Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi
Mwanamke mmoja wa Kijiji cha Mtitu
wilayani Kilolo mkoani Iringa, Grace Lubava (33), amemuua mtoto wake kwa
sumu na kisha naye kujiua kwa njia hiyohiyo na baadaye mumewe, George
King’ung’e (45), kujinyonga kwa kamba kutokana na vifo hivyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa,
Ramadhani Mungi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi na kwamba
mama huyo alifariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu katika Zahanati
ya Kilolo.
“Kifo cha mama na mtoto kilitokea baada
ya mumewe kumzuia mkewe kwenda kumwona baba yake ambaye alikuwa
amelazwa katika Hospitali ya Tosamaganga,” alisema Mungi.
Alisema kuwa mume alimzuia mke huyo
kwenda hospitali kwa madai kuwa alikuwa anakwenda kwenye mambo yake
binafsi jambo ambalo lilimkera mwanamke huyo kiasi cha kufikia uamuzi
huo.
Kamanda Mungi alisema baada ya King’ung’e kubaini vifo hivyo na msingi wake, aliamua kwenda porini na kujinyonga.

via>>Mwananchi
No comments:
Post a Comment