Tuesday, 24 June 2014

Anguko Maradona baada ya mechi na Nigeria...



Chini ya Diego Maradona Argentina ilifika fainali za kombe la dunia 1990. Na baada ya hapo Maradona akaanza kuporomoka taratibu. Alianza kwa kufungiwa miezi 15 kwa kuonekana kwa chembechembe za kokaini kwenye damu yake.
Na mwaka 1994, baada ya kufunga bao murua dhidi ya Ugiriki, wapenzi wa soka tukaamini kuwa Maradona amerudi kwenye kiwango chake. Lakini, baada ya mechi na Nigeria ikagundulika kuwa Maradona ametumia vidonge vya kuongeza nguvu aina ya Efedrin.
Na hapo ikawa anguko kuu la Maradona.
Maggid.(P.T)

No comments:

Post a Comment