Wednesday, 18 June 2014

NSSF YAHITIMISHA ZOEZI LA UPIMAJI AFYA KANDA YA ZIWA



Published in Jamii
1_ad145.jpg
Banda la NSSF.
2_41042.jpg
Meza kuu wakifurahi wakati wimbo wa mkoa wa Kagera ukiimbwa.
Toka Kushoto, Dr.Ruta Thomas, Mganga Mkuu mkoa wa Kagera, Bw.Adoh Mapunda
,Mkurugenzi wilaya ya Bukoba, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, Mkuu wa mkoa wa
Kagera, Bw.Leornard Faustine Kachebonaho, Mwenyekiti wa Chama cha msalaba
mwekundu , Kagera . Dr.Ali Mtulia Meneja wa Mafao ya Matibabu –SHIB na Mratibu
wa Chama cha Msalaba mwekundu mkoa wa Kagera, Bi.Robi Wambura.
3_24ae4.jpg
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Masawe (katika), akikagua mabanda wakati wa zoezi la kupima afya bure kwa wakazi wa Mkoa wa Kagera.(A.I).
1_e420e.jpg
Ndugu zangu,
Septemba kumi, 2006 nilikutana na ndugu na kaka yangu Muhidin Issa Michuzi pale Food World Restaurant, Maktaba Street, Dar es Salaam.
Kaka Michuzi na mimi tulizungumza kwa kirefu juu ya masuala ya kublogu. Wakati huo blogu ilikuwa ni kitu kipya sana hapa nyumbani. Na hakika hapa nyumbani alianza Muhidin Michuzi kuwa na blogu ya habari na picha. Mimi ni kati ya wachache tuliofuatia kwa hapa nyumbani.
Kwenye mazungumzo yetu pale Food World, nilimwambia Michuzi niwe nachangia kwenye Michuzi blog kwa kumtumia picha na habari kutoka vijijini, ni kwa vile nimekuwa nikiishi Iringa na kufanya kazi za vijijini tangu 2004.
Michuzi aliniangalia na kusema; " Maggid, mimi nafikiri nawe uwe na blogu yako mwenyewe yenye kutoa zaidi taswira za maisha ya vijijini".
Michuzi na mimi tumefahamiana tangu miaka ya 80 mwishoni. Kilichotuunganisha na Michuzi tangu wakati huo ni picha, kama Michuzi, nami pia nimekuwa na mapenzi makubwa na picha tangu utotoni.
Michuzi aliufahamu uwezo wangu, na ndio maana akaona bora niongeze nguvu kwa kuanzisha blogu yangu mwenyewe.
Na ndipo hapo ' Mjengwablog' kama wazo l a ' blogu kama kijiji' likazaliwa, na Jumanne ya Septemba 19, 2006, ndipo picha ya kwanza na maelezo iliingizwa kwenye Mjengwablog. Naam, nimeratibu shughuli za ' Mjengwablog' kama ' Kijiji' tangu 2006. Ndio sababu ya kuitwa ' Mwenyekiti'. Ina maana ya ' Mwenyekiti' wa Kijiji cha ' Mjengwablog'!
Na profile picture yangu ya kwanza kwenye Mjengwablog ilikuwa nimetinga shati hilo hilo nililovaa nikiwa na Michuzi ( Pichani).
Hakika, nyingine ni kumbukumbu muhimu sana katika kuandika historia ya chimbuko la blogu Tanzania. Kuna umuhimu wa kuweka kumbukumbu hizi katika maandishi ili yasaidie vizazi vijavyo.
Maggid Mjengwa,
0754 678 252
1_0d189.jpg

Kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka 1990, bila kutarijiwa, Cameroon ikawa nchi ya kwanza ya kiafrika kuingia hatua ya robo fainali.
Leo inacheza na Croatia. Itakuwa cameroon nyingine tofauti na tuliyoiona ilipocheza na Mexico na kufungwa moja bila.
Tumewaona mexico wakiwatoa jasho brazil jana. Bila shaka, mexico ilikuwa timu ngumu sana kwa cameroon kufungua dimba nao.
Baada ya mechhi yao ya kwanza cameroon watakuwa wamejipanga upya. Ndio maana ya kusema, leo tutaiona cameroon nyingine ksbisa. Na hata ikitoka sare leo, basi, kwenye mechi yao na brazil tunaweza kushuhudia kisa cha mende kuangusha kabati...
Na tusubiri tuone.
Maggid Mjengwa.

Kipa wa Mexico ainyima Brazil ushindi

Published in Michezo
1_4b94c.jpg
Ochoa aliokoa mikwaju tele ya Brazil
Mexico walipata pointi moja dhidi ya Brazili, katika mechi ya kundi A iliyomalizika bila ya timu yeyote kutisa wavu wa mwenziye katika uwanja wa Estadio Castelao huko Fortaleza.
Brazil walishindwa kufunga bao na ilikua sio kama timu ile iliyoishinda Croatia mabao 3-1 matika mechi ya ufunguzi .

No comments:

Post a Comment