Mwonekano kwa nje kumbe ndani kuna siri kubwa imejifichaHabari gani wana ndugu ni kitambo kidogo tangu nilipofika katika eneo la nanenane jijini mbeya wakati huo kulikuwa na watu wengi sana hadi nikashanga kuna nini nikaambiwa kuna maonyesho ya nanenane nikajaribu kuingia nikapata tabu mlangoni kutokana na kundi kubwa wa wananchi waliojitokeza kwenda kuangalia maonyesho ya nanenane nikajitahidi kubananana nikalipa kiingilio japo ningeweza kuingia kwa kutumia kitambulisho cha kazi nilitaka tu kujua nini kinajili mlangoni wakati wa kuingia.Nikatoa shilingi mia tano wakubwa wa mlango wakaniruhusu kuingia.Ndani ya uwanja kulikuwa kumependeza na mapambo mbalimbali nikawa nashangaa mabanda mbalimbali hamadi nikakutana ofisi moja iliyofahamika kwa jina la TASO nikaambiwa ndio wahusika wa uwanja huo na ndio wasimamizi wa mazingira yote nikafurahi nikawasifia walivyopendezesha mazingira nikamaliza nikageuka nikarudi nitokako. Leo nimeamkaa asubuhi mapema nikawaza niende wapi nikaoshe macho kama waswahili wanavyosema niakaona mahali pazuri ni nanenane nikajipanga nikaondoka kuelekea viwanja kufika mlangoni sikukuta walinzi mlangoni nikashangaa nikajiuliza leo vipi mbona hamna watu kama wale wala hamna kiingilio basi kama ilivyo kawaida ya kazi zetu nikajaribu kujua nini kinaendelea nikamwona mama nikamsalimia nikamuuliza swali. HABARITALK:Mimi nimekuja matembezi mama ila nilichokiona kimenishangaza awamu iliyopita nilikuja hapa kulikuwa na watu wengi mlangoni wakiingia na kutoka huku wengine wakikusanya kiingilio leo wameenda wapi? MAMA:mwanangu hivi ndivyo inavyokuwaga baada ya kumalizika kwa maonyesho ya nanenane mlangoni huwa tunaingia bila kiingilia pia hakunaga biashara zinazoendelea humu ndani hivyo mwanangu ingia bila wasiwasi. HABARITALK:Nikajikongoja kuingia viwanjani kama ilivyokuwa shabaa yangu toka nitokako hamadi nilichokiona sikuamini nikajiuliza inamaana jalala limeamia huku nikizidi kushangaa nikapitiwa na nzi waliotoka kwenye uchafu nikaondoka kwa haraka nikizani nimeshinda wale nzi kufika mbele nikakumbana na makopo nikawazua mawazo nikakumbuka kuna kampuni niliikuta eneo hilo inamaana waliondoka bila kufanya usafi wa mazingira nikabaki bila jibu nikiangalia ile ofisi ambayo niliambiwa inashughulika na mazingira ya nanenane imefungwa nikakosa nikakosa wakumuuliza hilo hilo. Kwa mwonekano hule nikajiuliza je ingekuwa maonesho yanadumu kwa mwezi mzima? nadhani ningekuja na ndege ndogo kwasababu nafasi ya kupita ingekosekana. | |
|
No comments:
Post a Comment