Na Hudugu Ng'amilo
Mlipuko wa bomu katika eneo ambalo wapenzi wa mpira Nigeria walikuwa wanaangalia mechi za kombe la dunia umeuwa watu wapatao 21.
Mashahidi
na maafisa wa afya walisema Jumatano kwamba watu wapatao 20 wengine
walijeruhiwa katika mlipuko huo ambao ulitokea Jumanne katika mji wa
kaskazini mashariki wa Damaturu.
Makundi
ya watu wengi walikuwa wamekusanyika katika kituo cha eneo la nje cha
kuangalia mpira wa kombe la dunia kati ya Brazil na Mexico kwenye
televisheni kubwa.
Mashahidi wanasema bomu ambalo inaelekea lilifichwa katika bajaji lilipuka muda mfupi baada ya mechi hiyo kuanza .
Mashahidi wanasema bomu ambalo inaelekea lilifichwa katika bajaji lilipuka muda mfupi baada ya mechi hiyo kuanza .
Hakukuwa
na madai ya mara moja ya kuhusika .Damaturu ni mji mkuu wa jimbo la Yobe
na moja ya mikoa ya kaskazini ambayo iko chini ya hali ya hatari,
kufuataia mfululizo wa mashambulizi mabaya yanayohusiana na kundi la
wanamgambo wa kiislam la Boko Haram.
CHANZO SAUTI YA AMERIKA
CHANZO SAUTI YA AMERIKA
No comments:
Post a Comment