Na Hudugu Ng'amilo
Wakili
mmoja nchini Misri ameiambia BBC kwamba mahakama imezingatia hukumu ya
kifo cha wanachama 182 wa kundi la Muslim Brotherhood .
Washtakiwa
hao ni miongoni mwa watu 700 wanaoshtakiwa kwa kukishambulia kituo
kimoja cha polisi katika eneo la Minya mwaka uliopita.
iIongozi wa kundi hilo Mohammed Badie ni miongoni mwa wale waliohukumiwa kifo.
Washtakiwa wengine watano walipewa hukumu nyengeine ya kati ya miaka 15 na 55 huku wengine wakiachiliwa huru.
Hukumu iliotolewa mnamo mwezi Aprili ambapo jaji aliwapatia hukumu ya kifo washtakiwa wote ilizua pingamizi kutoka kwa makundi ya kupigania haki za kibinaadamu.
CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment