Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Taasisi
moja kutoka Uingereza inayohusika na kampeni dhidi ya upangaji matokeo
kwenye mpira wa miguu (match fixing) itafanya uwasilishaji
(presentation) juu ya suala hilo kwa waandishi wa habari za michezo
nchini.
Uwasilishaji
huo utafanyika kesho (Julai 5 mwaka huu) saa 11 jioni kwenye hoteli ya
Accomondia iliyopo Barabara Nkrumah jijini Dar es Salaam.
Wataalamu
hao wa kupiga vita upangaji matokeo ambao pia wataelezea jinsi matokeo
yanavyopangwa, jana (Julai 3 mwaka huu) walifanya uwasilishaji wao kwa
wachezaji na benchi la ufundi la timu ya Taifa ya vijana wenye umri
chini ya miaka 17 (Serengeti Boys).
Taasisi
hiyo yenye kibali kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) katika utoaji elimu ya kubaini upangaji matokeo, vilevile inatoa
elimu juu ya athari zinazopatikana kutokana na upangaji matokeo.
MAFUNZO YA TIKETI ZA ELEKTRONIKI MBEYA
Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeendesha mafunzo ya matumizi ya
tiketi za elektroniki kwa wadau wa mpira wa miguu mkoani Mbeya.
Mafunzo
hayo yamefanyika jana na leo (Julai 4 mwaka huu) kwenye Uwanja wa
Sokoine, na kushirikisha wasimamizi wa mechi, viongozi wa Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA) na makatibu na maofisa habari wa
klabu za Tanzania Prisons na Mbeya City.
Wengine
walioshiriki mafunzo hayo ni Meneja wa Uwanja wa Sokoine na msaidizi
wake, wasimamizi wa milangoni (stewards) na waandishi wa habari wa
mkoani Mbeya.
Mafunzo
hayo yanahitimishwa kesho (Julai 5 mwaka huu) kwa mechi kati ya Tanzania
Prisons na Mbeya City itakayochezwa Uwanja wa Sokoine kuanzia saa 10
kamili jioni. Kiingilio ni sh. 3,000, na tiketi zilianza kuuzwa Julai
Mosi mwaka huu kupitia M-Pesa, CRDB Simbanking na maduka ya Fahari
Huduma.
(A.I).
No comments:
Post a Comment