Serikali
ya Tanzania imesema ugonjwa wa dengue umeonekana kuanza
kupungua
katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania kutokana na wananchi
kuchukua tahadhari kuhusu ugonjwa huo.
Akiongea
na mtandao wetu Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii,
Nsachris Mwamwaja amesema mpaka siku ya jana wagonjwa wawili
pekee
waliokuwa wamelazwa na mmoja kuthibitika kuugua ugonjwa huo.
Aidha,
Mwamwaja amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kwa
kusafisha mazingira ili kutokomeza kabisa ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment