakumba wanandugu hao haina uhusiano na mabadiliko ya binadamu,
kwamba wanaanza kurudi katika zama za mwanzo ambako inaelezwa walitembea
kwa miguu minne, wengine wakisema walianza kuwa nyani.
Ndugu hao watano ambao ni
kaka na madada, wakiwa na umri wa miaka 16 hadi 34 kutoka kijiji cha
Jimbo la Hatay, kusini mwa Uturuki, walianza kufuatiliwa na wanasayansi
mwaka 2005 baada ya kugundulika na watu kutoka nje ya kijiji chao.
Wanatembea kwa mtindo wa kutambaa kama dubu kwa mikono na wanaweza kusimama tu kwa muda mfupi, kwa magoti yao.
Utafiti
wa hivi karibuni ulifanywa na wanasayansi, Shapiro, Whitney Cole, Scott
Robinson na Karen Adolph, wote wa Chuo Kikuu cha New York, Jessica
Young wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Northeast Ohio na David Raichlen, wa
Chuo Kikuu cha Arizona.
“Lakini hawa hawana
uhusiano na mgeuko wa binadamu kwamba baada ya kupitia hatua kadhaa za
mabadiliko, sasa wanarudi katika hatua za awali, hilo halipo,” mmoja wa
wanasayansi hao amenukuliwa akisema.
Nadharia za awali zilidai
familia ya Ulas ilikuwa ikitembea kama nyani, na kupendekeza kuwa huenda
ni hatua ya kurudi nyuma kwa mabadiliko ya binadamu.
Lakini sasa, wanasayansi wa
Kimarekani wamethibitisha kwa kusema wanandugu hao wanakabiliwa na
kasoro isiyoonekana na hutokea mara chache.
Katika ripoti
iliyochapishwa na PLOS One, watafiti walisema familia hiyo wanatembea
kwa namna tofauti kama nyani, ambao wakitembea huweka mikono upande
mmoja na miguu upande mwingine wakijirudiarudia.
Walidai kutembea kwa wanandugu hao ni matokeo ya hali ya kurithi ambayo husababisha uwiano wa akili kutatizika.
“Nilikuwa na hamu ya kuweka
rekodi sawa, kwa kuwa haya madai ya asili na sababu ya kutembea kama
mnyama wa miguu minne imechapishwa mara kwa mara, bila kuwepo uchambuzi
wa kwa nini wanatembea hivyo, na watafiti ambao si wataalamu wa namna
mamalia wa hali ya juu wanavyotembea," Mtafiti Kiongozi Liza Shapiro wa
Chuo Kikuu cha Texas alilieleza gazeti la The Washington Post.
“Tumeonesha wanyama wa
miguu minne wanavyofanana na mtu mzima mwenye afya njema ambaye
ameambiwa atembee kwa miguu minne wakati wa kufanya majaribio.
Mwaka 2005, watafiti wa
Uingereza walikubali katika utafiti tofauti kuwa utembeaji wa ndugu hao
unatofautiana na baadhi ya mamalia wengine, ikizingatiwa wenyewe hubeba
uzito wao wote kwenye viganja vya mkono na kifundo cha mkono na sio
kiungio.
Hata hivyo, Mtaalamu wa
Bayolojia wa Uturuki, Uner Tan awali alidai wanandugu hao, ambao pia
wanaonekana kuwa wameathirika kwenye ubongo wanakabiliwa na hali
inayoitwa Uner Tan Syndrome.
Alisema watu wanaokabiliwa
na hali hiyo hutembea kwa miguu minne na mara nyingine huzungumza kama
wanyama na huwa na mtindio wa ubongo.
“Ghafla nimegundua
wanatembea kwa mtindo kama nyani kama walivyokuwa wahenga wetu… nilikuwa
wa kwanza kupendekeza kuwa kuna uwezekano wa hali ya binadamu kugeuka
na kurudi enzi za zamani za ubinadamu,” alisema.
Wandugu hao ambao wazazi
wao wanatembea kawaida, mara ya kwanza walirushwa mwaka 2006 kwenye
dokumentari ya BBC2, dokumentari hiyo ikiitwa The Family That Walks On
All Fours.
Wakati mabinti wawili na
mtoto mmoja wa kiume wamekuwa wakitembelea mikono miwili na miguu
miwili, mtoto mwingine wa kiume na kike mara nyingine huweza kutembea
wakiwa wamenyooka sawa, ingawa si kwa muda mrefu.
Profesa Nicholas Humphrey,
ambaye aliitembelea familia hiyo mara mbili wakati wa dokumentari hiyo,
alisema, “inashangaza kama mfano wa kitu cha ajabu cha maendeleo ya
binadamu. Lakini kinachovutia ni jinsia wanavyoweza kuishi katika
ulimwengu wa kisasa.”
Alisema alifikiri familia
hiyo imerudi katika silika ya mfumo wa tabia iliyojikita ndani sana
kwenye ubongo, lakini aliachwa wakati wa mageuko.
“Sidhani kama walitakiwa
kuwa wanyama wanaotembelea miguu minne kutokana na jeni zao, lakini
mfumo wa utengenezaji jeni zao zinawaruhusu kuwa hivyo,” alisema.
Wanandugu hao watano ambao
wana kaka na dada zao wengine 14 ambao hawajaathirika na hali hiyo,
hutumia muda mwingi kukaa nje ya nyumba yao ya familia iliyoko
kijijini.
Hata hivyo, mmoja wao hutembea kijijini, kuchanganyika na kuzungumza na watu.
No comments:
Post a Comment