STARS KUTIMKIA BOTSWANA
WACHEZAJI
26 wa timu ya taifa ya Tanzania-Taifa Stars wanatarajiwa kuingia
kambini Jumatatu ijayo kwa ajili ya safari ya Gaborone, Botswana. Kwa
mujibu wa Kocha Msaidizi wa Stars Salum Mayanga, amedai kuwa wachezaji
hao wanatakiwa kuripoti katika hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam
kujiandaa kwa safari hiyo inayotarajiwa kuwa Juni 24 mwaka huu. Wachezaji
hao ni wanaotakiwa kuripoti kambini ni Deogratias Munishi, Aishi
Manula, Benedictor Tinoko, Kelvin Yondani, Said Moradi, Nadir Haroub,
Joram Nason, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Edward Charles, Aggrey
Morris na Pato Ngonyani. Wengine
ni Frank Domayo, Amri Kiemba, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Said Juma,
Haruna Chanongo, Himid Mao, John Bocco, Simon Msuva, Kelvin Friday,
Ramadhan Singano, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa na Mwegane Yeya.
No comments:
Post a Comment