Kama ulivyosikia katika kile kilichotokea siku ya jumatano (June 2)
katika kipindi cha xxl kupigana kwa watangazaji watatu wa kipindi hicho
Fetty, B12 na Adam Mchomvu, ndani ya dakika chache sauti ikasambaa kwa
mamilioni ya watanzania, kiufupi zoezi hilo halikuwa na uhalisia wowote
kwa watangazaji hao,
bali ni katika kuwaelimisha watanzania kupaza sauti pale ambapo kitu
kisichokizuri katika jamii inayotuzunguka ni muhimu sana kupaza sauti
haraka.
kama mtu mmoja unauwezo wa kupaza sauti na kuiweka nchi yetu katika
Amani, basi kwa kila kinachohatarisha amani kinachototokea , mtaani
kwetu, iwe ni kwa rafiki ndugu jamaa ama mtanzania mwezako, basi paza
sauti kwa uzito kama huo ulioonekana siku ya juma tano, ukimya hausaidii
No comments:
Post a Comment