Katibu
Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amemtaka Rais Jakaya Kikwete
kujitokeza hadharani kutafuta suluhu ya kupata mwafaka wa mchakato wa
Katiba Mpya kwa kuwa hakuna mamlaka nyingine zaidi inayoweza kuunusuru.
Pia,
amewatahadharisha viongozi wa dini kuwa makini na kauli zao wanazozitoa
za kuwataka wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kurejea
bungeni Agosti 5.
Dk Slaa
aliyasema hayo juzi katika mahojiano maalumu na gazeti hili, makao makuu
ya Chadema Mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
"Mwenye
rungu la kuweza kutengua kitendawili hiki ili turudi bungeni ni Rais
(Kikwete) mwenyewe, hakuna mwingine,"alisema Dk Slaa.(P.T)
"Tatizo
aliyesaini waraka uliowasilishwa na Warioba ni Rais mwenyewe, alisaini
ukurasa wa kwanza na wa mwisho, kwa taarifa rasmi za kina Warioba, Rais
alishirikishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba hatua kwa hatua na kwa
kila hatua alisema sawa mchakato uendelee,"alisema Dk Slaa.
Alikumbusha
kuwa wakati akipokea Rasimu ya Pili ya Katiba, Rais Kikwete alisema:
"Mtapata rasimu, ijadilini na itapitishwa na Bunge. Kwa mwanasheria
yeyote, lugha kujadiliwa na kupitishwa haitoi ruhusa ya kubadilishwa,
inatoa ruhusa kuboreshwa. Ndiyo utaratibu wa sheria zote duniani."
"Sasa
anapofika mahali anayeleta wazo ni Rais, lakini kwa bahati mbaya
anayekwenda kupindua pia ni Rais na amekwenda mbali zaidi kiasi cha
kusema kwamba kama Serikali tatu ile ile ambayo yeye ameisaini
itapatikana, jeshi litapindua nchi.
"Anayezungumza
ni Rais, hakuna mamlaka nyingine inayoweza kutengua kitendawili hiki.
Wanaweza kuja maaskofu, ...masheikh, asasi mbalimbali... hatimaye hakuna
anayeweza kutengua kwa sababu aliyeufanya ni mwenye mamlaka ya
juu,"alisema.
Dk Slaa
aliyewahi kuwa Mbunge wa Karatu kwa vipindi tofauti alitaja mambo matano
anayopaswa kuyafanya Rais Kikwete ili wajunge wa Bunge Maalumu la
Katiba wanaounda Ukawa waweze kurejea bungeni.Aliainisha la kwanza ni
majadiliano kuwa na misingi iliyo wazi akisema Ukawa haipo tayari
kufanya mambo na kuishia kupewa pipi na kwamba Katiba Mpya lazima
ipatikane kwa maridhiano.
Alitaja
jambo la pili kuwa ni lazima wao , Ukawa wahakikishiwe kuwa kanuni
hazichezewi baada ya kupitishwa na siyo kama ilivyofanya CCM, baada ya
Ukawa kutoka bungeni akisema hatua hiyo ni sawa na uhuni. Lingine ni
kuhakikishiwa kitakachojadiliwa ni rasimu iliyowasilishwa na Tume ya
Marekebisho ya Katiba si kingine.
Huku
akitoa mfano wa hotuba ya Mwalimu Julius Nyerere ya Juni, 1965 akisema
ndiyo iliyowajibu CCM kuhusu msimamo wa Serikali mbili waliodai ni
kuenzi aliyoanzisha Nyerere, Dk Slaa alisema;
"Itakuwa
upumbavu kama watu wataamini kwamba katiba haibadiliki, hata kama
imedhihirika kuwa haitoshelezi tena haja ya wananchi kwa wakati ule."
No comments:
Post a Comment