
POLISI
imetangaza operesheni nchi nzima ya kukamata madereva wa pikipiki
(bodaboda), wasiofuata sheria za usalama barabarani, wakiwemo wanaopita
taa nyekundu bila kuruhusiwa.
Msemaji
wa Jeshi la Polisi, Advera Senso alitoa tamko jijini Dar es Salaam jana
wakati akizungumza na waandishi wa habari.Licha ya operesheni kulenga
kudhibiti madereva wa vyombo hivyo wanaopita taa nyekundu, makosa
mengine yatakayosababisha sheria kuchukua mkondo wake ni kutozingatia
alama na michoro ya usalama barabarani.
No comments:
Post a Comment