Muangalizi:
Jose Mourinho (kulia) amekuwa akiwatembelea watoto wanaosumbuliwa na
njaa pamoja na wagongwa wa UKIMWI nchini Ivory Coast akiwa kama balozi
wa Mpango wa Chakula Duniani. BOSI wa Chelsea, Jose Mourinho anadhani
chama cha soka nchini England, FA kingetoa faini za mpira wa miguu
anazolipa kwa kuwasaida watu wenye shida kama sehemu ya upendo.
Badala ya
kuangalia kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil, Mourinho
amewatembelea watoto wanaosumbuliwa na njaa na wagonjwa wenye virusi vya
UKIMWI nchini Ivory Coast akiwa kama balozi wa umoja wa mataifa wa
Mpango wa Chakula Dunia. Mreno huyo alisema anataka kuona mpira unafanya
kazi zaidi kusaidia mpango wa Chakula Duniani (WFP) na akapendekeza FA
itumie faini anazotozwa kuwasaidia watu wenye shida.(P.T)
"Nitalipa (faini) kwa tabasamu kama hela zinakwenda sehemu sahihi,"
Aliwaambia ITV wakati wa ziara yake. 'Huo ni uzoefu, kwakweli nimepata
uzoefu,". Alisema kocha huyo mwenye miaka 51 huku akishindwa kuzuia
machozi yaliyokuwa yanamlenga. "Na aina ya uzoefu ambapo najisikia
kidogo". "Ni machungu, lakini wakati fulani huwa ni nzuri kwa roho".
Mpango
wa Chakula Dunia ni shirika kubwa la kimataifa linaloshughulikia balaa
la njaa duniani kote. Mwezi mei, Mourinho alitozwa faini na FA ya Euro
10,000 kwa maneno yake aliyosema juu ya viongozi wa mechi baada ya
Chelsea kufungwa mabao 2-1 na Sunderland na kujikuta akivunja rekodi ya
kucheza mechi 77 bila kufungwa nyumbani.
Chanzo:Shaffihdauda
No comments:
Post a Comment